Tetesi: Sharti Moja kubwa waliopewa viongozi waliofika Ikulu ni hili hapa

Yaani haki za watu za kikatiba zinapokwa mchana kweupe huku wapokwaji wakihalalisha haki zao za msingi kupokwa
Mku soma hapo juu unaambiwa Mbowe alishaenda siku kuu ya Uhuru Mwanza
 
Mazingira na utaratibu uliotumika kukutana na wapinzani unaacha sintofahamu kubwa! Ni hii ndo sababu wengi watakuwa na maoni tofauti na zaidi ya yote kuwa na wasiwasi juu ya kuwepo ajenda ya siri ilopangwa na CCM nyuma yake. Kuna maswali mengi ambayo yanaibua mjadala juu ya mkutano ule wa Rais na baadhi ya viongozi wa upinzani:-
MOSI; Kwanini nini vikao hivi vije baada ya mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM ambayo rais ndio mwenyekiti wake?
PILI;Kwanini Rais aliamua kuitisha mkutano na kiongozi mmoja mmoja badala ya kuwaita viongozi wote wa upinzani kwa wakati mmoja?
TATU: Je kama kweli serikali na CCM ambacho ndicho chama mama wa vyama vyote wana dhamira ya dhati ya kufanya uchaguzi kuwa huru na waki, ni kwanini jambo hili lisitafutiwe dharura na kuruhusu mabadiliko katika sheria za uchaguzi na muundo wa tume ya uchaguzi na badala yake liishie katika kutoa ahadi na matamko?
NNE; Iwapo uchaguzi usipokuwa huru na wa haki, Je waathirika wakaitafute haki wapi?....Maana katiba ya sasa hairuhusu kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya urais hata kama wagombea walioshindwa hawakutendewa haki!

Serikali ikiaandaa mazingira yanayoondoa sintofahamu hii na kujibu maswali haya wananchi wengi tutakuwa tumeelewa vema maana na dhana nzima ya vikao vya Ikulu kuwa havikuwa na principle ya DIVIDE AND RULE!
 

Kwa hali ilivyo, hayoyote yanawezekana, kwani wapinzani wenyewe hawapatani na kila mmoja anachumia tumbo lake. Wamefanya siasa kama biashara na bidhaa inayouzwa ni Chama na wanachama.
 
Sasa kusimamisha wagombea nalo ni jambo la kuambiwa kufanya??

Unafaidika vipi na huu upotoshaji??
 
aka rushwa.
aka mlungula.
aka kitu kidogo.
mahakama ya mafisadi aka futuhi!
 
Bado Ni tetesi, ila ingewezekana Ni vizuri waweke wazi kwa umma..walichozungumza....

Ila alichofanyiwa Mbatia huko Mbeya kinathibitisha kuwapo kwa maridhiano ya jinsi fulani. Time will tell the tale!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Hii tafsiri yako uliyoandika hapa ni uzushi mtupu na propaganda watu wa intelijensia ikilenga kuwaingizia hisia mbaya wapinzani za kutoaminiana. This is calculate dirty job against upinzani, na hasa ikilengwa Chadema.

Tunajua CCM hawaogopi kila chama cha upinzani. Wanaogopa Chadema. Magufuli haogopi upinzani. anaogopa kukutana kwenye uchaguzi na Chadema. Yaani pamoja na wapinzani kukaa kifungoni kisiasa kww miaka 5 bado CCM na Magufuli hawajiamni kushinda bila hila za kijinga kama unazotumia hapa?

Basi kama ndivyo CCM ni dhaifu kuliko watu wanavyodhani, na hii hasa ndiyo hofu yao.
 
Lipumba, Seif, Zitto na Mbatia wajue tu kwamba mpinzani yeyote kati yao ambaye HATAONGELEA MADAI YA TUME HURU YA UCHAGUZI, huyo atakuwa ni msaliti na kwa hakika hasira cha Wananchi zitamrudi kupitia sanduku la kura.
 
Hao wanajirahisisha sana,Zitto ni bonge la mnafiki
Lipumba, Seif, Zitto na Mbatia wajue tu kwamba mpinzani yeyote kati yao ambaye HATAONGELEA MADAI YA TUME HURU YA UCHAGUZI, huyo atakuwa ni msaliti na kwa hakika hasira cha Wananchi zitamrudi kupitia sanduku la kura.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…