PreGE2025 Sheikh Ponda: Tushiriki Uchaguzi, Piga kura kisha Linda Kura yako

PreGE2025 Sheikh Ponda: Tushiriki Uchaguzi, Piga kura kisha Linda Kura yako

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sheikh ponda kishaanza kuingizwa mkenge kuchanganyika na wahuni.
Daah ACT ni wahuni tu
 
Hawa watu wanaokuja na mawazo haya wanaishi tanzania au wako kenya kwa majirani, ETI TUTALINDA KURA, hii elimu tunayofundishwa mashuleni na vyuo vyetu ni bure kabisa, sioni hata faida yake. Unalinda hizo kura wewe ni polisi, hata mguu pande hujui, watu mna masiala
 
Ustaadhi kaingia mkenge.....unazilindaje sasa hizo kura....mtu ambaye mimi nilimuelewa ni Bwege....alisema wazi no mpaka ccm waamue kukutunuku....ila kulinda ni uongo...hii dol katili unalindaje....watu wpo radh kunynga
 
Yaan hawa watu wangekuwa serious.....the best way ilikuwa ni kuungana wote watake reforms....baada ya kuzipata angalau sehemu zile wana nguvu wangechukua majimbo.....sasa hv sehemu wenye nguvu yupo anayetmia dol...wanachomokaje kwa wvnja minguu na uno😂..ukikomaa sana unptzwa
 
Ponda, Ado, Dorothy, Mchinjita wanaunguruma ndani ya Viunga vya Manzese, Juni 18, 2025

"Safari hii tutatangazwa watake wasitake! Wabunge wa upinzani huenda bungeni kwa nguvu ya ulinzi wa kura. Kupiga kura ni haki, na kulinda kura pia ni haki." Naibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo.
​

Wamesahau kama wamesaini mkataba wa maadili ya uchaguzi moja wapo ni kuto kulinda uchaguzi na wasimamizi kutokuwa na simu janja ili msimamizi asipige picha za matokeo ya uchaguzi na kusambaza
 
Naona ustazi nae ameshaanza kunywa vinywaji vilivyopigwa marufuku.
 
Keshafika bei huyu. Hana lolote.

Unaendaje kupiga kura ukijua kuna wizi? Si wehu huo. Kwa nini usidai mabadiliko yatakayohakikisha kura zinakuwa salama muda wote?

typical mentality za kichadema, kila asiekubaliana na msimamo wao kafika bei. Munakosa hata aibu
 
Nawaza Kwa sauti kubwa sana. CCM na serikali yake wamenunua silaha za kutosha. Uchaguzi wa serikali za mitaa masanduku yaliingizwa Kwa nguvu na wakurugenzi yakiwa yamejazwa kura wakipewa ulinzi na TISS na Tanpol,mawakala hawakuwepo vituoni.

ACT wanapaswa kufikiri broadly vinginevyo mchezo ule ule wenye biashara yao washatia fedha kwapani mapema.
 
Unalindaje wakati tayari mlisaini fomu za maadili ambazo hata simu hamtakiwi kuwa nazo vituoni na wamewaandalia vita wale watakaovuruga uchaguzi.
Elimu ya nchi hii inayofundishwa shuleni ni hovyo kabisa.
FB_IMG_1750006752704.jpg
Heche aliuliza,ni elimu au matope?
 
typical mentality za kichadema, kila asiekubaliana na msimamo wao kafika bei. Munakosa hata aibu
Huo ndo ukweli. Kataa kubali shauri yako.

Hakuna siasa genuine na serious za kuiondoa CCM madarakani huko ACT Wazalendo. Hakuna siasa za kuwaletea wananchi mabadiliki ya kweli kwa faida za kweli kwenye hicho chama.

Na huyu Sheikh kujiunga huko ndo yaleyale ya kufika bei hakuna jipya.
 
Ponda angebaki tu kuwa mwanaharakati wa Kiislamu kwani Bakwata tayari ni kitengo cha CCM hivyo haitetei maslahi ya Waislamu, ni yeye Sheikh Ponda peke yake ndiye alikuwa mtetezi wa Waislam.
Naungana na wewe kabisa. Shehe kaingiaje huku? Kazi yake ya Shura ya Maimamu inadorora wakati anafanya kazi nzuri sana kwenye majukwaa ya haki ya mwenyezi Mungu.
Halafu mbona hawasemi watalindaje wakati moja ya kipengele kwenye maadili ni kupiga kura halafu ondoka ukakae mita 100 au kwako usubiri utangaziwe mshindi? Inamaana hawakukiona hiki wakati wa kusaini maadili mpaka waanze kulazimisha wanachi kuvunja sheria za uchaguzi na kufanya vurugu bila sababu?
Shehe wetu baki njia kuu kwenye Shura ya Maimamu.
 
Back
Top Bottom