Mimi kwenye hili simuongelei Mufti tu na wala haijalishi ni Askofu, Shekh au hata rafiki tu nikiona mtu ana dalili za kishirikina na hasa za waziwazi kama hizi kujivisha mipete mizito napata ukakasi na huyu mtu, hata nyumbani kwangu simkaribishi. Dini imetukataza kabisa shirki sasa siwezi kuongozwa na mtu anayebeba taswira ya shirki.
lakini sababu sijui kazi ya mipete ile wanayovaa hawa viongozi wa dini ndio maana nimeuliza na kama haya mapete ni sehemu ya ibada zetu basi wangekuwa wanahubiri kutuomba na sisi tuvae kama yana faida kwao kwanini yasiwe na faida na kwetu sisi waumini wao. Kuna siri gani mle??