Hili tatizo la ulafi litaisha lini? Tende zimetolewa msaada toka Uarabuni. Sisi hizi ndo zinatufanya tutembee tukisema tumefunga ili tuje zipata.
Wewe unakula tende na wake zako na watoto. Unanywea chai, unalia ugali. Si sawa. Hizo tende walitakiwa wapate watu wote. Zigawiwe msikitini hapo Mburahati. Maana nasikia hata waliopewa Tandale nako zimefanyiwa uhuni na Sheikh Mtopea anauza.
Hii si sawa. Tusipitilize please katika njaa zetu. Tukumbuke bila tende sisi kufunga kwetu hakuna maana na hatutafunga sasa. Watu wanaonesha upendo wanatupatia msaada wa tende unakula wewe na wake zako watatu na mitoto yako mivibaka?
Si sawa huo ni ukorofi. Kwa nini tende zote ule wewe? Ukorofi huo. Ndiyo ni ukorofi. Yaani sisi tule mitambi tu na uji wa pilipili. Nyie mle tende? Huo ni ukorofi. Bakwata mliangalie hili.