Sharti la Serikali kuleta cheti cha kusomea uchungaji ili kufungua kanisa (nimeikuta facebook)

Kitchener

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
13,833
Reaction score
27,753
Kuna mdau mlokole mwenzangu nimekuta amesambaza lalamiko hili kule facebook, limenichoma sana. Nitahighlight maeneo ambayo nimeona kuna ukweli mzito.

ANASEMA HIVI;

1. Kwanza kabisa, napenda kuufahamisha umma kwamba, mimi sio mchungaji, ila ninasali.

2. serikali ya Tanzania haimtambui mtu kama mchungaji afungue taasisi ya kidini, kusajili ndoa au hata kufungua kanisa kama hajasoma chuo cha uchungaji. Ni wazi serikali ilikuwa na nia njema ya kudhibiti utapeli kupitia dini, hivyo mtu alete cheti kuthibitisha kuwa yeye ni msomi wa hiyo imani yake na ni kwa misingi hiyo anaenda kufungua kanisa au kuwa mchungaji. HOJA NI WHETHER HII HIMEFANYA KAZI? HII IMESAIDIA KUPUNGUZA UTAPELI NA UONGO?

3. Kanisa la kwanza, ni kanisa la Mitume (na sio hili katoliki), Watu walijazwa na kutembea na Roho Mtakatifu, ilifika mahali Filipo alipomhubiria towashi wa Kushi, alipomaliza alinyakuliwa na Roho toka sehemu ile akaenda kuonekana Samaria, ni sawa na wewe utoweke machoni pa watu uonekane mkoa mwingine sasaivi kwa namna walivyotembea na Roho (nimeweka katoliki hapo ili kuweka record sawa,huwezi kuta Roho katoliki akijionyesha hivyo, na sisemi kwa nia mbaya I am trying to be honest kwa nia njema tu);

WAEFESO 2:20-22 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho. Hii maana yake, katika kanisa la kwanza huwezi kukuta wanauza maji au mafuta ya upako, huwezi kuta wanauza chupi za upako, kuleta nywele za utosi, na utapeli wooote huu.

4. Kanisa la kwanza huwezi kuta mchungaji mwenye cheti cha uchungaji, aposto au nabii, anawafundisha waumini kwamba, mnatakiwa kutoa makafara ya kuku, kondoo na kuchinja wanyama umwage damu ili utajirike, jambo ambalo hata mashehe wamechukizwa nalo. Kuna mchungaji mmoja alikuwa muislam hapo dsm, akabadili dini, akaenda kusoma uchungaji akapata cheti, pamoja na kwamba ni msomi wa dini ya kikristo, lakini anafundisha watu kuchinja ili watoe kafara, anafundisha watu kuwa huwezi kuacha uzinzi, kwamba huwezi kumwamini mkeo, na anafundisha mapotofu. Je? Kipimo cha kuwa na cheti ambacho serikali iliweka, kinaona huyu ni bora kuliko ambao hawajasoma lakini walikuwa wanafundisha kuwa Kafara letu ni Damu ya Yesu Kristo tu, hatutakiwi kuchinja ili tupate pesa kama uganga wa kienyeji.

5. Kama kuna wachungaji wenye vyeti, lakini bado wanauza injili, wanaelekeza watu wachinje wanyama kumwaga damu ili wapate pesa na utajiri, wanapiga pesa waziwazi, hii imesaidia au haijasaidia?

6. Hoja kuu hapa ni je? Mbona pamoja na kuweka condition hiyo, wameibuka matapeli wengi zaidi wenye vyeti? Imesaidia? Inatakiwa kuendelea kuwepo au mambo hayo ya nani ni mchungaji au nani sio wayaache kwa Mungu mwenyewe na kwenye uongozi wa taasisi (eg. Wakatoliki wana viwango vyao nani ni padre, Lutheran wana viwango vyao vya kumtambua mtu kama mchungaji, Makanisa ya kipentekoste yana viwango vyao n.k au hata hao wasiwe ndio kipimo).

