Utakufa na stress kijana.Hakuna kitu inaitwa mfumo Kristu.Tatizo mnasoma Isalmic law na masomo mengine ya kiarabu halafu mnataka kuwa absorbed kwenye mfumo.Yaani nisome Canon law halafu niajiriwe kuwa hakimu,hell no!Ndo maana mnataka mahakama ya kadhi.Punguza.malalamiko na makasiriko.In short hakuna mfumo Kristo.Someni!
Nan...
Bahati mbaya umeifinga akili yako kwa hiyo huwezi kujifunza chochote kipya unaugua ugonjwa wa kuogopa ukweli.
Nimeeleza mara nyingi hapa kuwa tatizo si kuwa Waislam hawapeleki watoto kusoma bali kuna njama ndani ya serikali yetu inayoendeshwa na mawakala wa Kanisa ya kuwazuia Waislam wasipate elimu.
Angalia mfano huu wa watoto wa Kiislam waliopelekwa shule kusoma:
USIA WA MAREHEMU KITWANA SELEMANI KONDO KWA WATANZANIA
Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania May 24, 2017 0
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999
''Lakini tuende kielimu.
Ninayo ripoti ya mwaka huu.
Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu.
Asilimia 29 ni wengine. Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21.
Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe. Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.
Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu.
Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga.
Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha. Mwalimu Nyerere alisema zamani ifanywe bidii ya kuwanyanyua waliokuwa chini.
Sasa bidii hii siyo ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Bidii hii ni ya kuwakandamiza waliokuwa chini.''
Bunge lilikuwa kimya limejikunyata kwani haya hayakuwa yanaelezeka katika sheia zozote za utafiti wa takwimu.
Yapo mengi.
Unatuammbie tusome.
Unadhani Waislam watu wa kufunzwa umihumu wa elimu?
Mwaka wa 1968 Waislam wanajenga Chuo Kikuu.
Chuo kikahujumiwa na serikali yenyewe.
Ndiyo maana hapa mnakuja nyie kutujibu watu ambao mnanufaika na hii dhulma.
Waziri wa Elimu hakuwa na kinywa cha kuwaambia Waislam hawaleti watoto shule kusoma.
Mwandishi akimuhoji Kitwana Kondo nyumbani kwake Upanga 2012