Sheikh Hamisi Mataka: Nilivyokoseshwa elimu ya Sekondari

Point
 
Uthman,
Kuna kisa hiki cha huyu mwanafunzi Adam Ramadhani Kindenge aliyekuwa
mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Gilman Rutihinda.

Adam alikuwa mwanfunzi hodari akiongoza darasa lakini hakuchaguliwa
kwenda sekondari.

Kama tunavyosoma hapa majibu ya labda siku ya mtihani hakufanya vizuri
nk. nk.

Baba yake, Mzee Ramadhani Kindege hakuridhika na akadai lazima aoneshwe
karatasi za mwanae vinginevyo watafikishana mbali.

Kesi hii ilikuwa ya kufedhehesha kwani walipokuja kuangalia karatasi za mtihani
ikaja kugundulika kuwa wanafunzi wa Kikristo waliokuwa na alama za chini sana
wamechaguliwa na Adam na wenzake mfano wa yeye wameachwa juu ya kuwa
walikuwa na lama za juu.

Huu ndiyo ukweli ambao sisi tukiujua kwa miaka mingi sana.
Kuwa leo haya tunayajadili hadharani ni jambo la faraja sana kwetu.
 

Story za vijiweni tu hizo.
 
Hearly,
Nami nitasaidia katika kueleza yale ambayo yameonekana katika Wizara ya Elimu kuhusu shutuma za ubaguzi na kufanya upendeleo.

Naingia Maktaba In Shaa Allah.

Hearly,
Nimeingia Maktaba na nimwweka mkasa wa kijana Adam Ramadhani Kindenge
wa Shule ya Gilman Rutihinda aliyefanyiwa dhulma na Wizara ya Elimu kwa kuacha
kuchaguliwa hali ya kuwa alikuwa na uwezo mkubwa wa masomo.

Naweka mkasa mwingine.

Mwanafunzi Kopa Abdallah yeye alichaguliwa kwenda sekondari kutoka Shule ya
Kichangani, Kilosa mwaka wa 1983.

Kopa jina lake likakatwa na nafasi yake kupewa Anthony Samirani.
Hivi tusemavyo Kopa Abdallah ni dereva.

Huyu Kopa Abdallah kama walivyo wengi waliodhulumiwa miaka nenda miaka rudi.
 
Story za vijiweni tu hizo.
Nanren,
Mimi nina hadhi yangu katika utafiti na uandishi.
Siwezi kunyanyua kalamu kuandika, ''stori za vijiweni.''

Lakini ikiwa limekushtusha ukaona kuwa huu ni uongo haya hayawezekani
mimi sina tatizo na hilo.

Muhimu ni kuwa tujadili matatizo haya kwa uwazi kama hivi na viongozi wetu
wajue wao ndiyo wenye jukumu la kutoa haki kwa wote bila ubaguzi.
 
Sheikh anachonikera anarandaranda mtaa mmoja tu haendi mtaa wa PhD kutembea maana yake ndio nini sasa kizunguuka na post graduate diploma na master kazaa...uwezo unao nenda kapige hiyo kitu ili uweleweke maalim
 
Astaghfirullah! Ulianza darasa la kwanza ukiwa na umri wa miaka 11 tena jijini Dar es Salaam! Nikiwa na umri wa miaka 11 nilikuwa niko darasa la 6 tena kijijini! Ngoja nikae kimya.


Ndiyo tatizo la kuendekeza dini na mila za watu ambazo hazina manufaa kwetu hata kidogo, ni haibu sana.
 
Hata mimi ilinikuta hii mkuu,
 

Nimekuelewa mkuu, japo bado siamini kuwa watu waliokosa nafasi za sekondari miaka yetu ile migumu walikoseshwa kwa sababu ya dini zao.

Nimeeleza kwenye post nyingine kuwa ushindani wa nafasi za sekondari miaka ile ulikuwa mgumu sana. Nikatoa mfano wa nilikosoma mimi ambako 100% tulikuwa wakristo lakini bado tuliminywa vibaya, shule zilikuwa zinatoka 'kapa' miaka kadhaa bila kutoa mwanafunzi anayejiunga sekondari ya serikali.