7. Kwani, mfano, mimi nikiitwa na Mungu, anaefanya kazi ni mimi au Mungu aliye ndani yangu ndiye ananiwezesha? Hiyo itanilazimu kusoma ili niwaonyeshe cheti kwanza ndio mniruhusu au naweza kuruhusiwa kuanzisha ila niwe najijenga mwenyewe kusoma Biblia na pengine hata kwenda kwenye uchungaji? Kwanini cheti kiwe kigezo wakati Mungu aliyeniita hakuwa na hiyo condition ila aliamua yeye kunichagua hivyo hivyo bila kuwa na cheti? Mungu kanichagua bila cheti afu wewe mwanadamu tena usie hata na Mungu unizuie kwa kigezo cha cheti?

8. Mimi mfano, tangu mdogo nasoma Biblia, hiyo Bible nimeshaisoma yote mara kadhaa, ni mtu wa kuhubiriwa tangu udogo hadi ukubwa, halafu leo uje useme nahitaji cheti? Kwani kwenye cheti wanafundisha nini? Si namna ya kumanage kanisa, historia ya kanisa etc kuna kuwa na course kadhaa na wewe unachagua moja tu, kama ilivyo kwenye secular, unaweza kwenda chuo ukachagua kusoma sheria na mwingine uchumi, wewe uliyesoma sheria hata kama una degree lakini you are too ignorant kwenye mambo ya uchumi ambayo haaujasomea, na je? Sasa kwenye uchungaji nako si unachagua course moja tu zingine bado hutakuwa vizuri nazo? Kuna umuhimu wa cheti ili uwe mchungaji? Mimi nasema NOOOO!

9. Petro, pamoja na kwamba alizunguka na Yesu miaka 3, lakini alikuwa mvuvi kabisa, hakuwa msomi wa sheria za dini kama Paulo na wengine, yeye alikuwa ni regular synagogue goer kama waumini wengine wa kawaida tu, LAKINI ALIPOSHUKIWA NA ROHO MTAKATIFU, kwa sababu ni Roho ndiye alikuwa anaongea ndani yake, alihubiri siku ya Pentecoste hadi wasomi wa dini wakapondeka mioyo na siku moja waliokoka watu 3,000. Stefano naye alikuwa mwanafunzi wa kawaida tu na akiwa amejaa Roho Mtakatifu aliwahubiria wasomi wa dini ya kiyahudi akieleza kuanzia historia ya Ibrahim hadi Yesu, wakachomwa mioyo yao. Hawa wote hawakuwa wasomi.
10. Ukweli ni kwamba, serikali ambayo haimjui Mungu, watendaji wake wengi wana mahirizi viunoni, wala rushwa, na wenye dhambi, hawana moral authority kumchagulia Mungu nani awe mtumishi wake na nani asiwe mtumishi wake, MUNGU HUMCHAGUA YEYE YULE AMTAKAYE, HUMREHEMU YEYE YULE AMTAKAYE NA HUWEZI KUMUULIZA KITU, NI YEYE AMEAMUA.

11. Jambo lingine, Mungu alivyo, huwa hamchagui yule aliyekamilika, yule unayemwona ni msomi na mwenye hekima ya dunia hii, 1 WAKORINTHO 1:27 – 31 INASEMA; Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; Tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; Mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; Kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

12. NB: yote niliyoandika, simaanishi kwamba vyuo vya Biblia ni vibaya, hapana, hata kipindi cha Eliya Mtishbi ukisikia kuwa kulikuwa na wana wa manabii waliokuwa wanafundishwa maana yake kulikuwa na chuo cha kufundisha watu Neno la Mungu. NI muhimu, lakini, kuna umuhimu wa kuweka limit hadi mtu asome hata kama ameitwa na Mungu? Kuna wengi wameitwa, wana Nguvu za Mungu lakini hawawezi kuendelea huduma ya Kimungu kwa kuzuiwa na serikali ambayo imewapa vibali waganga wa kienyeji wanauza madawa ya kichawi na uaguzi huko lakini kwa Mungu wanaweka vizingiti;

13. Pia, wengi wanalalamika kwamba, mbona kuna double standard? Mfano, hao wanaouza mafuta na maji n.k mbona tunawajua wengi tu ni darasa la saba na hajawahi kusoma, isipokuwa ni wale wanajipendekeza kwa serikali? Kwa nini hao mmewakubali kufungua makanisa, na tunayaona wanayofundisha raia ni mapotofu na utapeli, ila kwa sababu wapo karibu na serikali mmewaacha?

