M nshamsameehe ila siwezi kuwa wake tena naomba anijibu haya maswalihuyo mama mtoto wake atampeleka wapi wakati kwao tayari anajulikana na mimi nafasi yangu itakuwa wap
Nimekuwa nikiangalia comment za watu hapa,na nikawa na kigugumizi cha kuchangia
moreen baby sasa unaongea,na asante kwa hatua hii!
Sasa naomba huu mjadala ufungwe uhamie pm na kwenye simu zenu!
Kuna baba aliwahi piga simu kituo cha redio live akasema,popote ulipo (akataja jina) elewa nakupenda sana naomba uwe mke wangu naye akataja majina yake.Yule mwanamke by coincidence alisikia hiyo short msg live,na kweli walirudiana!
Kitendo alichokifanya
uran leo ni cha kishujaa na ujasiri kwa wanaume wa siku hizi,nkupongeza sana
uran kwa kukubali kutunza na kulea kiumbe chako,hiyo tu inaonyesha ulivyo mwanaume wa namna gani!
moreen baby lione hilo,,kaa naye,mzungumze muweke misingi ya hayo maswali yako ya msingi yanajibiwa vipi na mtafanya nini!!Wahenga wanasema,"Mpende akupendaye
moreen,
uran anakupenda,hivyo ni wewe kulipokea pendo lake!
Sisi wote ni binadamu na wala sio malaika,tunafanya makosa,pengine kwa kutodhamiria kama ilivyotokea kwa
uran!Cha msingi ni kukubali kuwa umekosa na kuomba msamaha,na kuahidi kutorudia kuyafanya hayo!Kwa wanaume tulio wengi,kuomba msamaha na kunyenyekea kwa mkeo ni shughuli pevu,sana sana atajifanya anakununulia zawadi hata ya gari ilimradi tu kusema nisamehe mke wangu hasiiseme!
moreen baby umempata
uran mwanaume muungwana kabisa na anayejua thamani ya Pendo,husiipoteze nafasi hiyo!