Sheikh Said Mwaipopo ametoa tuhuma nzito dhidi ya Makamu Mwenyeiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, akimtuhumu kwa vitendo vya utapeli na kujipatia fedha kwa njia za kutisha matajiri.
Katika maelezo yake, Sheikh Mwaipopo amedai kuwa Heche alisafiri hadi nchini Afrika Kusini na kupokea kiasi cha dola laki mbili kutoka kwa mfanyabiashara anayeishi Afrika Kusini akifahamika kwa jina la 'Nilesh', kwa lengo la kumsafisha kisiasa na kumtengenezea sifa nzuri.
"Heche amekuwa yeye ndio kinara sana wa kusema viongozi wa kiserikali kwa ubaya kwamba ni wezi, mafisadi. Heche nilimsikia akimsema waziri mkuu, Mwigulu Nchemba; kwamba Mwigulu Nchemba hana lolote, hana maana, kazi yake ni kusuluhisha ndoa. Sasa kwa nini yeye tukimgeuza na yeye tuone kama analika, tunamkuta na yeye amechacha, amevunda?"