Sheikh
Mohamed Said
Wewe endelea kuandika historia kama unavyoipokea. Wanaodhani wewe wakosea wanayo nafasi ya kuandika ukweli wao.
Itoshe kusema wapo wengi sana wanaokufuatilia na kuiamini historia unayoiandika. Tarehe 14 Oktoba ilikuwa ni siku ya Kumbukumbu ha Kifo cha Mwalimu Nyerere na mwaka huu kupitia Clubhouse kulikuwa na mjadala wa maadhimisho ya siku hii. Mmoja wa Wazungumzaji alikuwa ni Mh. Tundu Antipas Lissu. Bwana Lissu katika mjadala ule alisifia sana kazi yako hii ya Life and Times of Abdulwahid Sykes. Aliwa rai sana wasikilizaji wasome kitabu hicho kwani kimeandikwa na Mwanahistoria makini na anayejua kutafuta chanzo cha habari vizuri.
Hivyo pamoja na maneno mengi ya mitandaoni humu ikutie moyo hata Wanasiasa wengi wa Kitanzania ambao baadhi yao humu wanawasikiliza wao hukusoma na kukufuatilia vyema