Sheikh wa Mkoa wa Dar ashangazwa na jinsi watu wanavyojipa Uaskofu hovyo hovyo mitaani

Huyu Sheikh huwa ana points Sana....! Kama hapo kuna ujumbe fulani anaufikisha Kwamba hizi nafasi Za Uaskofu inabidi zitendewe haki. Sio Mtu Kala Maharage Kashiba anajiita Askofu...!
 
Takbiiir
 
Sheria ya Ili uwe mchungaji/Shekhe degree ya philosophy iwe lazima from accredited universities,na sio hizo Ph.D za jalalani za kina Gwajiboy.
 
He is right kuwa askofu kanisa katoliki ni sala na toba siyo rahisi hata kidogo. Ila makanisa ya siku hizi eti hata Masanja askofu. Tuna utani na Mungu
 
Ila kuna ujinga mwingi mtaani siku hizi, hata mimi kesho naweza kujenga kibanda changu, tukaweka speaker uchwara na familia yangu then naanza kujiita mtume/nabii/askofu e.t.c, eti naponya Corona, Kansa, and nafufua misukule! Ni ujinga na fujo, Sheikh yupo sawa
 
Haya makanisa ya mifukoni mwa watu ndio yamekuja kuharibu kila kitu, watu wanajipachika hilo jina kutafuta mkate wao wa kila siku.
Huwa wanaanza choka mbaya, mtafute baada ya miaka miwili utashangaa, and ni bullies, wanawapelekesha sana waumini wao!! Huo upuuzi wa hawa maaskofu uchwara nimeupiga marufuku home kwangu
 
Vipi kuhusu yeye na Usheikh wake alinunua wapi? Vipi ahadi yake kuhusu Mange? Mbona bado anadunda kitaa?
Nadhani tujadili hilo alilosema, hayo mengine tumwachie yeye
 
Mambo ya Ngoso wawaachie kina Ngoso wenyewe, maana hawa watu wakisemwa hawakawii kutoa hukumu za kifo! Sasa sijui kipi afadhali, kutoa hukumu za kifo kwa makosa ambayo yanasameheka au kujipachika uaskofu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…