Uchaguzi 2020 Sheikh Alhad Mussa Salumu: Upande ambao haujaridhika kuhusu Uchaguzi usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria

Uchaguzi 2020 Sheikh Alhad Mussa Salumu: Upande ambao haujaridhika kuhusu Uchaguzi usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria

Pumbavu kabisa.
Mungu si fedhuli mpaka asikie maombi ya hawa wanafiki.
Corona ilifail kwasababu ya hali ya hewa na kinga yetu ya asili.
Mungu hawezi kufanya vitu nusunusu, au hawezi kufanya hili ajashindwa lile.
Umaskini mbona unaendelea?
UKIMWI mbona unazidi kutafuna taifa?.
Baadhi ya watu Wana watolea maneno ya fedheha ao viongozi wa dini Ila wakumbuke wao viongozi wa dini na serikali pamoja na baadhi ya Wananchi walimwomba Mungu dhidi ya Corona na Mungu akasikia maombiyetu na kutunusuru na janga la Corona. Leo wanaomba tuungane katika kuiombea nchi yetu utulivu bado kuna watu Wana watolea maneno ya ki fedhuli. Ni Mambo ya kuhuzunisha sana.
 
Huyu ni shehe wa Dar, kila kitu kipo dodoma kwanini asimuachie shehe wa Dodoma kusema
 
Anajua kabisa matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa mujibu wa katiba hayahojiwi wala hakuna chombo chochote kinaweza kupinga. Anawezeje kusema huo ujinga? Lakini pia maandamano siyo furugu, maandamano yanalindwa name polisi. Maandamano ndiyo njia pekee ya kudai haki kwenye uchaguzi huu
 
Ukweli wa dhuluma yote wanaujua, lakini kwa unafiki wao wanakimbilia tu kuwazuia wanaotaka kudai haki!

Hebu Waseme aliyeibiwa kura za urais atadai haki kwa njia ipi kwa katiba yetu hii?
 
Huu ni ushauri mzuri lakini wenzetu wanataka kushinda tu kila mara.

Haki inakuwa imetendeka pale wao wanaposhinda.
 
Na nyinyi waandishi mnaotuletea sijui shehe ugali wa Dar kasema hivi au vile, mliuliza hao waliowaitisha kama kulikuwa na HAKI kwenye uchaguzi?

Narudia

Mliuliza kama HAKI imetendeka kwenye uchaguzi?
 
Mwenyekiti wa Tume ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salumu amewasihi watanzania kuendelea kumshukuru Mungu kwa wema aliowatendea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa salama na amani.

Ameyazungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma, akiwa pamoja na wajumbe wa tume ya kitaifa ya maridhiano na wa mkoa wa Dodoma.

Aidha, Sheikh Alhad Mussa amesema kuwa inatakiwa sasa baada ya uchaguzi kumalizika salama ni kuungana kuendelea kuiombea kwa Mungu serikali iliyoshinda iongoze vema.

“Tunashukuru Mungu Uchaguzi umeisha kwa amani na salama, kilicho mbele yetu ni kuungana kuendelea kuiombea Mungu Serikali iliyopo madarakani ituongoze salama.

Katika chaguzi zote kuna kushinda na kushindwa, huwezi kukubalika na kila mmoja haiwezekani, manabii wa Mwenyezi Mungu na hata Wacha Mungu hawakukubalika nao walipingwa, hii ni desturi ni jambo la kawaida,”amesema Sheikh Alhad.

Ameshauri upande ambao haujaridhika usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria na hata jumuia hiyo inaweza kuweka mambo sawa.

“Kubwa tunawaomba Watanzania Nchi yetu iendelee kuwa salama na utulivu, tunahitaji nchi yenye amani ili tuweze kufanya shughuli zetu kwa ukamilifu bila bughudha yoyote, tusijaribu kuchezea amani iliyopo, tutajuta, tuna mifano mingi ya nchi mbalimbali zilizochezea amani, kuirejesha ni ngumu sana.”