14. Je? Hii condition imesaidia kupunguza wachungaji matapeli au imezuia zaidi wale wa kweli walioitwa na Mungu wasiingie kwenye huduma?

15. Solution ni nini? Sio kwamba serikali iwaruhusu tu wote lakini iwe inawamonita nyendo zao?

HAYA,WAPENDA WALOKOLE NA WAPINGA WALOKOLE MNASEMAJE HAPO?
 
Je, ni kweli kwamba serikali ya Tanzania haimtambui mtu kama mchungaji afungue taasisi ya kidini, kusajili ndoa au hata kufungua kanisa kama hajasoma chuo cha uchungaji?

Kwa sheria gani?
 
Wanakuja subiri Mimi sina TOFAUTI na Yule mwamba aliyedandia chopa.ukinipa ela Tu nako nyuma yako.
 
Sio cheti tu makanisa yanapaswa kulipa kodi , hiyo biashara yao inainyima serikali mapato makubwa sana.
Kulazimisha cheti ili mtu awe mchungaji, katika nchi yenye uhuru wa kikatiba wa kuabudu, ni kuvunja uhuru wa kikatiba.

Kwani Yesu alikuwa na cheti gani?
 
Je, ni kweli kwamba serikali ya Tanzania haimtambui mtu kama mchungaji afungue taasisi ya kidini, kusajili ndoa au hata kufungua kanisa kama hajasoma chuo cha uchungaji?

Kwa sheria gani?
ni kweli, ukienda kusajili kanisa pale, utatakiwa kuonyesha cheti, au taasisi ya mlengo wako. na hiki ndicho kimemfanya yule mchungaji wa mbeya hadi leo anaichukia serikali na amekuwa adui wa serikali, na ni kwa sababu ameapa kwamba hatasoma kwa sababu kuitwa na Mungu sio kusomea.

sema mwandishi huyu kule facebook kamlenga sana prophet IBM anayefundisha msaafu kanisani, ila ningekuwa mimi ningetoa mfano wa CHIFU GODLOVE pedeshee ambaye inasemekana ana cheti cha uchungaji na anatarajia kufungua kanisa. akienda pale mambo ya ndani, hawatakuwa na sababu za kumzuia kwa sababu ana cheti cha uchungaji.
 
Kulazimisha cheti ni ujinga tu.

Unaona sasa, kama kuwapiga watu huyo ana cheti na bado anawapiga watu.
 
Kulazimisha cheti ili mtu awe mchungaji, katika nchi yenye uhuru wa kikatiba wa kuabudu, ni kuvunja uhuru wa kikatiba.

Kwani Yesu alikuwa na cheti gani?
chief godlove ana cheti cha uchungaji na ana qualify. ila kuna wengine wameitwa hawapo kama yeye but watazuiwa kwa sababu hawana cheti. imenifikirisha sana, na wakati uo huo waganga wa kienyeji wanapewa vyeti kwenye tiba silia, ila watu wa Mungu wanazuiwa.
 
Hayo mambo ya kulazimisha vyeti kwa wachungaji ni uvivu wa kufikiri tu.

Ukishaweka uhuru wa kuabudu kikatiba maana yake watu wakimtaka mchungaji asiye na cheti waweze kuwa naye.

Ukilazimisha mchungaji awe na cheti kilichopitishwa na serikali hapo ndiyo mwanzo wa kuweka dini ya serikali.
 
Hayo mambo ya kulazinisha vyeti kwa wachungaji ni uvivu wa kufikiri tu.

Ukishaweka uhuru wa kuabudu kikatiba maana yake watu wakimtaka mchungaji asiye na cheti waweze kuwa naye.

Ukilazimisha mchungaji awe na cheti kilichopitishwa na serikali hapo ndiyo mwanzo wa kuweka dini ya serikali.
nadhani serikali inapaswa kulifikiria hili mara ya pili.
 
Kulazimisha cheti ili mtu awe mchungaji, katika nchi yenye uhuru wa kikatiba wa kuabudu, ni kuvunja uhuru wa kikatiba.

