PostGE2025 Sheikh Ndauga: Nguvu hutumiwa kwa ulinzi na siyo kuadhibu sauti za wananchi

PostGE2025 Sheikh Ndauga: Nguvu hutumiwa kwa ulinzi na siyo kuadhibu sauti za wananchi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
"Tunatoa wito kwa serikali na taasisi za ulinzi na usalama
kutumia utaalamu busara na weledi katika kudhibiti misuguano kuepuka matumizi ya nguvu kupita kiasi, kushughulikia sababu badala ya dalili.

Kujihusisha na mazungumzo ya kujenga nchi badala ya vitisho na matumizi ya nguvu. Katika taifa lolote lililojengwa katika misingi ya amani haki na upendo na uongozi wenye utu Nguvu hutumiwa kwa ulinzi na siyo kuadhibu sauti za wananchi.

Tunashauri kuanzishwa kwa mfumo wa haki uadilifu na usawa wa kudumu wa majadiliano kati ya serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa na vijana ili kujenga tamaduni na kusikilizana kabla migogoro haijafikia kiwango cha ghasia na uvunjifu wa amani"

Wito huo umetolewa na Sheikh Abdallah Ndauga, Rais wa Umoja wa Wanazuoni Tanzania (Hay-Atul Ulamaa), wakati akiongea na Waandishi wa Habari, Novemba 17,2025.


 
sasa itakuwaje kwa mashekhe ubwabwa wa bakwata
 
Back
Top Bottom