Ni jambo jema
Alitoa siri kwamba Mchakato wa kuomba Mahakama ya Kadhi Serikalini haukufika mwisho
Nikajua tu ameshajivuruga!
Tena mbele ya DG wa TISS sheikh Rashid Othman mstaafu tarehe 29 January 2023
The Director of Tanzania Intelligence and Security Services (TISS), Mr Rashid Othman ....
TOKA MAKTABA :
AN NUUR gazeti Habari
SIKU ya Ijumaa tarehe 3
Agost 2012
Sheikh Mohamed Idd aliulizwa maswali kuhusu kadhi wa BAKWATA na yeye akajibu maswali hayo kwa maudhui yenye kichwa cha habari: “Kumpokea Kadhi ni nusu shari na kumkataa ni shari kamili.”
Chini ya kichwa cha habari hiki kuna maoni mengi kuhusu kadhi huyu lakini kwa bahati mbaya, yote yalikua ni ya kukurupuka tu. Bali hata hicho kichwa cha habari chenyewe ni cha kukurupuka tu kwa sababu katika Uislamu hakuna lugha hiyo.
Kwamba kitu kimoja hicho hicho kukikubali ni dhambi ndogo na kukikataa ni dhambi kubwa. Istilahi ya aina hii Sheikh Mohamed Idd kaipata wapi? Hata huko TAMTA alikosoma istilahi hii haiko.
Suala hili liko wazi kuwa huu ni munkar na ni wajibu juu ya Waislamu kuupinga na kuuondoa kwa nguvu zote. Serikali ilitoa ahadi nyingi (kupitia Waziri Mkuu) Kumkataa Kadhi huyu wa Bakwata ni wajibu kwamba ahakama ya Kadhi itarejeshwa kwa utaratibu mzuri ambao utaweza kuwaridhisha Watanzania na mchakato wake bado ulikua unaendelea.
Mara Mufti wa Bakwata anakurupuka na makadhi wake ni vipi? Hivi Sheikh Mohamed Idd hili halioni kuwa ni munkar na ni khiyana kubwa ambayo Mufti Simba kawafanyia Waislamu?
Kukurupuka huku ni dalili kwamba Mufti mwenyewe ni dhaifu na kwa sababu ya udhaifu wake, watu wenye
tamaa ya ulimwengu wanapata nafasi ya kumtumia.
Hatua hii ya Mufti wa B a k w a t a k u k u r u p u k a haikua ni ya bahati mbaya kama Sheikh Mohamed Idd anavyodhani, ilikua na malengo maalumu na baadhi yake ni haya yafuatayo: Ni kutaka kutetea ushabiki
kwa lengo la kuendelea kuwagawa Waislamu kwa matakwa ya kanisa.
Pili, Mufti wa Bakwata anafanya hivyo ili kuwahi kulinda nafasi yake mapema. Kwa sababu Mufti alikua a n a j u a k w a m b a w a l e mashekh wa taasisi nyengine ni wanazuoni wenye elimu ya juu kuliko yeye, kama ukadhi utapatikana katika mchakato ule, yeye Mufti wa Bakwata ataambulia sifuri. Hali kadhalika Sheikh Alhadi Musa hilo alikua analijua.
Tatu, hili ndilo la umuhimu zaidi na ndilo linalobainisha faida kubwa waliyoipata Maaskofu. Ni wazi kwamba
Maaskofu hawaridhiki sisi Waislamu tuwe na uhuru wa kuabudu hapa nchini, na katika huo uhuru wa kuabudu
ni kuwa na Mahakama ya Kadhi. Wanafurahi Mufti akiteuwa makadhi kwa sababu wana hakika kwamba atateua watu dhaifu (wachovu) ili Mahakama ya Kadhi nayo iwe dhaifu. Na hiyo ndiyo sera ya BAKWATA tangu
siku Mwalimu Nyerere alipoianzisha. Sera ya kuudhoofisha Uislamu kwa kuwateulia viongozi dhaifu.
Hebu Sheikh Mohammed Idd fikiria wewe mwenyewe kama hiki si kichekesho. Unateuwaje Kadhi kabla hujaunda Mahkama yenyewe? Nini hadhi ya Kadhi wa Bakwata katika mfumo wa Sheria nchini hivi sasa?
Sheria gani ya nchi imewekwa kumtambua Kadhi huyo, kazi zake na mamlaka yake? Kipi kimezidi au kupungua katika mfumo wa Mahkama nchini kabla na baada ya Mufti wa Bakwata kutaja Kadhi? Mbona tunakuwa wapofu na wachovu wa kujua mambo kiasi hiki?
Imeandikwa na : Saidi
Kesi Mbwimbwi