Shekh Zuberi Mufti wa Tanzania ni wazi anahitaji msaada

Shekh Zuberi Mufti wa Tanzania ni wazi anahitaji msaada

Huyu naye mleta amepuyanga mbona na wewe elim yako kama muft hivyo ulikuwa na haja gan kukimbilia kuleta mada hapaa ovyoo na kutuaminisha kuna bifu kumnee bure kbs na wewe
Wapi nimesema na elimu? Mimi sina elimu yoyote elimu yangu ni basic tu kama watu wengine. Nadhani nenda kaangalie timbwili huko youtube halafu uje hapa na mrejeo. Wewe unapigiwa simu saa saba usiku kesho asubuhi omba msamaha kabla ya swala ya Eid halafu unasema hakuna shida?
 
Najuwa hilo lakini mzee Mufti hilo hataki anasema yeye ndio mwenye mamlaka na yuko busy kila mara kugombania mamlaka. Ndio kila mara akiitwa sehemu basi anahitaji sana kuitwa kwa majina ya kutukuzwa sijui mheshimiwa mkuu na makorokoro mengi kutukuzwa. Lakini yote mimi ya hawa jamaa kuvaa mipete kama waganga wa kienyeji mpaka leo sielewi ya nini yale? na sio Mufti wengi 95%, je hawa wanaamini kweli Mungu au nyuma ya pazia washirikina.
Huwezi kutenganisha Uislamu na ushirikina vinaendana sambamba na pamoja.
 
Huwezi kutenganisha Uislamu na ushirikina vinaendana sambamba na pamoja.
Sasa mbona sisi waislamu na hapa naongelea mimi na pete moja tu kadogo cha ndoa yale ya kwao 100% ushirikina na mimi nakataa kuongozwa na mshirikina haijalishi una elimu kubwa kiasi gani mimi nakungalia wewe hapo mbele. Mipete ya rangi rangi mpaka mtu unatisha.
 
Leo kwa bahati nzuri nimepitia sehemu nikakuta kuna issue ya msikiti wa Mtoro wakimuoba msamaha Mufti, nikataka kuangalia nini kimetokea tarehe 29 ya Ramadhan.

Nikarudi kutafuta clip nikaipata kumbe kuna Shekh msikitini alisahihisha kauli ya kidini aliyotoa siku alipoenda kufunga darsa wanaita "Busati" , Mufti alisema siku ya shaka ni 29 Ramadhan kwa maana hujui mwezi umeandama au hapana lakini baada ya kuondoka Shekh wa msikiti akasema kwa heshima tu Mufti ulimi umeteleza kidini imeandikwa siku ya shaka ni 30 sio 29. Bwana jamaa wakapigiwa simu saa 7 usiku watu wameshalala kuwa lazima waombe radhi msikitini kabla swala ya Eid kuanza na wakafanya hivyo.

Kwa maoni yangu Mufti ni kweli aliteleza lakini namuona ni mtu fulani anapenda kutukuzwa sana na yuko busy kupigania kitu kinaitwa mamlaka hata mambo ya mwezi alitumia dakika 15 kulilia mamlaka ya kutangaza mwezi kuwa ni yeye tu, sasa shida yote hii ya nini? yuko busy kutishia watu wanao pingana naye kielimu tu watu wakitaka kutoa matamko kwa kudai mamlaka hiyo ni yake tu lakini kikubwa kuliko yote, mtu ukiwa unashaka na elimu yako hujiamini basi unakuwa muoga kulinda kiti chako lakini kama elimu imejaa basi wala asingetafuta heshima kwa nguvu heshima ingemfuata tu. Mufti umekuwa muoga sana nini unaogopa? au unahisi wako watu nje huko wamekuzidi elimu kwa mbali sana. Mimi naamini kuwa Mufti ni lazima elimu yako iwe juu ya wengine hapo heshima itakuja tu automatic.
Hivi mpaka leo kuna mbwa wanawafuatilia bakwata? Mbwa koko nyie
 