Kwani Yesu alikuwa na cheti gani?
Naunga mkono hoja . Ila hawa watu nafikiri wangepaswa kulipa kodi tu🤔
 
kuna hoja hapo mwamba kasema, kama mtu ameitwa na Mungu akahubiri, mtu huyo amekuwa akihudhuria church anafundishwa kila week maisha yake yote, ni kitu gani asichokijua? na anasema, kwani chuoni watakufundisha yote, si kozi moja tu huwezi kusoma kila kitu cha kuendeshea kanisa? Ukweli ni kwamba, wapo wachungaji wanatumia sana mwanya huo kuibia waumini, lakini nakubaliana naye kwamba, hata wakipata vyeti haiwazuii kutapeli wananchi, na wewe selikali huwezi kuchuja nani au nani asiwe mchungaji hata wale aliowaita Mungu kikweli. serikali iliyojaa watu waovu inachuja maamuzi ya Mungu kwa mtu.
 
nadhani serikali inapaswa kulifikiria hili mara ya pili.
Mimi mpaka sasa sijakubali kwamba serikali inalazimisha vyeti mpaka nioneshwe sheria au kanuni hiyo.

Haya mambo mengine ni uelewa wa watu tu.

Mimi nilikuwa na babu yangu mmoja mzee alikuwa ana kanisa lake. Alikuwa anaitwa mpaka Ikulu na Mwinyi wakati rais akikaa na viongozi wa makanisa.

Yule mzee hakuwa na cheti chochote.

Haya mambo yameanza lini?
 
alichosema ni cha kweli. kama hauamini, nenda wewe pale kajifanye unafungua kanisa (dhehebu) ndio utajua ukweli. ila mwamposa, kuhani hawana vyeti, ila wana madhehebu. hata lusekelo hana cheti. ila haguswi.
 
Naunga mkono hoja . Ila hawa watu nafikiri wangepaswa kulipa kodi tu🤔
Kuna historia kubwa sana iliyopelekea dhana nzima ya separation of church and state.

Makanisa na nyumba za ibada nyingine yalitetewa kama sehemu maalum za jamii. Kadiri miaka inavyoenda, umaalum huo unapotea.

Kuna hoja za kusema makanisa na taasisi za kidini zilipe kodi, pia kuna hoja za kupinga dhana hii.

Hoja za kutaka kodi kwa taasisi za kidini ni pamoja na.

1. Usawa chini ya sheria. Sheria inataka kila mtu na taasisi ziwe sawa chini ya sheria. Ukipanga kodi kwa taasisi zisizo za kidini na kuondoa kodi hizo kwa taasisi za kidini, umeondoa usawa na kuweka upendeleo kwa taasisi za kidini.

2. Kuongeza mapato kwa serikali. Serikali ikitoza kodi taasisi za kidini, itaongeza mapato.

3. Uwazi na uwajibikaji. Kutoza kodi taasisi za kidini kutaongeza uwazi na uwajibikaji. Sasa hivi ni rahisi sana watu kufanya money laundry kwenye taasisi za kidini kwa sababu hazitoi kodi wala kuwa audited.

Hoja dhidi ya kutaka taasisi za kidini zitoe kodi.

1. Separation of religion and state. Kuna watu wanaona kutoza kodi taasisi za kidini kutaingilia uhuru wa dini na serikaki inaweza kutumia kodi kunyamazisha taasisi za dini zisiikemee inavyotakiwa.

2. Kazi za kijamii nyingi ambazo taasisi za dini inazifanya bila kutafuta faida zitaingiliwa ikiwa taasisi za dini zitatakiwa zitoe kodi.

