Shelutete na Lema wang'olewa TANAPA

Shelutete na Lema wang'olewa TANAPA

Huyo shelutete ni fisadi mkubwa ni sawa alivyoondolewa
Haiingii akilini hii
Ingekua ndo sababu S/Kali ingesema kujisifia upgaj kazi wake

Ila hapa itakua Wameziba Wale kina Somalia Wamerudi kazini kuchukua vyao
 
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza ukomo wa utumishi wa maofisa wake wawili kwa sababu ambazo hazijawekwa bayana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma, watumishi hao ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema na kwamba utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania unaujulisha umma wa Watanzania na wadau wote wa uhifadhi na utalii kuwa waliokuwa watumishi waandamizi wa TANAPA, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema, utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Shirika halitahusika na jambo lolote watakalojihusisha nalo kwa niaba ya shirika,” inaeleza taarifa hiyo ambayo hata hivyo haijabainisha sababu za kukoma kwa utumishi wao.

Mwananchi lilimtafuta Ofisa Uhifadhi Mwandamizi wa Tanapa anayeshughulika na Mawasiliano, Catherine Mbena kujua sababu za kukoma kwa utumishi wa maofisa hao, hata hivyo hakuwa tayari kuzungumzia sababu hizo akidai kwamba shirika halijataka kuweka bayana.

“Tukiwa tunataka kufanya hivyo (kueleza sababu) tutawaambia, lakini for now (kwa sasa) tuna hilo tangazo tu,” amesema Mbena
Mleta tarifa umeingia mitini

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 

Attachments

  • FC2DAA6F-6A46-405D-A163-437E98FAEAF1.jpeg
    FC2DAA6F-6A46-405D-A163-437E98FAEAF1.jpeg
    48.8 KB · Views: 11
Hukawii kusikia wamainglia wa nyama kinyume cha maumbe na bila hiari
 
Lete Maneno.....
Kuna hotel moja huko kilimanjsro , moshi mjini alikuwa anakwenda kuchukua invoice za madai ya mikutano, kulala na ukumbi . Bila hata kuwepo kwa mikutano ili akuchukue fedha Tanapa
 
Kuna hotel moja huko kilimanjsro , moshi mjini alikuwa anakwenda kuchukua invoice za madai ya mikutano, kulala na ukumbi . Bila hata kuwepo kwa mikutano ili akuchukue fedha Tanapa
Ndugu Zangu Majizi Yapo Hata Ccm

Alikuwa Ananenepesha Ng'ombe Siku Ya Mnada Sasa Ameharisha Hauziki
 
Ila adhabu za vigogo raha sana, unapigwa chini kazi lakini hawachukui hata senti yako wala kukufunga, ila nesi angeiba panado hospitali shughuli yake angeiona aisee
 
Back
Top Bottom