TANZIA Sheikh Hassan Mohamed Said Kinyozi Mpigania Uhuru na Mmoja wa Waasisi wa TANU Lindi amefariki Dunia

TANZIA Sheikh Hassan Mohamed Said Kinyozi Mpigania Uhuru na Mmoja wa Waasisi wa TANU Lindi amefariki Dunia

Kuna mambo huwa yanashangaza sana tena sana kuhusu huyu mtoa mada huwa muda mwingine namfanananisha na sheikh Rogo,mfano mji wa daresalam wakati ule kabla haujawa na muingiliano mkubwa nikweli jamii kubwa walikuwa ni waislamu ambacho ni kitu cha kawaida kwa mikoa ya pwani,mimi binafsi natokea mkoa wa mtwara ndiko kwetu na mwaka 2012 watu wa mtwara walileta mgomo wa kuwa gesi haitoki hali ambayo ilileta machafuko makubwa mno hususani mkoa wa mtwara wote,hamasa zilitoka kwenye mimbari za misikiti tofauti hapa mjini na kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa gesi isitoke na kama unavyojua mtwara asilimia 93% ni waislamu na pia nakumbuka mimi na ndugu zangu tulijihimu kabisa uwanja wa mashujaa kwenye kisomo cha albadir na hiyo siku uwanja ulifurika mno utadhani siku ya iddi vile,sasa je ni sahihi kuhusisha lile vuguvugu la kudai gesi na uislamu kisa eti wengi wao walikuwa waislamu?
Akikujibu uje uniambie, nimekaa pale Naliendere
 
Tatizo maandiko yako karibu yote huwa yana harufu ya udini, uliza wengine
Sisi wakristo tunaojielewa hatujaona huo udini au wewe mwenzetu ni mgonjwa WA Akili? Maana uoga ukizidi Sana ni matatizo ya Akili
 
Huyu mtoa mada mara nyingi sana huwa anahusisha mapambano ya kudai uhuru na uislamu eti kisa walikuwa eti wanafanya kisomo kabla nyerere hajaenda UN mara hivi mara vile..... nimemtolea mfano mwaka 2012 wakati wa vuguvugu la gesi hapa mtwara vilifanyika visomo misikitini na pia ulifanyika uchawi pia na ikasomwa albadir pale uwanja wa mashujaa kumshtakia Allah juu ya ile dhulma ila yote kwa yote dhumuni kuu ilikuwa ni kwamba gesi isitoke huku mtwara,kwahiyo zilitumika mbinu tofauti ila lengo lilikuwa moja kuwa gesi isitoke sasa je ni halali siku na miaka ijayo watokee watu kama huyu Mohamed Saidi wahusishe suala la kudai gesi na uislamu eti kisa sijui wakina sheikh matola na sheikh badi ndio waliongoza hivyo visomo na harakati zote za kudai gesi? Tusipotoshane munapozeeka zeekeni kwa amani
Akikujibu uje uniambie, nimekaa pale Naliendere
 
Huyu mtoa mada mara nyingi sana huwa anahusisha mapambano ya kudai uhuru na uislamu eti kisa walikuwa eti wanafanya kisomo kabla nyerere hajaenda UN mara hivi mara vile..... nimemtolea mfano mwaka 2012 wakati wa vuguvugu la gesi hapa mtwara vilifanyika visomo misikitini na pia ulifanyika uchawi pia na ikasomwa albadir pale uwanja wa mashujaa kumshtakia Allah juu ya ile dhulma ila yote kwa yote dhumuni kuu ilikuwa ni kwamba gesi isitoke huku mtwara,kwahiyo zilitumika mbinu tofauti ila lengo lilikuwa moja kuwa gesi isitoke sasa je ni halali siku na miaka ijayo watokee watu kama huyu Mohamed Saidi wahusishe suala la kudai gesi na uislamu eti kisa sijui wakina sheikh matola na sheikh badi ndio waliongoza hivyo visomo na harakati zote za kudai gesi? Tusipotoshane munapozeeka zeekeni kwa amani
Umenena vema, suala la uhuru sio la eneo moja wala dini flani pekee.
Pale Masasi magari ya halmashauri na baadhi ya majengo yalitiwa moto na waislam, wakristo na wasio na dini kipindi hicho cha kugomea gas na kila kona ilikuwa patashika hiyo 2012 kwa maeneo ya kusini lakini hauwezi husisha suala hilo na imani flani japo imani flani ilionekana kusimamia harakati kwa vile hilo ndio kundi kubwa.
 
SHEIKH HASSAN MOHAMED SAID KINYOZI MPIGANIA UHURU NA MMOJA WA WAASISI WA TANU LINDI AMEFARIKI DUNIA

Jioni hii imenifikia taarifa kutoka Lindi kuwa Hassan Mohamed Said Kinyozi mmoja katika vijana waliowasha moto wa kupigania uhuru wa Tanganyika Southern Province, yaani Jimbo la Kusini amefariki dunia akiwa na umri wa kiasi cha miaka 90.

Nakumbuka kama jana siku nilipofika Lindi kwa basi dogo nikitokea Mtwara.

Barabara ya Lindi Mtwara ilikuwa mbovu sana miaka ile basi likiendeshwa kwa tahadhari kubwa.

Nakumbuka tulipoingia Lindi tunaelekea stendi natazama yale mandhari ya mji nageuza shingo huku na huku zile nyumba naziona mfano wa nyumba za Mtaa wa Swahili Dar es Salaam miaka ya 1950.