3. Uhuru wa watu kuabudu wanavyotaka unaweza kuingiliwa ikiwa taasisi zao za kidini zitatakiwa watoe kodi.

Kuna namna ya kufanya shughuli fulani za taasisi za kidini zitozwe kodi, na shughuli nyingine ambazo zinaonekana kuisaidia jamii na kufanywa bila kuangalia faida ya kifedha kwa taasisi ya kidini (mfano shule na hospitali za kidini ambazo zipo kuhudumia jamii na si kupata faida ya kifedha), ziachwe bila kutozwa kodi.
 
alichosema ni cha kweli. kama hauamini, nenda wewe pale kajifanye unafungua kanisa (dhehebu) ndio utajua ukweli. ila mwamposa, kuhani hawana vyeti, ila wana madhehebu. hata lusekelo hana cheti. ila haguswi.
Hapa tunajadili mfumo rasmi ulivyo au matatizo yanayofanya mfumo rasmi usifuatwe?

Kuna mtu ana sheria au kanuni inayolazimisha mtu anayetaka kufungua kanisa lake awe na cheti cha masomo ya uchungaji?

Mnaweza kuweka hiyo sheria au kanuni hapa?

Vipi nikitaka kuanzisha "Kanisa La Kupinga Mafarisayo" na kusema mchungaji anaongozwa na Roho Mtakatifu, habari za vyeti ni Ufarisayo tu?

Hamuoni kuwa hapo mkinilazimisha niwe na cheti ili kufungua kanisa langu, wakati mimi imani yangu ni kuwa kupata cheti ni Ufarisayo tu, naongozwa na Roho Mtakatifu, mtakuwa mmeniingikia uhuru wangu wa kuabudu?
 
Kuna mdau mlokole mwenzangu nimekuta amesambaza lalamiko hili kule facebook, limenichoma sana. Nitahighlight maeneo ambayo nimeona kuna ukweli mzito.

ANASEMA HIVI;

1. Kwanza kabisa, napenda kuufahamisha umma kwamba, mimi sio mchungaji, ila ninasali.

2. serikali ya Tanzania haimtambui mtu kama mchungaji afungue taasisi ya kidini, kusajili ndoa au hata kufungua kanisa kama hajasoma chuo cha uchungaji. Ni wazi serikali ilikuwa na nia njema ya kudhibiti utapeli kupitia dini, hivyo mtu alete cheti kuthibitisha kuwa yeye ni msomi wa hiyo imani yake na ni kwa misingi hiyo anaenda kufungua kanisa au kuwa mchungaji. HOJA NI WHETHER HII HIMEFANYA KAZI? HII IMESAIDIA KUPUNGUZA UTAPELI NA UONGO?

3. Kanisa la kwanza, ni kanisa la Mitume (na sio hili katoliki), Watu walijazwa na kutembea na Roho Mtakatifu, ilifika mahali Filipo alipomhubiria towashi wa Kushi, alipomaliza alinyakuliwa na Roho toka sehemu ile akaenda kuonekana Samaria, ni sawa na wewe utoweke machoni pa watu uonekane mkoa mwingine sasaivi kwa namna walivyotembea na Roho (nimeweka katoliki hapo ili kuweka record sawa,huwezi kuta Roho katoliki akijionyesha hivyo, na sisemi kwa nia mbaya I am trying to be honest kwa nia njema tu);

WAEFESO 2:20-22 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho. Hii maana yake, katika kanisa la kwanza huwezi kukuta wanauza maji au mafuta ya upako, huwezi kuta wanauza chupi za upako, kuleta nywele za utosi, na utapeli wooote huu.

4. Kanisa la kwanza huwezi kuta mchungaji mwenye cheti cha uchungaji, aposto au nabii, anawafundisha waumini kwamba, mnatakiwa kutoa makafara ya kuku, kondoo na kuchinja wanyama umwage damu ili utajirike, jambo ambalo hata mashehe wamechukizwa nalo. Kuna mchungaji mmoja alikuwa muislam hapo dsm, akabadili dini, akaenda kusoma uchungaji akapata cheti, pamoja na kwamba ni msomi wa dini ya kikristo, lakini anafundisha watu kuchinja ili watoe kafara, anafundisha watu kuwa huwezi kuacha uzinzi, kwamba huwezi kumwamini mkeo, na anafundisha mapotofu. Je? Kipimo cha kuwa na cheti ambacho serikali iliweka, kinaona huyu ni bora kuliko ambao hawajasoma lakini walikuwa wanafundisha kuwa Kafara letu ni Damu ya Yesu Kristo tu, hatutakiwi kuchinja ili tupate pesa kama uganga wa kienyeji.