Na katika sekondari za serikali wanafunzi wa kiislamu walikuwepo, tena na uhuru kamili wa kuabudu. Baadhi ya shule za serikali ninazozijua zilikuwa na masjid ndani ya shule ambako wanafunzi wa kiislamu waliweza kusimamisha swala kwa utaratibu wa dini yao.

Walipikiwa futari wakati wa Ramadhani na waliruhusiwa kushiriki kwenye shughuli za chama chao cha wanafunzi waislamu pamoja na shule nyingine kama dini nyingine zilivyofanya. Kila dini ilikuwa na mwalimu mshauri wa wanafunzi wa dini hiyo, na nikiwa A-level mwalimu wa waislamu alikuwa secondmaster. Sasa hapo sijui mtu anafelishwaje, kwa ulinzi wote huo?

Kwa ujumla, fursa za elimu zilikuwa finyu kwa wote. Wengine walijiongeza kama alivyofanya Sheikh Mataka, lakini naweza kusema wapo waliojitahidi zaidi katika kujiongeza, na naamini hiyo ndiyo iliyoleta tofauti.

Inawezekana zilikuwapo individual cases (siyo institutional) za ubaguzi kama aliosema Sheikh Mataka kuwa alifanyiwa, na kwa kadri nijuavyo cases kama hizo zipo hadi leo kama zilivyo dhulma nyingine ambazo zinatakiwa kupigwa vita sana.

Siamini kuna taasisi yoyote iliyomtuma yule mwalimu kumtamkia Sheikh Mataka kauli za kibaguzi za kumkatisha tamaa, hivyo naamini kuwa kama Sheikh Mataka angeweka lalamiko rasmi lazima hatua ingechukuliwa.
 
Sheikh Hongera sana. Matarajio yangu ni kwamba andiko lako lita-inspire vijana kutokubali kushindwa hasa kwenye elimu.
Hongera sana.
 
Mshika 2 moja humponyoka!wahenga hawakukosea!huku mwanafunzi kule mwl wa madrassa.....mwambie alikua kilaza tu asitafute sababu nyingine za kitoto!
 
Tatizo letu waislam tumekua tukitafuta excuse zisizo na msingi kwenye matatizo yetu binafsi, mm baba yangu ni muislam na alipata bahati ya kwenda ya katoriki ikifahamika kuwa ni muislam, nadhani sheikh Hamis angetafuta sababu gunuine kwann hakuchaguliwa kusema alikua anashika nafasi ya kwanza darasani haitoshi pengine alikia anaongoza darasa la wajinga!
 


Ndugu yangu kayaman,ulifanya utafiti juu ya hili?Hao wajinga wenzie Ustaadh Mataka walichaguliwa lakini yeye aliachwa.Kuna kisa kanipa mzee wangu wakati anasoma middle school Tabora.Yeye alikuwa hodari sana darasani walimu wake wazungu wakimpenda sana,matokeo ya mwisho yakitoka yeye hayumo katika wanaondelea.Ndipo mwalimu wake akamwita na kumwambia usipobadili jina lako hautopata nafasi ya kujendelea na masomo.Ilimbidi aanze kuitwa Moses badala ya Mussa na kumalizia jina la kilugha.Toka alipofanya hivyo hakupata kikwazo chochote kwenye elimu.

Ndugu zetu msitubeze,kwa kuwa nyinyi hamkuathirika basi isimaanishe hali ilikuwa sawa.Tumeyaishi hayo maumivu kwa muda mrefu sana, hatutaki kulipwa chochote wala upendeleo wa aina yeyote bali haki itendeke.
 
Sheikh Uthman,
Ahsante sana kwa nasaa zako na uungwana ulioonyesha.
Nimeweka hapa mifano miwili ya tatizo hili:
  1. Kopa Abdallah
  2. Abdallah Ramadhani Kindenge
Hizi ni kesi za kweli kabisa na Wizara ya Elimu walitaarifiwa.

Ngoja niweke kisa kingine kuhusu hii dhulma.

