Leo kwa bahati nzuri nimepitia sehemu nikakuta kuna issue ya msikiti wa Mtoro wakimuoba msamaha Mufti, nikataka kuangalia nini kimetokea tarehe 29 ya Ramadhan.
Nikarudi kutafuta clip nikaipata kumbe kuna Shekh msikitini alisahihisha kauli ya kidini aliyotoa siku alipoenda kufunga darsa wanaita "Busati" , Mufti alisema siku ya shaka ni 29 Ramadhan kwa maana hujui mwezi umeandama au hapana lakini baada ya kuondoka Shekh wa msikiti akasema kwa heshima tu Mufti ulimi umeteleza kidini imeandikwa siku ya shaka ni 30 sio 29. Bwana jamaa wakapigiwa simu saa 7 usiku watu wameshalala kuwa lazima waombe radhi msikitini kabla swala ya Eid kuanza na wakafanya hivyo.
Kwa maoni yangu Mufti ni kweli aliteleza lakini namuona ni mtu fulani anapenda kutukuzwa sana na yuko busy kupigania kitu kinaitwa mamlaka hata mambo ya mwezi alitumia dakika 15 kulilia mamlaka ya kutangaza mwezi kuwa ni yeye tu, sasa shida yote hii ya nini? yuko busy kutishia watu wanao pingana naye kielimu tu watu wakitaka kutoa matamko kwa kudai mamlaka hiyo ni yake tu lakini kikubwa kuliko yote, mtu ukiwa unashaka na elimu yako hujiamini basi unakuwa muoga kulinda kiti chako lakini kama elimu imejaa basi wala asingetafuta heshima kwa nguvu heshima ingemfuata tu. Mufti umekuwa muoga sana nini unaogopa? au unahisi wako watu nje huko wamekuzidi elimu kwa mbali sana. Mimi naamini kuwa Mufti ni lazima elimu yako iwe juu ya wengine hapo heshima itakuja tu automatic.