Serikali ya Tz imeshughulikia ugaidi wa Sheikh Farid na wenzie kwa namna bora kabisa. Usitafute ushahidi kama wanavyoatoa ushahidi wa kesi za ufisadi. Nakumbuka siku ya kwanza baada ya ule mhadhara kulitokea maandamano kwenda kituo cha polisi Madema, kisha kanisa la TAG kariakoo likachomwa moto.
Mapadri walipigwa risasi akiwemo Padri Evaristi, Watalii walimwagiwa tindikali, Wageni walichapwa viboko kwa kuvaa nguo fupi. Kama Serikali isingechukua hatua sitahiki pengine ZNZ ingegeuka kuwa Mogadishu au Kismayu au Syria.
Marekani kupitia jarida la Chuo Cha Ulinzi liliitaja UAMSHO kama kundi la ugaidi na viingozi wake waandamizi walipewa mafunzo Kandahar.
Tuamini ilichofanya Serikali kwa kuwa ni kwa masilahi mapana ya nchi yetu, wewe mwenyewe
Mohamed Said na Mimi. Jiulize kwa nini wasikushike wewe binafsi na wakamshika Sheikh Farid na Sheik Mselem.
Naamini siyo kila taarifa ya Serikali na kwa ajili ya umma wote wa Watanzania, zingine ni kwa matumizi ya vyombo vya dola tu.