Mzee Mohammed Said,Asalaam Aleykum!
Lengo la mada yako haswa ni nini?
Ni waislamu kunyimwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na dini yao?
ama ni
Kuungaunga elimu sio tatizo kwa maana walioungaunga na waliounganisha elimu moja kwa moja mnakuja kupanga foleni moja kwenye kutunukiwa vyeti?
Kama lengo ni hilo la pili ninakuunga mkono sana na niwatie shime wale wanaoungaunga elimu kuwa malengo yao yatafanikiwa,hakuna kukata tamaa.
Maprofesa wengi wa zamani ninaowafahamu hasa wa udsm ni miongoni mwa wengi waliopitia njia ndefu hadi hapo walipo.
Kama lengo lako ni hilo la kwanza ,nachelea kusema haupo sahihi.
Acha kuwa miongoni mwa wanaolialia bure ama kwa kutaka kueta uchochezi wa kidini.
Ungetuambia wale wote waliopitwa na Shehe Mataka na wakaenda sekondari hawakuwepo waislamu?
Unaweza kututhibitishia haya ama ni stori tu za kuchochea moto?
Acha kulia lia shehe wangu