The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Kiongozi wa Taasisi ya Asaalam Islamic Foundation Sheikh Muharram Mziwanda ameeleza kushangazwa na Kauli ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) kuwa kilichofanyika Oktoba 29, 2025 ilikuwa maandamano na si vurugu, uharibifu na wizi kama ilivyoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini, akiitaka TEC kuachana na matamko aliyodai kuwa yanachochea ghasia na hasira.
Sheikh Mziwanda amebainisha hayo Jumapili Novemba 16, 2025 Jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari, akirejea kauli ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa waliowahi kueleza kuwa Oktoba 29 wangekinukisha, kufanya uasi na kuvuruga uchaguzi mkuu.
Akirejea kauli ya Rais wa TEC, Askofu Wolfgang Pisa, Sheikh Mziwanda amehoji lilipokuwa baraza hilo wakati kile alichokiita kauli za chuki, hasira na hamasa zilipokuwa zikitolewa na baadhi ya wanasiasa, huku pia akieleza kusikitishwa na namna ambavyo TEC hawajaeleza chochote kuhusu uharibifu na wizi wa mali za umma na za watu binafsi uliotokea hapo Oktoba 29.
"Kuna wakati hadi unauliza au baraza linahusika? kwasababu mapito wanayopita TEC yanatutia mashaka. Na mimi niwazindue wananchi kwamba yale hayakuwa maandamano kwa mujibu wa waasisi wa tukio lile kwasababu wao walisema wanaenda kukinukisha. Mimi niombe hata kama viongozi wa dini tunashiriki kwenye harakati basi tuzingatie harakati zenye maslahi kwa nchi yetu." Amesema Sheikh Mziwanda.
Mziwanda ameliomba Baraza la Maaskofu kusimama katika nafasi yao ya kushirikiana na serikali katika kuijenga nchi, akiwataka yale yote yanayoashiria amani waliunge mkono na yote yenye kuhatarisha amani wayakemee ikiwamo kauli zilizokuwa zikitolewa mapema za kuhamasisha na kutangaza kuhusu vurugu na ghasia hizo za Oktoba 29, 2025.