Morogoro Municipal Education Officer aliwaandikia Walimu Wakuu wa Shule zote za Msingi
Morogorobarua yenye rejea No. E10/MMC-1/183 ya 9 June, 1998 akiwaelekeza wapeleke
kwake majina wanafunzi Wakatoliki wa darasa la saba.

Gazeti la An - Nuur wakaarifiwa kuhusu hili na wakaipata barua yenyewe ambayo waliifikisha
Wizara ya Elimu kutaka maelezo.

Wizara ikasema kuwa itachunguza.
Kwa nini sisi tunaeleza na kuandika taarifa hizi hapa.

Hatufanyi haya kujifurahisha.

Tunayafanya haya ili hii dhulma ifahamike kwa wote wanaoathirika na mwendo huu tukitegemea
kuwa viongozi wetu watakomesha dhulma hii kwa njia za salama kwani dhulma ikidumu huangamiza
 
Kayaman, Mielekulechoma,
Nakuomba msome na post nyingine ambazo visa kama hiki cha Sheikh
Mataka vimeelezwa.

Ikiwa wewe Kayaman ni Muislam nadhani unafahamu ikiwa umesoma,
ilm iliyoka katika madras khasa katika kuwafunza wanafunzi ''hifdh.''

Elimu ya kuweza kuhifadhi na kusoma ''ghibu,'' kile ulichofundishwa.
Sheikh Mataka akiwa mtoto mdogo tayari alikuwa mwalimu wa chuo
akisomesha na alipofika Mchikichini akawa mwalimu pia kwa kuwafunza
wanafunzi wenzake.

''Kilaza,'' kutumia lugha iliyotumika ingawa ya kejeli, Sheikh Mataka
hawezi kuwa na sifa hizo.

Naamini umeona vyeti alivyoweza kupata baada ya kumaliza elimu ya
msingi.

Mwisho nakusihini kuwa mueleza fikra zenu kwa adabu na uungwana.
Haya si mambo ya kuandika kwa kejeli na kebehi.
 
Mkuu huu uzi umenipa mawazo fikirishi kidogo naomba niruhus ni kote sehemu ya maelezo yako..
“Mwalimu wangu wa Historia Mzee Kasunsumo alipata kuniambia: '’Sheikh Khamis, pamoja na uwezo wako wa kielimu hutochaguliwa kwenda sekondari na kinachokuponza ni huu ualimu wako wa Dini ya Kiislamu” kutokea hapo ningependa kufahamu kama katika shule uliyosoma ni wakristo pekee (ama wengine wasio dini ya Kiislam) ndo walikuwa wanafaulu tu? Ilikuwaje ukaweza unga unga sehemu nyingine kielim ili hali wewe ni “muislam”..nataka fahamu hayo sheikh manake najua kuna watu wengine wengi tu (wengine wamepata kuwa viongozi wakubwa tu nchi hii) ambao walikuwa na “akil”kwelikweli walivyokuwa shule ya msingi (na pia walikuwa Wakristo) lakini hawakufaulu au “kuchaguliwa” wakalazimika kutumia mbinu mbadala hata kubadili ubini ili mradi waendelee… unalizungumziaje hili?
 
Mo mimi mwenyewe baba yangu ni mkristo jina lake lilikatwa akapewa mtu mwingine tunaliwekaje hilo kwenye historia
 
Hiyo hatua iliyochukuliwa dhidi ya huyo Municipal Education officer ni sahihi, na inapaswa wengine wote waliobainika kutenda mambo yanayoashiria ubaguzi wachukuliwe hatua. Mimi bado naona kuwa mengi ya matendo haya yalifanywa kwa utashi binafsi wa mtendaji, sio kwa kufuata maelekezo ya taasisi au mfumo wowote rasmi, hivyo ni bora kila case ikashughulikiwa binafsi. Na zikishashughulikiwa nyingi hivyo, hata mwingine anayetaka kufanya hivyo atasita.
Hili nalichukulia kama ubaguzi ninaouona nchi za Marekani na Ulaya dhidi ya watu weusi na wasiokuwa wazungu. Sera iko wazi kuwa ubaguzi ni kinyume cha sheria, lakini bado wapo wanaobagua hadi leo. Na dhambi nyingine zote ni hivyohivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…