Sheikh mkuu wa mkoa wa dar es salaam amesema maneno ya mh lukuvi kutasfiriwa vibaya.ameonya waislamu kuwa waungwana na wasimwelewe vibaya lukuvi sbb hakuwa na nia mbaya,ni watu wachache au kikundi cha watu wenye nia ovu kutumia maneno ya lukuvi kisiasa na kiimani alisema sheikh.hi ni kwa mujibu wa magezeti asubuhi rfa
Huyu lazima afie korokoroni!Hapa ndipo namkumbuka sana Sheikh Ponda.
Thanks mkuu, inasikitisha kuona mtu anaweka maslahi yake mbele kuliko kutetea Uislam.
Huyu lazima afie korokoroni!
Kaka suala hapa si kuutetea UISLAMU,hapa tatizo ni viongozi wetu wamekuwa waropokaji mno.Waathirika ni sisi wananchi wa kawaida ambao tunaishi vyema bila kujali dini zetu.
Sijaona sababu za msingi za Lukuvi kupanda madhabahuni nakuanza kufanya nasaha zisizokuwa na kichwa wala miguu.Na kwa mawazo yangu sababu huyu alienda kumwakilisha WM basi nina uhakika aliloliongea linabaraka ya serikali yetu sikivu.
Na mwsiho kaka yangu muda wote wanaoanzisha vita ni viongozi waliomadarakani.Hebu tuone Cetral Afrika kinachotokea leo,viongozi wamekimbilia ughaibuni wao na familia zao, wamewaacha raia wakiuana wenyewe kwa wenyewe kama kuku kwa sababu ya dini zao.Leo mashekhe na maaskofu ndiyo wanaopiga kwata kutafuta marithiano, na wakifanikiwa watakuja haraka kutaka kufanyika kwa UCHAGUZI,na waliokuwa wanauawa hawatadhaminiwa kamwe,dhamani yao ni kwenye KURA tu.
Tuwaone na hawa nchi changa zaidi Afrika South Sudan,nao ni yale yale waliopingana ni wanasiasa leo kiama kwa raia wa kawaida,masikini wasio na hata muelekeo wa kesho tutakuwa hai au lah,viongozi wamezikimbiza familia zao ughaibuni na wanasiasa wako busy kwenye 5STAR hotels wakifaidi maisha,wakibishana huku raia wakiteketea.
Leo Lukuvi anafanya yale yale yaliyofanywa na Viongozi wa Central Afrika na South Sudan,chama tawala,wanasheria,waandishi wahabari,kiongozi mkuu wa nchi,hawa wote wamenyamaza kimya wanasubiria bomu lipasuke wakimbilie ughaibuni wao na familia zao na raia tumalizane,vita ikiisha (Tukishamalizana)watarudi kuendelea kutawala.:shock::A S cry:😕
Huyu mkuu wa bakwata dsm nilikuwa namheshimu sana na hata kwenye vikao vya dini tulipokuwa tunakutana naye tulijua ni miongoni mwa watu wasafi na wenye mtazamo wa kitaifa. Kwa alilofanya Jana ninaanza kuwa na wasiwasi nae
Mungu anasema ktk vitabu vitakatifu kuwa, waheshimuni wale wenye mamlaka juu yenu! Watanzania jifunzeni kuwaheshimu viongozi wenu hata kama wamekosea , tuoyeshe alipo kosea kwa hoja sio matusi
umeeleweka
Lukuvi hajahamasisha watu kufanya vurugu, bali ametoa maoni yake na namna anavyoiona nchi inakoelekea! Lakini Ponda amekuwa akiwahamasisha watu kufanya vurugu na pia amekuwa akifanya mikutano ambayo mwisho wake huchochea watu kufanya vurugu!Kwani huyo Shekhe Ponda anatofauti gani na Lukuvi?Au huyu sababu ni Waziri kwenye chama chetu?Tuwe watu tunaomuogopa Mungu,haki lazima itendeke.Hata Lukuvi anastahili kufia korokoroni.Haijalishi wadhifa wake.
Sheikh ubwabwa huyu....
Lukuvi hajahamasisha watu kufanya vurugu, bali ametoa maoni yake na namna anavyoiona nchi inakoelekea! Lakini Ponda amekuwa akiwahamasisha watu kufanya vurugu na pia amekuwa akifanya mikutano ambayo mwisho wake huchochea watu kufanya vurugu!
Nadhani utakumbuka alivyowahamasisha watu kususia sensa na pia alivyowaongoza watu kuvamia kiwanja cha wenyewe akidai ni mali ya waislamu!