Sheikh Mohamed Said heko wewe ni gwiji la historia Sasa mambo yanajitokeza hadharani!

Sheikh Mohamed Said heko wewe ni gwiji la historia Sasa mambo yanajitokeza hadharani!

Status
Not open for further replies.

Mdondoaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Posts
5,108
Reaction score
1,137
Asalaam aleykum Al-Akh,

Sheikh Mohammed Said kwa muda mrefu tumekuwa tukijadiliana kwa marefu na mapana kuhusu historia ya Tanzania. Ukaleta kitabu cha life and times of Abdulwahid Sykes watu wakakubeza. Kikaja kitabu chengine cha the Rise of Muslim Militants wakakubeza.

Ukweli umeanza kujitokeza bungeni sasa baada ya Tundu Lissu kumwaga hadharani mtama kuwa kiini cha Tatizo la nchi hii ni nani na kwanini? Na mambo yanavyozidi kwenda mbele nadhani mengi yatajitokeza hadharani.

Kassim Hanga alivyokuwa ametamkwa nilitokwa na machozi kwani kwa muda mrefu watu wamekuwa wakiogopa kusema what happened to this person na who is responsible for his death. Na wengineo wengi.

Binafsi nakupa hongera ukweli umeanza kudhihirika. Na akina Nguruvi, Mwanakijiji na wengineo mtakeni Radhi Sheikh Mohammed kwa kumbeza na usoni mambo yatazidi kuja hadharani na mchakato wa katiba hii.

Nilikuwapo!
 
Ndugu yangu uko sahihi kabisa,siku zote subira huleta nuru kwenye mikanganyiko.Yanayosemwa sasa kwenye bunge maalumu la katiba Sheikh Mohamed aliyazungumza kabla na watu wakambeza na kumuita mchochochezi akiwemo rafiki yetu Yericko Nyerere.

Juzi nimestaajabu kumsoma Yericko Nyerere aka Jason Bourne akiandika maneno ya kifedhuli kabisa kuhusu mwalimu Nyerere.Sijui yale mahaba yake yamefutika vipi.Kipindi chote cha mjadala wa sheikh Mohamed Said sijasoma hata sehemu moja akimkosea adabu mwalimu Nyerere japokuwa yeye alikebehiwa sana.Inshallah hata ule ukandamizaji wa waislamu kwenye elimu na utawala kuanzia kipindi cha mwalimu mpaka sasa ipo siku utakuja kufunuliwa kama ujanja ujanja wa mwalimu katika muungano unavyoanikwa leo hii.
 
Time will tell tusubiri Ukweli hupanda ngazi pole pole hadi mwisho wa safari ijapokuwa uongo hutumia lifti unapopanda .
 
mmh na mie ngoja nipite kwanza nikakimbizane na kibarua will pop in again from 5 pm to see how my fellows will give their inputs
 
sijajua kwanini ccm wanatuburuza katika suala la Muungano. ila muda utafika na kuongea ukweli, ni wakati wa kujua ukweli juu ya historia ya nchi yetu na muungano.
 
Mkuu Ritz,

Tafadhali naomba uwalete wale vinara wa ufia Unyerere humu-JF...akina Nguruvi3,Mag3,Mwanakijiji,Chama wa Gongo la Mboto na vilaza/wanafiki wenzao wangine...ili nije kuwasuduku hapa hapa jamvini!

Hayo yanayowekwa hadharani kwasasa kukhusu unyama wa yule Nyerere...mbona ni kiduchu mno!? Yaani pana uchafu na uharamia mwingi mno wa yule Julius alofanza kwa Watanzania wengi tu wasio na hatia!

Tutauweka ukweli woote hadharani na kuwazindua misukule yoote iliyopo kwenye comma...hoja uhai!

Yericko Nyerere,njoo hapa uje kumtetea yule Babako Mzazi,au!?

Ahsanta sana.
 
Alichosema Tundu Lissu Bungeni kuhusu Nyerere ndicho anachokisema kila siku humu JF Mzee Mohamed Said.

Bahati nzuri leo hii watu wengine tena viongozi wa vyama vya upinzani unamuongelea Nyerere alichowafanyia Watanzania.

Shukran sana Akhy Mohamed Said

Nakala gombesugu

Mkuu Ritz...Shukran na nimekusoma!

Sasa Watanzania woote kwa pamoja,bila ya kujali itikadi zao za kisiasa,imani zao za kidini au matabaka yao...wamechoshwa kuzidi kuendelea kuwa misukule ya Baba wa Taifa!?

