Karungikana
JF-Expert Member
- Jan 8, 2017
- 913
- 844
Sheikh uchwara, shame on you!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baadhi ya watu Wana watolea maneno ya fedheha ao viongozi wa dini Ila wakumbuke wao viongozi wa dini na serikali pamoja na baadhi ya Wananchi walimwomba Mungu dhidi ya Corona na Mungu akasikia maombiyetu na kutunusuru na janga la Corona. Leo wanaomba tuungane katika kuiombea nchi yetu utulivu bado kuna watu Wana watolea maneno ya ki fedhuli. Ni Mambo ya kuhuzunisha sana.
Nimekumbuka movie ya kihindi inaitwa Andhaa Kanoun maana ya ni SHERIA NI KIPOFU lile sanamu likafungwa kitambaa
Mwenyekiti wa Tume ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salumu amewasihi watanzania kuendelea kumshukuru Mungu kwa wema aliowatendea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa salama na amani.
Ameyazungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma, akiwa pamoja na wajumbe wa tume ya kitaifa ya maridhiano na wa mkoa wa Dodoma.
Aidha, Sheikh Alhad Mussa amesema kuwa inatakiwa sasa baada ya uchaguzi kumalizika salama ni kuungana kuendelea kuiombea kwa Mungu serikali iliyoshinda iongoze vema.
“Tunashukuru Mungu Uchaguzi umeisha kwa amani na salama, kilicho mbele yetu ni kuungana kuendelea kuiombea Mungu Serikali iliyopo madarakani ituongoze salama.
Katika chaguzi zote kuna kushinda na kushindwa, huwezi kukubalika na kila mmoja haiwezekani, manabii wa Mwenyezi Mungu na hata Wacha Mungu hawakukubalika nao walipingwa, hii ni desturi ni jambo la kawaida,”amesema Sheikh Alhad.
Ameshauri upande ambao haujaridhika usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria na hata jumuia hiyo inaweza kuweka mambo sawa.
“Kubwa tunawaomba Watanzania Nchi yetu iendelee kuwa salama na utulivu, tunahitaji nchi yenye amani ili tuweze kufanya shughuli zetu kwa ukamilifu bila bughudha yoyote, tusijaribu kuchezea amani iliyopo, tutajuta, tuna mifano mingi ya nchi mbalimbali zilizochezea amani, kuirejesha ni ngumu sana.”
Amesema viongozi wa Dini walimlilia sana Mungu ili Uchaguzi uvuke kwa salama na amani, hivyo inabidi kumshukuru Mungu kwa wema wake aliotutendea. na kwamba wakifanya hivyo Mungu atatuzidishia.
Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa viongozi wote walioiombea kwa Mungu nchi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa corona na Uchaguzi Mkuu na sasa iko salama hivyo tuendelee kumshukuru Mungu naye ataendelea kutusikiliza.
Hili lijamaaa yaani linakimbelembele sijui shekh gani huyu