Shelutete na Lema wang'olewa TANAPA

Shelutete na Lema wang'olewa TANAPA

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza ukomo wa utumishi wa maofisa wake wawili kwa sababu ambazo hazijawekwa bayana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma, watumishi hao ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema na kwamba utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania unaujulisha umma wa Watanzania na wadau wote wa uhifadhi na utalii kuwa waliokuwa watumishi waandamizi wa TANAPA, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema, utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Shirika halitahusika na jambo lolote watakalojihusisha nalo kwa niaba ya shirika,” inaeleza taarifa hiyo ambayo hata hivyo haijabainisha sababu za kukoma kwa utumishi wao.

Mwananchi lilimtafuta Ofisa Uhifadhi Mwandamizi wa Tanapa anayeshughulika na Mawasiliano, Catherine Mbena kujua sababu za kukoma kwa utumishi wa maofisa hao, hata hivyo hakuwa tayari kuzungumzia sababu hizo akidai kwamba shirika halijataka kuweka bayana.

“Tukiwa tunataka kufanya hivyo (kueleza sababu) tutawaambia, lakini for now (kwa sasa) tuna hilo tangazo tu,” amesema Mbena
3f61971eedbb4de087e3216b425e3401.jpg
 
Hii ndio wanaita kustaafishwa kwa manufaaa mapana ya ummaa au?
 
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza ukomo wa utumishi wa maofisa wake wawili ambao ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema kwa sababu ambazo hazijawekwa bayana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma, watumishi hao utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania unaujulisha umma wa Watanzania na wadau wote wa uhifadhi na utalii kuwa waliokuwa watumishi waandamizi wa TANAPA, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema, utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022,” inaeleza taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Shirika halitahusika na jambo lolote watakalojihusisha nalo kwa niaba ya shirika.
 
Huyu Kamanda Lema alikuwa Mkomazi au kuna mwingine ?.
 
"utumishi umekoma"au wamefukuzwa kazi kwa manufaa ya "umma"?
Kuna tetesi wali "whistle blow "ishu nzito,inayowagusa wakubwa,sasa wameshughurikiwa
Wamefukuzwa. Yaan lugha iliyotumika hapo ni ya kistaarabu.
Ila technicaly imeaisha hiyo
 
Sio kila lema ana uhusiano na lema wa chadema. Lema ni koo tu.
Kabla hujakurupuka faham source yao kwanza
Yani ndivyo walivyo wapuuzi wachache, wanashindwa kuelewa hizo ni koo tu na nchi ni yetu sote. Yani kuitwa lema ndo tayari ana udugu na lema wa chadema?? Kwani ndugu wa Lema hafai kuitumikia nchi?? Yaan tabu
 
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza ukomo wa utumishi wa maofisa wake wawili kwa sababu ambazo hazijawekwa bayana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma, watumishi hao ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema na kwamba utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania unaujulisha umma wa Watanzania na wadau wote wa uhifadhi na utalii kuwa waliokuwa watumishi waandamizi wa TANAPA, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema, utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Shirika halitahusika na jambo lolote watakalojihusisha nalo kwa niaba ya shirika,” inaeleza taarifa hiyo ambayo hata hivyo haijabainisha sababu za kukoma kwa utumishi wao.

Mwananchi lilimtafuta Ofisa Uhifadhi Mwandamizi wa Tanapa anayeshughulika na Mawasiliano, Catherine Mbena kujua sababu za kukoma kwa utumishi wa maofisa hao, hata hivyo hakuwa tayari kuzungumzia sababu hizo akidai kwamba shirika halijataka kuweka bayana.

“Tukiwa tunataka kufanya hivyo (kueleza sababu) tutawaambia, lakini for now (kwa sasa) tuna hilo tangazo tu,” amesema Mbena
Huyo shelutete ni fisadi mkubwa ni sawa alivyoondolewa
 
Hawa walizuia kuruhusu vibali vya kusafirisha wanyama uarabuni.Nimeamini ukiwa mwema kwenye hii serikali utaishia kufukuzwa.Sisi wana Tanapa tumeumizwa sana na wazalendo wenzetu kufukuzwa
Híi ndo sababu pekee nayoweza amini,,
Wale watu wamerudi Kwa Kasi ya 6G,,[emoji134]
 
Back
Top Bottom