Sharti la Serikali kuleta cheti cha kusomea uchungaji ili kufungua kanisa (nimeikuta facebook)

Sharti la Serikali kuleta cheti cha kusomea uchungaji ili kufungua kanisa (nimeikuta facebook)

Kwa nini kila mtu anataka aanzishe kanisa au huduma yake binafsi?.

Mkifanya huduma chini ya taasisi inayowalea, mnahisi hamtakuwa maarufu au kupata maokoto ya kutosha?

Hiyo roho ya utengano ambayo inamea kila kukicha imetoka kweli kwa Yehova?

Haiwezekani kuendelea na injili kama afanyavyo Mwakasege huku akiwa chini ya uangalizi wa kanisa mama?.

Huu utaratibu wa utengano kutoka kwenye madhehebu yanayojiita ya kiroho ndo umetuletea akina "kiboko ya wachawi, wauza vifaa vya upako na wagaganga wengine wa kienyeji wajiitao manabii na mitume"

Yesu Anakuja
 
ni kanuni ndugu, zilizotungwa kwa mujibu wa sheria ya ufunguaji wa taasisi bila shaka kama sikosei. pia, jamaa kanikumbusha pakubwa kwa sababu hata mimi kuna raia kibao walipojua ni mwanasheria, wamekuwa wakiniuliza hili swali na kama nini wafanye, kwa sababu wana wito, Mungu kawaita ila amewaita bila cheti; kwa hiyo ni sawa na mwanadamu analimiti kile Mungu ameweka kwa mtu, kanuni zilitungwa kwa lengo la kudhibiti makanisa yanayoibuka kama uyoga, na waliohamasisha ziwepo walikuwa wapinzani na jambo hilo hivyo walikuwa biased nadhani, walisahau kuwa kuna uhuru wa kuabudu kwenye katiba, na kwamba unachoamini wewe sio lazima mimi nikiamini kwa sababu hii ni secular state, na pia, wakati unazuia makanisa, upande wa pili unatoa vibali kwa wapiga ramli waganga wa kienyeji ambao wanapiga sana watu. sasa labda watunga sheria iliyopelekea hiyo kanuni ni wateja wa waganga wa kienyeji ndio maana wanawapa vibali na hawaoni shida, mganga wa kienyeji hahitaji chetu cha kupigia ramli, ila mchungaji aliyeitwa na Mungu anahitaji cheti. mwanadamu anachuja takwa la Mungu kwa mtu.
Kanuni hiyo iko wapi? Unaweza kuiweka hapa?

Na kwa nini isiwe kinyume na katiba kwa kuingilia watu uhuru wao wa kuabudu, na haki yao ya kibinadamu ya kuabudu wanavyotaka, na hivyo kuwa batili?
 
Kwa nini kila mtu anataka aanzishe kanisa au huduma yake binafsi?.

Mkifanya huduma chini ya taasisi inayowalea, mnahisi hamtakuwa maarufu au kupata maokoto ya kutosha?

Hiyo roho ya utengano ambayo inamea kila kukicha imetoka kweli kwa Yehova?

Haiwezekani kuendelea na injili kama afanyavyo Mwakasege huku akiwa chini ya uangalizi wa kanisa mama?.
kwa sababu hata hizi zilizopo zilianza hivyo hivyo na zingezuiwa zisingekuwepo. mfano mimi kama mwanasheria, ningesema niache uanasheria, niwe mchungaji, hautakiwi kunichagulia pa kuchungia, pengine sitaki kuwa mrutheran hivyo usinilazimishe nikawe mchungaji wa lutheran, pengine sipendi kuwa TAG au kanisa lolote la pentekoste hata kama mlango nitakuwa nao wa aina yao lakini sitaki niwe chini ya taasisi yao kwa sababu wana taasisi na katiba zenye vipengele ambavyo mimi naweza nisipende, it is unfair kunilazimisha nijiunge nao au la nilete cheti ili uniruhusu nifungue ya jina lango. pia, katiba inaruhusu uhuru wa kuabudu, sio dhambi kufungua dhehebu, watakaoenda motoni ni wenye dhambi sio wanaofungua madhehebu hata yangekuwa milioni.
 
Kanuni hiyo iko wapi? Unaweza kuiweka hapa?

Na kwa nini isiwe kinyume na katiba kwa kuingilia watu uhuru wao wa kuabudu, na haki yao ya kibinadamu ya kuabudu wanavyotaka, na hivyo kuwa batili?
ni kwamba unabisha kwamba hizo kanuni na taratibu hazipo au unataka tuziweke kanuni hapa ili tuzijadili. kilichobaki hapa ni kutafuta kanuni tu tuziweke hapa ila hoja hii ni ya kweli na binafsi nawafahamu wengi wamekwamia hapo.
 
chief godlove ana cheti cha uchungaji na ana qualify. ila kuna wengine wameitwa hawapo kama yeye but watazuiwa kwa sababu hawana cheti. imenifikirisha sana, na wakati uo huo waganga wa kienyeji wanapewa vyeti kwenye tiba silia, ila watu wa Mungu wanazuiwa.
Watu wa Mungu hao matapeli!?
 
Mimi mpaka sasa sijakubali kwamba serikali inalazimisha vyeti mpaka nioneshwe sheria au kanuni hiyo.

Haya mambo mengine ni uelewa wa watu tu.

Mimi nilikuwa na babu yangu mmoja mzee alikuwa ana kanisa lake. Alikuwa anaitwa mpaka Ikulu na Mwinyi wakati rais akikaa na viongozi wa makanisa.

Yule mzee hakuwa na cheti chochote.

