Sheikh Mkuu amuombea dua Waziri Mkuu aoe mke wa pili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amemuombea dua Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aoe mke wa pili ilia pate utulivu zaidi katika mizunguko yake.

Ameyasema hayo wakati Waziri Mkuu alipokuwa mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi Julai 2, 2022.
 
Atakua kuna kajambo kakaona au kakasikia kuwa hatulii ni mtundu.
 
Duh!
Shehe anajuaje labda PM anatoshelezwa kikamilifu na huyo mmoja?!!!
 
Asimuingize mwenzake chaka, kwani yeye anao wawili?
  1. Ameona aliyepo hamtoshelezi?
  2. Amemuona anatamani sana kama yule wa Pangani?
  3. Au an binti anataka kumpasia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…