5. Kama kuna wachungaji wenye vyeti, lakini bado wanauza injili, wanaelekeza watu wachinje wanyama kumwaga damu ili wapate pesa na utajiri, wanapiga pesa waziwazi, hii imesaidia au haijasaidia?

6. Hoja kuu hapa ni je? Mbona pamoja na kuweka condition hiyo, wameibuka matapeli wengi zaidi wenye vyeti? Imesaidia? Inatakiwa kuendelea kuwepo au mambo hayo ya nani ni mchungaji au nani sio wayaache kwa Mungu mwenyewe na kwenye uongozi wa taasisi (eg. Wakatoliki wana viwango vyao nani ni padre, Lutheran wana viwango vyao vya kumtambua mtu kama mchungaji, Makanisa ya kipentekoste yana viwango vyao n.k au hata hao wasiwe ndio kipimo).

7. Kwani, mfano, mimi nikiitwa na Mungu, anaefanya kazi ni mimi au Mungu aliye ndani yangu ndiye ananiwezesha? Hiyo itanilazimu kusoma ili niwaonyeshe cheti kwanza ndio mniruhusu au naweza kuruhusiwa kuanzisha ila niwe najijenga mwenyewe kusoma Biblia na pengine hata kwenda kwenye uchungaji? Kwanini cheti kiwe kigezo wakati Mungu aliyeniita hakuwa na hiyo condition ila aliamua yeye kunichagua hivyo hivyo bila kuwa na cheti? Mungu kanichagua bila cheti afu wewe mwanadamu tena usie hata na Mungu unizuie kwa kigezo cha cheti?

8. Mimi mfano, tangu mdogo nasoma Biblia, hiyo Bible nimeshaisoma yote mara kadhaa, ni mtu wa kuhubiriwa tangu udogo hadi ukubwa, halafu leo uje useme nahitaji cheti? Kwani kwenye cheti wanafundisha nini? Si namna ya kumanage kanisa, historia ya kanisa etc kuna kuwa na course kadhaa na wewe unachagua moja tu, kama ilivyo kwenye secular, unaweza kwenda chuo ukachagua kusoma sheria na mwingine uchumi, wewe uliyesoma sheria hata kama una degree lakini you are too ignorant kwenye mambo ya uchumi ambayo haaujasomea, na je? Sasa kwenye uchungaji nako si unachagua course moja tu zingine bado hutakuwa vizuri nazo? Kuna umuhimu wa cheti ili uwe mchungaji? Mimi nasema NOOOO!

9. Petro, pamoja na kwamba alizunguka na Yesu miaka 3, lakini alikuwa mvuvi kabisa, hakuwa msomi wa sheria za dini kama Paulo na wengine, yeye alikuwa ni regular synagogue goer kama waumini wengine wa kawaida tu, LAKINI ALIPOSHUKIWA NA ROHO MTAKATIFU, kwa sababu ni Roho ndiye alikuwa anaongea ndani yake, alihubiri siku ya Pentecoste hadi wasomi wa dini wakapondeka mioyo na siku moja waliokoka watu 3,000. Stefano naye alikuwa mwanafunzi wa kawaida tu na akiwa amejaa Roho Mtakatifu aliwahubiria wasomi wa dini ya kiyahudi akieleza kuanzia historia ya Ibrahim hadi Yesu, wakachomwa mioyo yao. Hawa wote hawakuwa wasomi.
10. Ukweli ni kwamba, serikali ambayo haimjui Mungu, watendaji wake wengi wana mahirizi viunoni, wala rushwa, na wenye dhambi, hawana moral authority kumchagulia Mungu nani awe mtumishi wake na nani asiwe mtumishi wake, MUNGU HUMCHAGUA YEYE YULE AMTAKAYE, HUMREHEMU YEYE YULE AMTAKAYE NA HUWEZI KUMUULIZA KITU, NI YEYE AMEAMUA.