Haya mambo yameanza lini?
Tangu mwinyi aondoke madarakani ni miaka 30 sasa
 
Watu wa Mungu hao matapeli!?
kwa hiyo wewe kwako kukiwa na waovu wawili au kadhaa kwenye aina ya watu hao basi unaamini wote ni hawalifu? ivi unajua hata sisi tunachukia na kupinga huo upigaji lakini tupo kwa walokole. shida ni kwamba wanaotafutwa hapa ni walokole, hao wauza mafuta wamejivika tu jina kuwa ni walokole na wanatuponza sana tuonekana hatufai kumbe sisi tupo safi tu, na kwenye umoja wetu hawapo ila wanajifanya walokole ili wapige pesa. kingine, kama hao ni waovu mbona waganga wa kienyeji ya wapiga ramli mnawapa vibali?
 
Kuzuwia watu kwenda hospital kupata tiba,kutibu magonjwa yote kwa maombi..ni utapeli,uganga ni suala jingine na ramli zao,na ulokole hauthibitishwi na wewe na genge lako,madam wauza mafuta,watoa mapepo,watibu ukimwi kwa jina la yesu wanasema ni walokole basi ni walokole
 
ni kwamba unabisha kwamba hizo kanuni na taratibu hazipo au unataka tuziweke kanuni hapa ili tuzijadili. kilichobaki hapa ni kutafuta kanuni tu tuziweke hapa ila hoja hii ni ya kweli na binafsi nawafahamu wengi wamekwamia hapo.
Ninataka kujiridhisha kwamba kanuni hizo zipo kwanza, kwamba hili si jambo la watu kutoelewa, kuweka tafsiri mbaya, kwenda na matakwa yenye exception bila kuangalia exception process, au kuangalia ukiritimba wa kiserikali tu kuchukuliwa kuwa ndiyo kanuni.

Sijawahi kuziona na naona kama zipo zinavunja uhuru wa kikatiba na haki za binadamu kwa namna ya msingi sana kiasi cha kustaajabisha.
 
Mbarikiwa mwakipesile hadi ameingia jela na ugomvi wake na serikali ni kutomruhusu afungue dhehebu lake tangu enzi za magufuli hadi kesho. ukipeleka nyaraka pale wanataka upeleke cheti cha uchungaji kwamba umesomea, (nitatafuta sheria au rules nitakuwekea hapa), na hata ukileta, wanataka ulete barua toka kwa kanisa unaloassociate nalo, eg. TAG etc ambako huko utakuwa chini ya mwamvuli wao kwani wao tayari wanaexist na kuna ada utakuwa unawapa hao association kwa sababu wamekutambulisha, ni laki mbili kila mwaka kama sikosei. kwa hio jambo hili lipo kabisa wala sio uongo.
 
Kuzuwia watu kwenda hospital kupata tiba,kutibu magonjwa yote kwa maombi..ni utapeli,uganga ni suala jingine na ramli zao,na ulokole hauthibitishwi na wewe na genge lako,madam wauza mafuta,watoa mapepo,watibu ukimwi kwa jina la yesu wanasema ni walokole basi ni walokole
kwani ni nani amezuia watu wasitibiwe ndugu? wakati hao wanaoomba kusajiliwa dhehebu wanaenda hospitali na hawafundishi kuzuia waumini wasiende.
 
Mbarikiwa mwakipesile hadi ameingia jela na ugomvi wake na serikali ni kutomruhusu afungue dhehebu lake tangu enzi za magufuli hadi kesho. ukipeleka nyaraka pale wanataka upeleke cheti cha uchungaji kwamba umesomea, (nitatafuta sheria au rules nitakuwekea hapa), na hata ukileta, wanataka ulete barua toka kwa kanisa unaloassociate nalo, eg. TAG etc ambako huko utakuwa chini ya mwamvuli wao kwani wao tayari wanaexist na kuna ada utakuwa unawapa hao association kwa sababu wamekinyume na kutambulisha, ni laki mbili kila mwaka kama sikosei. kwa hio jambo hili lipo kabisa wala sio uongo.
Hili jambo ni kuingilia uhuru wa mtu wa kuabudu, ni kinyume na kanuni za separation of religion and state, ni kinyume cha katiba (freedom of conscience) na pia ni kinyume na haki za binadamu kama tulivyozikubali kwa ku ratify Universal Declaration of Human Rights ya December 10 1948.

Mimi sina dini, siamini katika uwapo wa Mungu, lakini nasimamia haki ya kila mtu kuweza kuabudu (au kutoabudu) kama anavyotaka.

Na kwa msingi huo, nitamtetea mtu yeyote anayeamini na kutaka kuanzisha kanisa lake bila ya kuwa na cheti cha uchungaji wala kudhaminiwa na taasisi nyingine yoyote ya kidini aweze kuanzisha hilo kanisa lake.
 
Ndiyo nimeuliza hili jambo limebadilika lini? Kanuni hizi ziko wapi?

Mpaka sasa hazijawekwa hapa.
Kuna kipindi walibadili sheria ya uhuru wa kuabudu ukiambatana na kuhubiri imani, kipindi kile cha mihandhara ya waislam, nafikiri walifika huko kwenye haya madai,mnufaika hapo ni Roma
 
Kuna kipindi walibadili sheria ya uhuru wa kuabudu ukiambatana na kuhubiri imani, kipindi kile cha mihandhara ya waislam, nafikiri walifika huko kwenye haya madai,mnufaika hapo ni Roma
Nimeomba kuona sheria au kanuni ya sasa ilivyoandikwa verbatim niisome mwenyewe.

Mpaka sasa sijaipata.
 
Back
Top Bottom