Sheikh Kishki yupo sahihi ila huyu Bwana Mdogo Shareef Firdaus ana nyota kubwa sana

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Kaka angu sheikh Kishki upo sahihi sana kuhusu sakata la huyu Bwana mdogo " Abdul Dunya" almaarufu " Shareef Firdaus".

Dogo ana karama sana ana nyota sana na anakubalika sana. Bora umpotezee tu.

Raia mitaani jijini Darusalama wanamkubali ile kinomanoma.

Kwa Raia mitaani, Kishki vs Shareef Firdaus ni sawa na YESU vs Baraba kwa wayahudi.

Waliambiwa kati ya Yesu na Baraba wanamchagua nani wakamchagua Baraba asie na haki mbele ya Yesu mwenye haki...

Yani ni sawa tu na ishu ya Kaini na Habili.

Habili alitoa sadaka yenye kuswihi ( yenye kukubalika mbele za Mwenyezi Mungu), Kaini akatoa sadaka isiyo swihi.

Mwisho wa siku Habili alie toa sadaka yenye kuswihi akauwawa na Kaini alie toa sadaka isiyo kubalika.

Cha kushangaza sasa Mungu akampromote Kaini, akampa kibali cha kuwa mtalii dunia nzima na akamuwekea alama kwamba ole wake atakae jaribu kumgusa Kaini.

Ushauri wangu kwa Sheikh Kishki.

Achana na Shareef Firdaus.
 
Nimeona mvutano wao youtube; dogo Sharifu ameanza kuuza maji na mafuta ya upako, chupa ya maji buku moja. Kishki amepinga kwa nguvu zote huku masheikh wakigawanyika kuhusu uhalali wa jambo hilo
Dini baana!
 
Sijui Ni uzee, sijaelewa kitu.
ni bifu kutoka Upande ule usiotumia nyama pendwa ambayo mapishi yake yaliiasisiwa na kabila linalozunguka mlima kilimanjaro.Kunadogo nayeye kutoka huo upande wa wapinga nyama pendwa ameibuka na kuiga style za kuongezea thamani mafuta ya kupikia yanayolimwa kwa wingi mkoa wenye mabinti wasiojua kusema NO badala ya Lita 10,000 amepambana anauza kwa Bei anayotaka.Sasa wameibuka wenzake wa huohuo upande unaopiga marufuku nyama pendwa na wazee wa kuvaa viatu vya wazi ilhali wao wakituuzia timberland tutimbe nazo kwenye nyumba zetu za ibada..Baadhi Hawataki kabisa na Wameanza kumpinga huyo dogo anayeonekana kwenye media anaushawishi kwa wenzake wa kuwamwagia hayo mafuta na wanamkubali balaa si wazee wala vijana wala kina Mama huwaambii kitu kutoka huo upande wenye kuvaa nguo za kujigubika bila kujali Hali ya hewa na Inaonekana kijiwe kimemchanganyia.
 
So ndg zetu wa makubazi nao wamempata 'Mwamposa' wao.
 
Yesu anaingia aje tena hapo sheikh?

You are very slow. Wewe hata ukiwa jambazi utauwawa eneo la tukio kwa sababu wenzake watakuacha na gari.

Hujui maana ya analogy?
 
Nimeona mvutano wao youtube; dogo Sharifu ameanza kuuza maji na mafuta ya upako, chupa ya maji buku moja. Kishki amepinga kwa nguvu zote huku masheikh wakigawanyika kuhusu uhalali wa jambo hilo
Kwamba hayo mafuta ndio yanaleta bahati, kuponya, kukuletea riziki etc.
Kwa namna hiyo, inakuwa ni SHIRIKI na ni kosa kubwa kwenye dini ya uislam.

Ile TAWHID inapotea.
 
Back
Top Bottom