11. Jambo lingine, Mungu alivyo, huwa hamchagui yule aliyekamilika, yule unayemwona ni msomi na mwenye hekima ya dunia hii, 1 WAKORINTHO 1:27 – 31 INASEMA; Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; Tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; Mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; Kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

12. NB: yote niliyoandika, simaanishi kwamba vyuo vya Biblia ni vibaya, hapana, hata kipindi cha Eliya Mtishbi ukisikia kuwa kulikuwa na wana wa manabii waliokuwa wanafundishwa maana yake kulikuwa na chuo cha kufundisha watu Neno la Mungu. NI muhimu, lakini, kuna umuhimu wa kuweka limit hadi mtu asome hata kama ameitwa na Mungu? Kuna wengi wameitwa, wana Nguvu za Mungu lakini hawawezi kuendelea huduma ya Kimungu kwa kuzuiwa na serikali ambayo imewapa vibali waganga wa kienyeji wanauza madawa ya kichawi na uaguzi huko lakini kwa Mungu wanaweka vizingiti;

13. Pia, wengi wanalalamika kwamba, mbona kuna double standard? Mfano, hao wanaouza mafuta na maji n.k mbona tunawajua wengi tu ni darasa la saba na hajawahi kusoma, isipokuwa ni wale wanajipendekeza kwa serikali? Kwa nini hao mmewakubali kufungua makanisa, na tunayaona wanayofundisha raia ni mapotofu na utapeli, ila kwa sababu wapo karibu na serikali mmewaacha?

14. Je? Hii condition imesaidia kupunguza wachungaji matapeli au imezuia zaidi wale wa kweli walioitwa na Mungu wasiingie kwenye huduma?

15. Solution ni nini? Sio kwamba serikali iwaruhusu tu wote lakini iwe inawamonita nyendo zao?

HAYA,WAPENDA WALOKOLE NA WAPINGA WALOKOLE MNASEMAJE HAPO?

Ngoja waisiraeli MK254 au Eli Cohen wajomba zake Mungu kutokea Goba watuletee mwongozo kwanza.
 
Hapa tunajadili mfumo rasmi ulivyo au matatizo yanayofanya mfumo rasmi usifuatwe?

Kuna mtu ana sheria au kanuni inayolazimisha mtu anayetaka kufungua kanisa lake awe na cheti cha masomo ya uchungaji?

Mnaweza kuweka hiyo sheria au kanuni hapa?

Vipi nikitaka kuanzisha "Kanisa La Kupinga Mafarisayo" na kusema mchungaji anaongozwa na Roho Mtakatifu, habari za vyeti ni Ufarisayo tu?

Hamuoni kuwa hapo mkinilazimisha niwe na cheti ili kufungua kanisa langu, wakati mimi imani yangu ni kuwa kupata cheti ni Ufarisayo tu, naongozwa na Roho Mtakatifu, mtakuwa mmeniingikia uhuru wangu wa kuabudu?
ni kanuni ndugu, zilizotungwa kwa mujibu wa sheria ya ufunguaji wa taasisi bila shaka kama sikosei. pia, jamaa kanikumbusha pakubwa kwa sababu hata mimi kuna raia kibao walipojua ni mwanasheria, wamekuwa wakiniuliza hili swali na kama nini wafanye, kwa sababu wana wito, Mungu kawaita ila amewaita bila cheti; kwa hiyo ni sawa na mwanadamu analimiti kile Mungu ameweka kwa mtu, kanuni zilitungwa kwa lengo la kudhibiti makanisa yanayoibuka kama uyoga, na waliohamasisha ziwepo walikuwa wapinzani na jambo hilo hivyo walikuwa biased nadhani, walisahau kuwa kuna uhuru wa kuabudu kwenye katiba, na kwamba unachoamini wewe sio lazima mimi nikiamini kwa sababu hii ni secular state, na pia, wakati unazuia makanisa, upande wa pili unatoa vibali kwa wapiga ramli waganga wa kienyeji ambao wanapiga sana watu. sasa labda watunga sheria iliyopelekea hiyo kanuni ni wateja wa waganga wa kienyeji ndio maana wanawapa vibali na hawaoni shida, mganga wa kienyeji hahitaji chetu cha kupigia ramli, ila mchungaji aliyeitwa na Mungu anahitaji cheti. mwanadamu anachuja takwa la Mungu kwa mtu.
 
Back
Top Bottom