Yaani Sheikh Mohamed Said alianzisha cheche hizi,sasa imekua kama vile relay race...hata baadhi ya Wanasiasa/Wabunge nao pia wameamua kumchana yule Baba wa Taifa!?

Yaani Tundu Lissu ameamua kumwaga ugali na kutoboa sufuria kabisa!? Daah! Chadema bana! Teeeh! Teeeh! Teeeh!

Ahsanta.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Ritz,
msimamo wako ktk mchakato wa kutunga katiba mpya ni upi?.serikali mbili/tatu?.
 
Last edited by a moderator:
Kuna harufu kubwa sana ya udini hapa, ngoja nikae pembeni nipige chabo kwa mbali

Yaleyale...yaani hata baadhi ya wenzenu hivi sasa wameshachoshwa na hizi cheap excuses zenu!? Daah!

Yaani Watanzania wakijadili au kumzungumzia yule Dikteta Nyerere,ndo wamekua wadini!?

Acheni kutumia siasa za kuchafuana na hoja muflis kwenye mijadala kama hii!

Nyerere alizoea kuishi kwa urongo,udanganyifu,vitisho na uzandiki! - By Hon. Tundu Lissu Chadema MP and Chief Political Strategist!

Ahsanta sana!
 
Haya Jussa,

Naye amewauliza huu upitishwaji wa sahihi wa siri wa zaidi ya siku moja kwa makamu wa rais ulilenga nini na kwanini baada ya kutia sahihi Zanzibar imekuwa ikilalamika kuwa benki kuu yake na sarafu yake imepotea???
 
mkuu Ritz,
msimamo wako ktk mchakato wa kutunga katiba mpya ni upi?.serikali mbili/tatu?.

wee Kadoda11! Usijeleta yale mambo yako ya udini hapa jamvini,plse!?

Maana naona nyinyi wafia Unyerere na vinara wa Islamophobia humu-JF...mmeshaanza kuitana na kusogea hapa jamvini...nafahamu yakua hamna hoja zozote za maana mtakazoleta kwenye mjadala huu ,zaidi ya matusi na kashfa ili ufungwe,au sio!?

Hivi kwanini anapojadiliwa yule Nyerere na Watanzania ambao kwa mitazamo yenu mnawaona/mnawakhis labda wao ni Non Catholics and/or Non Christians...you perceive them as a threat!?

Kwani hivi nyinyi mnataka yule Nyerere kujadiliwa tu na Makatoliki wenzake na Makasisi tu ndani ya Makanisa,sio!?

Ule utawala mbovu na wa kimabavu wa yule Dikteta Nyerere...uliathiri takriban Watanzania woote bila ya kujali dini/imani zao...na mpaka kesho Watanzania soote kwa pamoja tunazidi kutafunika kwa hii legacy chafu alotwachia yule Baba wa Taifa!...khasa sisi wanyonge tulioko huku vijijini!

Acha kujitoa ufahamu Mkuu...najua umenisoma hapo ninamaanisha nini!?

Nakutakia siku njema!

Ahsanta.
 
Last edited by a moderator:
Alichosema Tundu Lissu Bungeni kuhusu Nyerere ndicho anachokisema kila siku humu JF Mzee Mohamed Said.

Bahati nzuri leo hii watu wengine tena viongozi wa vyama vya upinzani unamuongelea Nyerere alichowafanyia Watanzania.

Shukran sana Akhy Mohamed Said

Nakala gombesugu

Ritz

Naona kama kawaida moderators wameipotezea ila Mohammed Said ameyazungumza yale ambayo hapa mjini watu wamekuwa wakiyafahamu siku nyingi. Na sasa huko bungeni ndio yaanza kutiririka vizuri.
 
Haya Jussa,

Naye amewauliza huu upitishwaji wa sahihi wa siri wa zaidi ya siku moja kwa makamu wa rais ulilenga nini na kwanini baada ya kutia sahihi Zanzibar imekuwa ikilalamika kuwa benki kuu yake na sarafu yake imepotea???

Daah! Nimekusoma na mangi mno yanasikitisha pasi mipaka!

Hakuna liso mwisho...leo nani alijua ati ingalifika siku hata Mwanachadema angeamua kuichana na kuivua nguo maiti ya Baba wa Taifa ndani ya Bunge!? Daah!

Ahsanta.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom