Tatizo kubwa mzazi mwenzio alikuwa au amekuweka plan A wakati wewe umemuona yeye ni plan B. Nadhani baada ya nyie kubarikiwa mtoto (hata kama hamkupanga), alijua ndo tayari mtakuwa familia yaani umuoe.
(maana inaelekea condom kwako ni proverb) utamfanyia hivo hivo. .
jamani mnanishutumu kwa kutotumia zana!?
inawezekana ni udhaifu wangu,au niseme ndio kosa kubwa la kwangu!
Sasa mimi kuishi nae kwakweli ni kunilazimisha!because I DON'T LOVE HER FROM MY HEART,ilikuwa ni katika kukata kiu hapa na pale
am telling you by then,i never had any plan!NEITHER A NOR B.nisingependa kuelezea kilichotokea kwakweli kwasababu..................dah!anyaways,AHSANTE KWA USHAURI!the thing is I DON'T LOVE HER!I have tried to in so many ways lakin IT NEVA WORKED
...,fikiria kama ungekuwa umekanyaga mawaya ingekuwa vipi! Udhaifu wako ndio uliokuponza ila sina nia ya kukulaumu. Nadhani wewe umelelewa kwa mapenzi toka kwa baba na mama hivyo ni jukumu lako pia kuhakikisha mnamlea mwanenu kwa mapenzi yote. Jiulize swali..., je nikioa mwanake mwingine mwanangu atapata wapi mapenzi ya dhati? Dont be selfish binti yako anahitaji malezi bora ya wazazi wote wawili.
dada angu,hii nikubali yaishe!UONDOE MKOSI!nakumbuka tulivyofahamiana,ni AIBU!baada ya hapo tuligombana sana TENA SAAANA!akakata mguu kama miezi kadhaa,aliporudi alikuwa na kazi AKALETA MAPOZI YA AJABU,kuonana nae ilikuwa mpaka uandike barua.sasa siku moja niliyokutana nae ilikuwa ST VALENTINE DAY,unajua tena hiyo siku ina 'ushaishi mkubwa' katika mambo hayo,na pia kuna kitu MOB SAIKOLOJI ILINIATHIRI!sasa kama ni shetani au ni mungu SIJUI!YAKATOKEA YA KUTOKEA!Its good kujua upande wako, je upande wa huyo bibie ukoje?Anakupenda inavyoonyesha kwanini akung'ang'anie tu jamani, au kuondoa nuksi tu yaishe?
HILI ALILITAMKA WAZI!Ila anaweza kukuharibia hata huko unakotaka kuoa, yaani mkose wote!
AHSANTE KWA USHAURI!
unajua nin,nimelelewa na nimekua hadi mzazi wangu mmoja akatangulia mbele ya haki,sikuwahi kuona WALA KUSIKIA baba na mama wakigombana.nilikuwa nasikia na kwenda kuamulia ugomvi kwenye ndoa za watu.I BELIEVE THAT BABA ALIISHI NA MTU ALIYEMPENDA!
naomba nieleweke kwamba SITETEI UOVU WANGU!ila kwasababu nimeshakosea hapa mwanzo,na ninajuta sana kwa hilo,NISINGEPENDA KUONA MY KID anakua akiona I AM NOT HAPPY WITH MY MARRIAGE!au akasikia tukifokeana na mama ake!unajua nini,i am about to tell you people WHAT HAPPENED
thank u SHISHI!at least you give me life
Geoff mkuu lazima urogwe kubali yaishe....warombo mademu wao wana vizizi sana utarogwa mashine haitapanda mtungi.....wanaroga hata ukiongea nae kwenye simu kwisha habari yako.....
ushauri hapo mpe live tu mtoto mchukue akigoma abaki nae....ila anza kutafuta mitishamba ya kujilinda..
Geoff mwanakwetu,
Usijunje daraja baada ya kulivuka. Ninavyoona mimi ni mweleze taratibu mzazi mwenzio na nina imani atakuelewa na mtakuwa marafiki wzuri tu ili muweze kumlea mtoto wenu kwa upendo asije akawa mtoto wa mtaani. Ukweli wote mnaujua nyie wenyewe, msifichane muwe wazi mjadili.Inauma sasa pale unapokuwa na mtoto na mzazi mwenzio akakataa kukuoa.na labda ukizingatia mwanamke lazima atakuwa alisacrifice mambo mengi ili kumlea mtoto wenu. We need to appreciate wale wanaotuletea na kutulelea watoto jamani. Kizuri zaidi umepata binti kama mama yake ( think twice). Pili jamani hata hizi ndoa tulizonazo haziko perfect. Ni mara ngapi tumepatwa mawazo laiti ningeolewa na.. au ningemuoa...Yote hii ni kuonyesha kwamba ni lazima tuishi kwa kuvumiliana sana. Muombe Mungu akupe ujasiri wa kukabiliana na yote.
...Ndio maana wanawake wengi siku hizi tunapanga foleni kwa waganga kuwakomesha kwa tabia zenu zisizo na huruma................