MAGUFULI HAHITAJI KICK YA MSIKITI!
Mwamba "JPM!"
John Pombe Magufuli... ameondoka Dunia na hatarudi kamwe.Hii ni kanuni ya ki-maumbile ya Ki-dunia,kulingana na mafundidho ya vitabu vitakatifu vya Mungu kwamba kila nafsi itapitia hatua hiyo kwa muda wake utakapiwadia.
Mimi ninachofurahia ni jinsi Magufuli alivyoacha "Landmarks" lukuki ambazo zinawatesa hawa wapigaji wa kisasa wa kisiasa!
Hawawezi kumfuta Magufuli kirahisi ilhali kaacha Landmark kila kona ya nchi
Nitaziorodhesha hapa na muelewe sababu ya Magufuli kutofutika kirahisi Hapa nchini.
IKULU ya Chamwino-Dodoma.
BWAWA LA UMEME la Nyerere.
UKUTA wa Mererani-Manyara.
DARAJA la Tanzanite-Dar es Salaam.
FLYOVERS ya Mfugale -Dar es Salaam.
STENDI YA MAGUFULI-Dar es Salaam.
BARABARA NJIA SITA-Ubungo mpaka mbezi na kuendelea mlandizi.Dar es Salaam.
STENDI KUU -Morogoro.
SOKO KUU-Mwanza.
STENDI KUU-Nyegezi,Mwanza.
STENDI KUU-Nyamhongolo Mwanza.
UWANJA WA NDEGE-Chato.
DARAJA LA WAMI- TANGA.
BOMBA LA MAFUTA -Hoima Uganda mpaka Tanga Tanzania.
RELI YA SGR-Dar es Salaam mpaka Mwanza.
Hizi ni Landmarks na sio vitu vinavyohamishika.ndio maana sijataja Meli wala Ndege.
Kuna pia Zahanati zaidi ya 478 pamoja na hospitali za Wilaya,Rufaa pamoja na za kanda kama Hospitali ya Rufaa Chato.
Kiongozi kama huyu huwezi futa legacy yake kwa kutumia keyboard.
Halafu watu fulani wenye kushiriki uovu kupigana na Legacy ya JPM huku wakitaka kuzitumia hizo Landmarks za JPM kwenye uchaguzi ujao wa 2025.Ushahidi uko wazi.
Watuambie kwanza hizo awamu zingine ukiondoa ya Baba wa Taifa JK Nyerere(R.I.P),na pia Benjamin Mkapa(R.I.P).
Hao wengine watuambie legacy zao walizotuachia zaidi ya Ufisadi,Majungu na Kupigana na Makaburi.
Na kama taifa!
Ni nini na zinatusaidiaje kwa sasa kama zipo?
Mkuu
Stendi kuu ya Morogoro hapo hapana, aliikuta labda useme akiwa waziri wa ujenzi stendi hiyo ilijengwa.
Labda hizi hapa
1. Soko kuu la Chifu Kingalu hilo ndio 'credit' zake
2. Soko kuu la Chuno Mtwara
3. Stendi kuu Tanga, Muheza na Korogwe
3. Stendi ya mabasi ya mfano-Same, Kilimanjaro
4. Soko kuu Nane nane Dodoma
5. Stendi kuu ya Ndugai Dodoma
6. Stendi kuu Ipogolo, Iringa
7. Hosteli na Maktaba chuo kikuu Dar Es Salaam
8. Ujenzi wa meli kubwa ziwa viktoria, Tanganyika na Nyasa
9. Mji wa mfano wa serikali Mtumba Dodoma (Magufuli Satellite City)
10. Hospitali ya Uhuru Chamwino Dodoma
11. Daraja la mto Wami Chalinze, Pwani
12. Mwekezaji mzawa kupewa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha sukari Bagamoyo (Bagamoyo Sugar-AZAM)
13. Ununuzi wa rada kwa kanda tano kwa ajili ya usalama wa anga
14. Uboreshaji wa mikataba ya madini kwa manufaa ya taifa baada ya kutungwa sheria wezeshi
15. Upanuzi wa bandari ya Mtwara na Tanga kwa kujenga magati mapana zaidi kuwezesha meli kubwa kutua nanga
16. Wananchi wasio na mamlaka na masikini kutetea kwa dhati na jitihada kuonekana
17. Heshima kwa watumishi serikalini kurejeshwa ijapokuwa kwa sasa wameota mapembe tena na kuanza kuwanyanyasa wananchi bila hata kuchukuliwa hatua stahiki
18. Kudhibiti mfumuko wa bei ya bidhaa ambazo ni mhimu kwa matumizi ya wananchi kwa kila siku
19. Jeshi kuaminiwa kiasi cha kutosha katika usimamizi wa miradi ya umma
20. Wananchi kuwa na uwezo wa kumiliki ardhi bila usumbufu na kujenga
Nk................