Amesema viongozi wa Dini walimlilia sana Mungu ili Uchaguzi uvuke kwa salama na amani, hivyo inabidi kumshukuru Mungu kwa wema wake aliotutendea. na kwamba wakifanya hivyo Mungu atatuzidishia.

Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa viongozi wote walioiombea kwa Mungu nchi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa corona na Uchaguzi Mkuu na sasa iko salama hivyo tuendelee kumshukuru Mungu naye ataendelea kutusikiliza.
Nimekumbuka movie ya kihindi inaitwa Andhaa Kanoun maana ya ni SHERIA NI KIPOFU lile sanamu likafungwa kitambaa
 
Wanashindwa kusema chanzo cha vurugu kitakuwa ni kipi wanawarukia walioshindwa kwa kudhurumiwa haki.
 
Watskaosababisha vurugu ni wale ambao hawatendi haki lakini hawasemwi.
 
Eti mesema

Upande ambao haujaridhika kuhusu Uchaguzi usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria.​

Labda angelituambia mbali ya taratibu ya sheria kuna taratibu gani nyengine za kufuata? Kwa nini huyu jamaa hakai kimya na kufanya kazi zake za kidini? Nilidhani Tanzania haina dini sana kwa nini watu wa dini wanajiingiza katika masuali ya siasa pamoja na uongozi wa nchi?
 
Mwenyekiti wa Tume ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salumu amewasihi watanzania kuendelea kumshukuru Mungu kwa wema aliowatendea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa salama na amani.

Ameyazungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma, akiwa pamoja na wajumbe wa tume ya kitaifa ya maridhiano na wa mkoa wa Dodoma.

Aidha, Sheikh Alhad Mussa amesema kuwa inatakiwa sasa baada ya uchaguzi kumalizika salama ni kuungana kuendelea kuiombea kwa Mungu serikali iliyoshinda iongoze vema.

“Tunashukuru Mungu Uchaguzi umeisha kwa amani na salama, kilicho mbele yetu ni kuungana kuendelea kuiombea Mungu Serikali iliyopo madarakani ituongoze salama.

Katika chaguzi zote kuna kushinda na kushindwa, huwezi kukubalika na kila mmoja haiwezekani, manabii wa Mwenyezi Mungu na hata Wacha Mungu hawakukubalika nao walipingwa, hii ni desturi ni jambo la kawaida,”amesema Sheikh Alhad.

Ameshauri upande ambao haujaridhika usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria na hata jumuia hiyo inaweza kuweka mambo sawa.

“Kubwa tunawaomba Watanzania Nchi yetu iendelee kuwa salama na utulivu, tunahitaji nchi yenye amani ili tuweze kufanya shughuli zetu kwa ukamilifu bila bughudha yoyote, tusijaribu kuchezea amani iliyopo, tutajuta, tuna mifano mingi ya nchi mbalimbali zilizochezea amani, kuirejesha ni ngumu sana.”

Amesema viongozi wa Dini walimlilia sana Mungu ili Uchaguzi uvuke kwa salama na amani, hivyo inabidi kumshukuru Mungu kwa wema wake aliotutendea. na kwamba wakifanya hivyo Mungu atatuzidishia.

Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa viongozi wote walioiombea kwa Mungu nchi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa corona na Uchaguzi Mkuu na sasa iko salama hivyo tuendelee kumshukuru Mungu naye ataendelea kutusikiliza.
Hili lijamaaa yaani linakimbelembele sijui shekh gani huyu
 
Hivi kuna mtu anamsikiliza huyu mpuuzi tuu!! Hivi alichaguliwa lini kuwa shekhe wa mkuu wa Dsm....hahaha pimbi hili
 
Namchukia sana huyu Sheikh. Tumbo njaa vinamuongoza kusema. Hata Lissu angeshinda angebadili uelekeo wa dishi lake.
 
Back
Top Bottom