Sheikh Ponda huwa ana tatizo gani? Kwanini anaogopwa sana?

Kumbu kumbu nzuri za sheikh Ponda anazo Omari Mahita, na utawala wa hayati Benjamin Mkapa.

Pale kwenye vurugu za mwembechai ni kielelezo tosha cha Ponds nakumbuka alikuwa akitafutwa na polisi na aliwaambia nitaenda kusali siku ya Eid na hamtanikamata na kweli alilifanya hilo kwa kuvaa nikab na hawakumtambua.

Huyu sheikh ni mwamba sana na serikali inajua nguvu yake wewe raia tu hauwezi kujua na inawezekana haya tunayoyasema wewe ulikiwa bado mtoto au bado ulikiwa haujazaliwa.
 
jamaa lakini mbona sio muongeaji sana, ila akiongea kidogo tu kunakuiwa na reaction kubwa either anakamatwa au anajibiwa na viongozi wengio wa Kiislam
 
Huyu Shehe ni msema ukweli na anapenda haki. Hamezi maneno na anayatamka kama yalivyo pasi na kupepesa macho. Kama mfalme yu uchi, hatasema kavaa nguo za rangi nzuri. Kamwe hasemi kijiko kikubwa bali atasema koleo. Siku zote watu wa aina yake hawakosi maadui na ndivyo ilivyo kwa huyu Shehe.
 
kwani kwenye hizo vurugu yeye alifanya kitu gani exactly hadi wakataka wamkamate na akawa anaogopwa hadi leo
 
Ponda anajua kujenga hoja na kuitetea nimtu mtulivu sana anapokua anaongea ni kweli ni mtu hatari kwani ukimuacha dakika watu wapo barabarani nimeshuudia Dodoma watu wanaapa kulinda kura. Ponda ni namba nyingine.
 
Mwana siasa aliyevaa joho la u-shekh kama cover up. Atafute jimbo agombee kama Gwaji.
 
Mwana siasa aliyevaa joho la u-shekh kama cover up. Atafute jimbo agombee kama Gwaji.
1 man army Bakwata tuna waona..mlishindwa kuita vyombo vya habari adi mkaenda kwenye mkutano wa fisiemu
 
Mtu ambaye sio mnafiki, huchukiwa na wengi
 
Ni mkweli na mpenda haki.
Lazima ataogopewa
 
Kama ana siasa kali za kuleta chuki na anaweza vunja amani basi lazima aogopwe, na twajuwa dola itakushughulikia kivipi...
 
Mji gani sheikh?
 
Kama ana siasa kali za kuleta chuki na anaweza vunja amani basi lazima aogopwe, na twajuwa dola itakushughulikia kivipi...
Anaevunja amani ya nchi hii wewe humjui?
Look around you.....
Utamuona anaendeshwa kwenye Viieite
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…