Nami nimo katika basi la Dar es Salaam Motor Transport (DMT) natokea Moshi shule nakuja likizo Dar es Salaam.

Nakumbuka nilikuwa nakabidhiwa kwa dereva Kapesa Johari kijana wa Gerezani kwani nilikuwa bado mdogo niko shule ya msingi hata uhuru bado.

Niko Lindi ndani ya basi naangalia minazi na nyumba zilizoezekwa kwa makuti.

Hii Lindi machoni kwangu ilikuwa sawasawa na Dar es Salaam ya udogoni kwangu.

Nilikuwa katika utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes na mwaka ulikuwa wa 1993.

Hassan Mohamed Said Kinyozi amefariki.

Nimemtaja shujaa mzalendo huyu Maalim Hassan Mohamed Kinyozi, mtoto wa Sheikh Kinyozi aliyekuwa anaendesha moja ya madrasa maarufu mjini Lindi iliyofahamika kama Madrasa ya Sheikh Kinyozi.

Madrasa hii bado ipo hadi leo na baada ya kifo cha baba yake marehemu Hassan Kinyozi alisimamia chuo hiki na kuendelea kusomesha hadi kifo kilipomchukua hii leo.

Kuna mtu alinikumbuka wakati nilipokwenda Lindi kufanya utafiti na mahojiano na Rashid Salum Mpunga na Yusuf Mohamed Chembera.

Huyu ndiye aliyenitafuta na kunipa taarifa ingawa hatukupata kuonana tena toka mwaka ule wa 1993.

Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes nikieleza historia ya TANU ni nani walioasisi chama cha TANU hapo Lindi utasoma maneno haya:

''...hawa wawili Ahmed Seif na Hassan Mohamed Kinyozi walikuwa ndiyo wafanyakazi wa kwanza wa TANU waliokuwa wakilipwa mshahara Southern Province.

Kwa ajili hii wakawa miongoni mwa wafanyakazi wachache sana walioajiriwa na TANU kwa wakati ule.

Suleiman Masudi Mnonji alitoa nyumba yake katika mtaa wa Makonde kuwa ofisi ya kwanza ya TANU kusini yote.

Baada tu ya kuanzishwa kwa TANU, Athumani Mussa Lukundu, kiongozi wa Lindi Dockworker's Union, aliunganisha chama chake na TANU.

Jambo hili kwa TANU lilikuwa la kuitia moyo sana kwa sababu Dockworker's Union ilikuwa na wanachama wengi na hatua ile iliongezea TANU nguvu.''

Bahati mbaya sana kuwa majina haya niliyoyataja hapo juu hayamo katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Naamini si wengi hata hapo Lindi kwenyewe wanaifahamu historia hii ya mzee wetu Hassan Mohamed Said Kinyozi.

Waasisi wakuu wa TANU ukimtoa Suleiman Masudi Mnonji walikuwa vijana wawili - Rashid Salum Mpunga na Yusuf Mohamed Chembera.
Baada ya kupokea taarifa ya msiba huu nikaanza kupiga simu huku na huku kutafuta picha ya marehemu.

Mmoja katika marafiki zangu wazawa wa Lindi akanitumia picha ya marehemu ya mwaka wa 1954 wakati huo akiwa kijana mdogo sana aliyopiga na wazee wa mjini wengi wao walikuja si muda mrefu kuwa mstari wa mbele katika TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Angalia picha ya pili hapo chini:

1.Aliyeketi chini mbele kushoto ni Hassan Mohamed Saidi Kinyozi
2. Aliyekaa kwenye kiti nyuma ya Hassan Kinyozi ni Rashid Salum Mpunga.
3. Aliyefunga tai ameketi ni Yusuf Mohamed Chembera.
4 Picha ilipigwa Ghana Restaurant 1954 na hii ilikuwa vilevile ni ofisi ya Lindi Seamens Club mahali walipokuwa wanakutana wanamji kwa mazungumzo na kituo cha harakati za TANU.
Picha ya tatu ni Hassan Mohamed Said Kinyozi katika ujana wake.

Sheikh Hassan Kinyozi ni mtu maarufu hata kwa wale ambao leo hawaijui historia yake kama mpigania uhuru.

Mtoto wa dada yake Bi. Salma bint Rashid ni mke wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Marehemu anategemewa kuzikwa leo Jumatano hapo Lindi.
Tunamwomba Allah amsamehe makosa yake na amweke Pepo ya Fidaus.

Amin.View attachment 2418084View attachment 2418085View attachment 2418131View attachment 2418132
Tafuta pesa Mzee, hiyo habari ya kujikuta bingwa wa kutetea dini zililetwa na majahazi zitakupotezea muda. Hazina tija yoyote kwako na kizazi chako.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Mini...
Hakuna suala la dini kaama mafunzo ya imani ya Uislam katika haya maandishi yangu.

Ninachofanya ni kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Wala katika hili sijapoteza kitu zaidi ya kunufaika na kazi ya ubongo wangu.

Nashukuru.
 
Wengine wanaona wivu kwa kutajwa wapiopigania Uhuru, watu hawataki kujifunza historia wakati hawajui historia ya Tanganyika na TANU.

Kwa akili fupi wao wanajua Nyerere tu ndo alileta Uhuru pekeyake Tanganyika nzima.
 
Back
Top Bottom