Tangawizi,
Mimi si mtu wa kujidanganya.
Mimi ni mtu wa ukweli.
Sijapatapo kuzungumza kuhusu vita katika maandiko yangu.
Kitabu changu kiimebadili historia nzima ya uhuru wa Tanganyika
na ukweli leo umejulikana nani aliasisi TANU na akina nani walikuwa
mstari wa mbele kupambana na ukoloni.
Aliyekuwa anajidanganya si mie.
Mie nimekuja na ukweli na katika huu nimekipata ninachokitafuta.
Hakika Tanzania ni kubwa kuliko matamanio yetu na ndiyo maana
baada ya zaidi ya nusu karne leo historia ya Tanzania imebadilika
na ukweli umejulikana.
Jina la Abdulwahid Sykes (1924-1968) katika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa sasa halihitaji kuelezwa sana.
Historia yake imekuwa ni historia ya kusisimua unapomsoma kuhusu yale aliyofanya katika kuunda chama cha TANU 1954 akianza na kubadilisha mwelekeo wa TAA alipoingia katika uongozi wake 1950.
Historia ya Abdul Sykes pia ina masikitiko pale baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 juhudi za makusudi zilipofanywa kulifuta jina lake katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na kwa hili si tu kuwa lilifutika jina lake peke yake bali na jina la mdogo wake Ally na la baba yao Kleist Sykes aliyekuwa muasisi wa African Association mwaka wa 1929.

Kulia: Ilyas Abdulwahid Sykes, Daisy Abdulwahid Sykes, Mwandishi akiwa ameshikilia Medali ya Mwenge wa Uhuru
Misky Abdulwahid Sykes na Kleist Abdulwahid Sykes
Ilichukua miaka 50 kwa Abdulwahid na mdogo wake Ally kutunukiwa medali ya ‘’Mwenge wa Uhuru,’’ kama utambuzi wa mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika wakiwa bega kwa bega na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere waliyemfahamu mwaka wa 1952.
Leo nimebahatika kuiona medali ya ''Mwenge wa Uhuru'' aliyotunukiwa Abdulwahid Sykes (post homous) na Rais Kikwete katika Viwanja vya Ikulu 9 Desemba, 2011 katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
Kuishika medali hii kwa mikono yangu kwangu kilikuwa kitu kilichokuwa na nafasi ya pekee katika moyo wangu.

Medali ya mwenge wa Uhuru aliyotunukiwa Abdulwahid Sykes katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa
Tanganyika 2011
(Picha kwa hisani ya mjukuu wa Abdul Sykes Aisha Kleist Sykes)

Mwandishi akiwa Azam TV akifanya kipindi cha Saba Saba 2015