TANZIA Sheikh Hassan Mohamed Said Kinyozi Mpigania Uhuru na Mmoja wa Waasisi wa TANU Lindi amefariki Dunia

Akikujibu uje uniambie, nimekaa pale Naliendere
 
Huwezi kuwa mtafiti mzuri kama tiyari una matokeo kichwani
Gulwa,
Kitu gani kimekufanya wewe udhani kuwa tayari nina matokeo?
Kwani wewe ushapata kusoma historia hii penginepo?
 
Tatizo maandiko yako karibu yote huwa yana harufu ya udini, uliza wengine
Sisi wakristo tunaojielewa hatujaona huo udini au wewe mwenzetu ni mgonjwa WA Akili? Maana uoga ukizidi Sana ni matatizo ya Akili
 
Huyu mtoa mada mara nyingi sana huwa anahusisha mapambano ya kudai uhuru na uislamu eti kisa walikuwa eti wanafanya kisomo kabla nyerere hajaenda UN mara hivi mara vile..... nimemtolea mfano mwaka 2012 wakati wa vuguvugu la gesi hapa mtwara vilifanyika visomo misikitini na pia ulifanyika uchawi pia na ikasomwa albadir pale uwanja wa mashujaa kumshtakia Allah juu ya ile dhulma ila yote kwa yote dhumuni kuu ilikuwa ni kwamba gesi isitoke huku mtwara,kwahiyo zilitumika mbinu tofauti ila lengo lilikuwa moja kuwa gesi isitoke sasa je ni halali siku na miaka ijayo watokee watu kama huyu Mohamed Saidi wahusishe suala la kudai gesi na uislamu eti kisa sijui wakina sheikh matola na sheikh badi ndio waliongoza hivyo visomo na harakati zote za kudai gesi? Tusipotoshane munapozeeka zeekeni kwa amani
Akikujibu uje uniambie, nimekaa pale Naliendere
 
Umenena vema, suala la uhuru sio la eneo moja wala dini flani pekee.
Pale Masasi magari ya halmashauri na baadhi ya majengo yalitiwa moto na waislam, wakristo na wasio na dini kipindi hicho cha kugomea gas na kila kona ilikuwa patashika hiyo 2012 kwa maeneo ya kusini lakini hauwezi husisha suala hilo na imani flani japo imani flani ilionekana kusimamia harakati kwa vile hilo ndio kundi kubwa.
 
Tafuta pesa Mzee, hiyo habari ya kujikuta bingwa wa kutetea dini zililetwa na majahazi zitakupotezea muda. Hazina tija yoyote kwako na kizazi chako.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Mini...
Hakuna suala la dini kaama mafunzo ya imani ya Uislam katika haya maandishi yangu.

Ninachofanya ni kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Wala katika hili sijapoteza kitu zaidi ya kunufaika na kazi ya ubongo wangu.

Nashukuru.
 
Wengine wanaona wivu kwa kutajwa wapiopigania Uhuru, watu hawataki kujifunza historia wakati hawajui historia ya Tanganyika na TANU.

Kwa akili fupi wao wanajua Nyerere tu ndo alileta Uhuru pekeyake Tanganyika nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…