Sheikh Kabeke: Vyombo vya ulinzi havihusiki na mauji ya wananchi

Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke amesema si kweli kwamba vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinahusika na mauaji ya raia akieleza kuwa tuhuma hizo hazina msingi na zinapaswa kupuuzwa.

Akizungumza na Jambo TV ofisini kwake, Sheikh Kabeke ametolea mfano matukio yaliyojitokeza Oktoba 29, 2025 akisisitiza kuwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama hutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kiapo walichoapa cha kulinda nchi, raia na mali zao.

"Kumekuwa na maneno kwamba Jeshi la Polisi linaua watu, usalama wa taifa unaua watu nisema sio kweli na katika hili nipo tayari ‘chalenji’ ya mtu yoyote," amesema

Sheikh Kabeke ameongeza kuwa askari wamepewa dhamana ya kulinda amani, usalama na ustawi wa taifa, hivyo si sahihi kuwahusisha moja kwa moja na madai ya mauaji bila ushahidi.
Angalizo: Bakwata ni Jumuiya ya CCM na jukumu lake ni kuwaghilbu Waislam waiunge mkono CCM.
 
BAKWATA wamepewa na nani dhamana ya kuwa wasemaji wa Serikali?

Ukiwa mlinzi kwenye duka la mangi na mlango wa duka ukawa unavunjwa na vitu kuibwa mara kwa mara bila wewe kuona anayevunja na kuiba, wewe ndiye utakuwa mhusika wa huo wizi. No excuses!
Hajakuambia ni msemaji wa BAKWATA, hayo ni maoni yake km mtanzania. Kwani Charles Kitima ni msemaji wa TEC?
 
Akiingia Rais mkristo...

Hawa masheikh hutowasikia tena, ila watakuwa wanatoa lawama chini kwa chini...

Wenzao wakristo wataendelea kutoa waraka na matamko mbalimbali kumpinga kiongozi bila kujali dini yake...

Maana wana credibility hiyo...

Inasikitisha kuona makundi, matabaka na utengano katika taifa

maana utasikia mbwa mwitu, bakwata, tec, wasiojulikana, waandamanaji, chawa, yaani ni mvurugano ambao mwisho wake sio mzuri
 
Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke amesema si kweli kwamba vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinahusika na mauaji ya raia akieleza kuwa tuhuma hizo hazina msingi na zinapaswa kupuuzwa.

Akizungumza na Jambo TV ofisini kwake, Sheikh Kabeke ametolea mfano matukio yaliyojitokeza Oktoba 29, 2025 akisisitiza kuwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama hutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kiapo walichoapa cha kulinda nchi, raia na mali zao.

"Kumekuwa na maneno kwamba Jeshi la Polisi linaua watu, usalama wa taifa unaua watu nisema sio kweli na katika hili nipo tayari ‘chalenji’ ya mtu yoyote," amesema

Sheikh Kabeke ameongeza kuwa askari wamepewa dhamana ya kulinda amani, usalama na ustawi wa taifa, hivyo si sahihi kuwahusisha moja kwa moja na madai ya mauaji bila ushahidi.
Kama vipi Masheikh wa Bakwata wachukue nafasi ya Msigwa. Maana kila kona ya nchi tunazisikia kelele zao tu.
 
Aliyeleta uislam bongo alikosea sana. Wanawaza udini 24 hours. Mwingine kaanzisha jeshi lake linaitwa chui mweusi.
 
Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke amesema si kweli kwamba vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinahusika na mauaji ya raia akieleza kuwa tuhuma hizo hazina msingi na zinapaswa kupuuzwa.

Akizungumza na Jambo TV ofisini kwake, Sheikh Kabeke ametolea mfano matukio yaliyojitokeza Oktoba 29, 2025 akisisitiza kuwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama hutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kiapo walichoapa cha kulinda nchi, raia na mali zao.

"Kumekuwa na maneno kwamba Jeshi la Polisi linaua watu, usalama wa taifa unaua watu nisema sio kweli na katika hili nipo tayari ‘chalenji’ ya mtu yoyote," amesema

Sheikh Kabeke ameongeza kuwa askari wamepewa dhamana ya kulinda amani, usalama na ustawi wa taifa, hivyo si sahihi kuwahusisha moja kwa moja na madai ya mauaji bila ushahidi.
Basi uturuhusu tuseme wahusika ni akina Shekh wanaofuga Mbwa mwitu na Tiger?ama una maoni tofauti na yangu Shekh?
 
Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke amesema si kweli kwamba vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinahusika na mauaji ya raia akieleza kuwa tuhuma hizo hazina msingi na zinapaswa kupuuzwa.

Akizungumza na Jambo TV ofisini kwake, Sheikh Kabeke ametolea mfano matukio yaliyojitokeza Oktoba 29, 2025 akisisitiza kuwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama hutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kiapo walichoapa cha kulinda nchi, raia na mali zao.

"Kumekuwa na maneno kwamba Jeshi la Polisi linaua watu, usalama wa taifa unaua watu nisema sio kweli na katika hili nipo tayari ‘chalenji’ ya mtu yoyote," amesema

Sheikh Kabeke ameongeza kuwa askari wamepewa dhamana ya kulinda amani, usalama na ustawi wa taifa, hivyo si sahihi kuwahusisha moja kwa moja na madai ya mauaji bila ushahidi.
Kwamba waislam wote nchini wanafaidi nini ?

Na kwamba silaha nchini zinamilikiwa na nani ?

Walioonekana na silaha 29/10/2029 na sare ama za polisi au jeshi la Tanzania walipata wapi nguo za serikali na nani aliwatuma kuua ? Kwa nini waliotafuta maiti za ndugu zao walinyimwa kuona na maiti hizo kufanyiwa uchunguzi na kisha ibada stahili ?
 
Ama hakika dunia ya kizazi chetu mwenyezi Mungu ametuacha tuishi kwa utashi wetu,kuna vitu vinatokea very negative ila ajabu maisha yanaendelea.
Ingekua maisha ya babu zetu tunayoyasikia kuna watu wangenyakuliwa wazima wazima mchana kweupe tunashuhudia.
Najiuliza kile kizazi cha nyoka kipo kweli?
Nyoka yawezekana alimtia mimba Eva n ndio uzao utendao maovu kwa binadamu wenzao 😢
 
Back
Top Bottom