Hivi mpaka leo kuna mbwa wanawafuatilia bakwata? Mbwa koko nyie
Acha matusi wewe toa hoja kama unayo basi mambo ya Mbwa koko ya nini? Mimi sifuatilii Bakwata lakini sina sababu ya kuwatukana matusi mepesi kama hayo. Kitu unaona wazi wanafanya mbele yako kosoa lile unalo ona sio Mbwa Koko, siajabu kukawa na Baba yako au Mama yako anafuata Bakwata sasa sijui tusi ni hilo hilo au....
 
Mleta mada kwanz utawambia siku ya shaka ni nini ama siku gani kisha ndio tutapata ufumbuzi.
 
Naona siku hizi anatambulishwa kama Mufti Sheikh Dr Abubakar Bin Zubeir.,😁.

Hakuna asiyependa mamlaka.
 
Khaa, labda sijaelewa...lkn siku ya shake ni mwezi 29!! Au umekusudiaje?
Huyo mleta mada hata hajui kinachozungumzwa kasikia sikia tu, na yeye kaongeza yake Kaleta.

Siku ya Eid mtoro walitolea ufafanuzi kuhusu Darsa ya Ramadan 29 ambapo kulikua na mtu alipingana na Mufti kuhusu Siku ya shaka Mufti alisema 29 na huyo jamaa alisema 30 that's it, sio mtaalam wa kilichozungumzwa ila Mufti alipiga simu kwa mshauri wake na Imamu wa mtoro saa 7 usiku wakajadili na kesho yake (siku ya Eid) mshauri wa Mufti akaja kulitolea ufafanuzi,

Hayo mambo ya Mufti kulazimishwa kuomba msamaha, sijui mwandamo wa mwezi na maneno mengine aliosema mleta mada sijayasikia, source nilikuwepo msikiti wa mtoro swala ya Eid wakati mshauri wa Mufti anaelezea.
 
Bakwata wamefunga siku 29

Sunni wamefunga siku 30

Qur'an ni ile ile

Je siku ya Shaka ni ipi? Karibu [emoji209]

Siku ya shaka ni 29.

Ukitimiza 30 ni lazima ufungue kwa sababu hakuna Ramadan ya siku 31.

Sunni walianza kutazama mwezi siku ya J3 ambapo ilikuwa siku ya 29 kwao sababu waliwahi kuanza kufunga. Bakwata hawakuwa na uhalali wa kuanza kutafuta mwezi siku hiyo maana wao walikuwa wana siku 28 za Funga na hamna funga yenye siku 28( ni siku 29 au 30 ).

Sunni waliukosa mwezi siku hiyo ya J3 wakaamua kukamilisha siku 30 za Funga na J5 ikawa ni siku ya Eid kwa lazima kwao hata kama mwezi usingeandama. Bahati nzuri mwezi ukaandama Duniani kote na Bakwata wakawa hawana kipingamizi, wakati huo washatimiza siku 29 za Funga na wanaruhusiwa kufungua, ndipo walipofungua.
 
Iko siku nikiwa kwenye darasa zao nitainuka na kuwauliza mipete kazi yake ni nini? Mimi binafsi nikiona mtu na mipete mikubwa utasema hirizi hapo hapo namdharau tu. Pete ya ndoa tu vaa lakini mahirizi hapana.

😇

Naona unatafuta nongwa...

Mipete wanavaa hadi maaskofu wa Kikristo...
 
Ila wanachafua dini tunaonekana vituko tu sababu ya hawa watu. Kugombani mamlaka na mwezi basi ndio kazi yao. Narudia tena ile mipete mikubwa kazi zake ni nini? sio hawa wanaamini Allah pekee? au na majini pia.
Hakujazungumzwa lolote kuhusu mamlaka ya mwezi, are you sure una information sahihi mkuu?
 
Back
Top Bottom