Uchaguzi 2020 Sheikh Alhad Mussa Salumu: Upande ambao haujaridhika kuhusu Uchaguzi usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria

Uchaguzi 2020 Sheikh Alhad Mussa Salumu: Upande ambao haujaridhika kuhusu Uchaguzi usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
1604477513025.png

Mwenyekiti wa Tume ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salumu amewasihi watanzania kuendelea kumshukuru Mungu kwa wema aliowatendea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa salama na amani.

Ameyazungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma, akiwa pamoja na wajumbe wa tume ya kitaifa ya maridhiano na wa mkoa wa Dodoma.

Aidha, Sheikh Alhad Mussa amesema kuwa inatakiwa sasa baada ya uchaguzi kumalizika salama ni kuungana kuendelea kuiombea kwa Mungu serikali iliyoshinda iongoze vema.

“Tunashukuru Mungu Uchaguzi umeisha kwa amani na salama, kilicho mbele yetu ni kuungana kuendelea kuiombea Mungu Serikali iliyopo madarakani ituongoze salama.

Katika chaguzi zote kuna kushinda na kushindwa, huwezi kukubalika na kila mmoja haiwezekani, manabii wa Mwenyezi Mungu na hata Wacha Mungu hawakukubalika nao walipingwa, hii ni desturi ni jambo la kawaida,”amesema Sheikh Alhad.

Ameshauri upande ambao haujaridhika usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria na hata jumuia hiyo inaweza kuweka mambo sawa.

“Kubwa tunawaomba Watanzania Nchi yetu iendelee kuwa salama na utulivu, tunahitaji nchi yenye amani ili tuweze kufanya shughuli zetu kwa ukamilifu bila bughudha yoyote, tusijaribu kuchezea amani iliyopo, tutajuta, tuna mifano mingi ya nchi mbalimbali zilizochezea amani, kuirejesha ni ngumu sana.”

Amesema viongozi wa Dini walimlilia sana Mungu ili Uchaguzi uvuke kwa salama na amani, hivyo inabidi kumshukuru Mungu kwa wema wake aliotutendea. na kwamba wakifanya hivyo Mungu atatuzidishia.

Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa viongozi wote walioiombea kwa Mungu nchi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa corona na Uchaguzi Mkuu na sasa iko salama hivyo tuendelee kumshukuru Mungu naye ataendelea kutusikiliza.
 
Watu wazima wanapojitoa fahamu huwa ni mtihani katika nchi ,
Kuna jambo, unapoona viongozi wengi wa Taasisi mbali mbali hawawezi kusema lolote basi ujue nchi au sehemu hio sio salama tena.

Ukiona viongozi wa jeshi na vyombo vingine vya usalama,na wakuu mbali mbali hawawezi kufanya wajibu wao kisheria basi ,kila wanachokifanya kinaonekana kuenda kinyume na sheria ya nchi ,basi ujue sehemu hio imeshavurugika kama ni nchi ndio imeshaharibika, tusitegeme wazungu watakuja wafanye au kutuweka sawa,unajua vita vya panzi furaha ya kunguru.

Tanzania zipo sheria nyingi tu ,lakini leo hii sheria zimewekwa kando ndio tunaona kila mmoja ni kiranja,la kutahadhari wale waliokatika madaraka ipo siku watarudi katika maisha ya uraiani.
 
Uchaguzi ni salama, amani na haki sio salama na amani mbona umeruka haki. Nadhani Shekh ubwabwa unataka kazi mpya uwe msuluhishi? unatumika vibaya sana na una mwisho mbaya sana. Halafu anayepiga kelele ni balozi wa USA kama unaudhubutu nenda kamwambie.
 
Uchaguzi ni salama, amani na haki sio salama na amani mbona umeruka haki. Nadhani Shekh ubwabwa unataka kazi mpya uwe msuluhishi? unatumika vibaya sana na una mwisho mbaya sana. Halafu anayepiga kelele ni balozi wa USA kama unaudhubutu nenda kamwambie.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Kiukweli inachekesha huku inaumiza,Viongoz wa dini nao wanapigania ugali wa watoto wao usije ukamwagika!
 
Hakuna dhambi viongozi wa dini kutii serikali hilo wala sio tatizo ni jambo zuri, shida inakuja viongozi kutosemea haki mtu anayekupenda ki kweli atakukosoa ili usikosee atakushauri unapokosea. Kiongozi ukiwa unaaminika kwa haki hukumu yako na kauli yako inakuwa na nguvu na kuheshimiwa.
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Kiukweli inachekesha huku inaumiza,Viongoz wa dini nao wanapigania ugali wa watoto wao usije ukamwagika!
Kibaya Zaidi Viongozi Wa Dini Wamejitoa Akili
Upande Wanaoupigania Ni Wazi Ccm, Wanachokitetea Ccm.

Walitakiwa WaweNEUTRAL Wakemee Uonevu Pande Zote, Waipiganie Haki Bila Kuangalia Maslahi Ya Chama Dola
 
Hakuna dhambi viongozi wa dini kutii serikali hilo wala sio tatizo ni jambo zuri, shida inakuja viongozi kutosemea haki mtu anayekupenda ki kweli atakukosoa ili usikosee atakushauri unapokosea. Kiongozi ukiwa unaaminika kwa haki hukumu yako na kauli yako inakuwa na nguvu na kuheshimiwa.
NIMEKUSOMA!
 
Baadhi ya watu Wana watolea maneno ya fedheha ao viongozi wa dini Ila wakumbuke wao viongozi wa dini na serikali pamoja na baadhi ya Wananchi walimwomba Mungu dhidi ya Corona na Mungu akasikia maombiyetu na kutunusuru na janga la Corona. Leo wanaomba tuungane katika kuiombea nchi yetu utulivu bado kuna watu Wana watolea maneno ya ki fedhuli. Ni Mambo ya kuhuzunisha sana.
 
Hii Tume ya Maridhiano imeundwa lini, kwa sheria gani na wajumbe wake wanapatikanaje?
 
Hawezi kutetea haki bora akae kimya ina maana yote yaliyofanyika kabla na katika uchaguzi hakuyaona!!! Tuna tatizo la kuwapata viongozi wa adilifu na wakweli,anashindwa kuwanasihi viongozi wa nchi kama alivyofanya Imam Ahmad bin ambal na Iman shafi kwa kusimamia ukweli mpaka wakatiwa maabusu na viongozi madhalim wakati wao
 
Aliyewahi kuona popote mtu kawashauri wapinzani hasa bavicha jambo jema kwa maslahi ya nchi wakakubali aniwekee hapa thread husika.
Hawa jamaa hua hawakubali ushauri kwa yeyote
 
Uchaguzi ushaisha bado masheikh na waislamu wanazorota jela. Kalizungumzia ili sheikh ?
 
Kwani sheria zetu mfu zinasemaje kuhusu matokeo ya Urais?
Maana nijuavyo mimi kuhusu matokeo ta Urais bongo huruhusiwi hata kuhoji.
Hii katiba yetu Rais inampa uungu.
Turudi kwenye ubunge na udiwani. Ni Mahakama gani au NEC iliyo upande wa CCM itatoa haki?
 
Back
Top Bottom