Shehe Kishk: Kiongozi anapaswa kuwe ni mtu wa Amani, mwenye Afya njema na akiba ya Chakula!

Shehe Kishk: Kiongozi anapaswa kuwe ni mtu wa Amani, mwenye Afya njema na akiba ya Chakula!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Shehe Kushk wa Jumuiya ya Temeke amesema kwa mujibu wa Qur'an tukufu Kiongozi wa kutawala duniani anapaswa kuwa na sifa kuu tatu, ambazo ni:
1.Mtu wa Amani

2. Mtu mwenye Afya njema

3. Mtu mwenye akiba ya Chakula

Kiongozi wa ngazi yoyote anapaswa kuwa na sifa kuu hizo tatu ili aweze kuwatumikia watu kwa uadilifu na pasipo ufisadi wala tamaa binafsi, amesisitiza Kishk.

Shehe Kishk amewageukia viongozi wenzake wa dini na kusema wana imani haba na kwamba hata wakijiunganisha wote hapa nchini kamwe hawawezi kuifikia imani ya Ibrahim kwa Mungu wake.

Shehe amewataka watanzania kuuombea uchaguzi ufanyike kwa njia za kheri na amani.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom