Kaka suala hapa si kuutetea UISLAMU,hapa tatizo ni viongozi wetu wamekuwa waropokaji mno.Waathirika ni sisi wananchi wa kawaida ambao tunaishi vyema bila kujali dini zetu.
Sijaona sababu za msingi za Lukuvi kupanda madhabahuni nakuanza kufanya nasaha zisizokuwa na kichwa wala miguu.Na kwa mawazo yangu sababu huyu alienda kumwakilisha WM basi nina uhakika aliloliongea linabaraka ya serikali yetu sikivu.
Na mwsiho kaka yangu muda wote wanaoanzisha vita ni viongozi waliomadarakani.Hebu tuone Cetral Afrika kinachotokea leo,viongozi wamekimbilia ughaibuni wao na familia zao, wamewaacha raia wakiuana wenyewe kwa wenyewe kama kuku kwa sababu ya dini zao.Leo mashekhe na maaskofu ndiyo wanaopiga kwata kutafuta marithiano, na wakifanikiwa watakuja haraka kutaka kufanyika kwa UCHAGUZI,na waliokuwa wanauawa hawatadhaminiwa kamwe,dhamani yao ni kwenye KURA tu.
Tuwaone na hawa nchi changa zaidi Afrika South Sudan,nao ni yale yale waliopingana ni wanasiasa leo kiama kwa raia wa kawaida,masikini wasio na hata muelekeo wa kesho tutakuwa hai au lah,viongozi wamezikimbiza familia zao ughaibuni na wanasiasa wako busy kwenye 5STAR hotels wakifaidi maisha,wakibishana huku raia wakiteketea.
Leo Lukuvi anafanya yale yale yaliyofanywa na Viongozi wa Central Afrika na South Sudan,chama tawala,wanasheria,waandishi wahabari,kiongozi mkuu wa nchi,hawa wote wamenyamaza kimya wanasubiria bomu lipasuke wakimbilie ughaibuni wao na familia zao na raia tumalizane,vita ikiisha (Tukishamalizana)watarudi kuendelea kutawala.:shock::A S cry:😕