Shelutete na Lema wang'olewa TANAPA

Shelutete na Lema wang'olewa TANAPA

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza ukomo wa utumishi wa maofisa wake wawili kwa sababu ambazo hazijawekwa bayana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma, watumishi hao ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema na kwamba utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania unaujulisha umma wa Watanzania na wadau wote wa uhifadhi na utalii kuwa waliokuwa watumishi waandamizi wa TANAPA, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema, utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Shirika halitahusika na jambo lolote watakalojihusisha nalo kwa niaba ya shirika,” inaeleza taarifa hiyo ambayo hata hivyo haijabainisha sababu za kukoma kwa utumishi wao.

Mwananchi lilimtafuta Ofisa Uhifadhi Mwandamizi wa Tanapa anayeshughulika na Mawasiliano, Catherine Mbena kujua sababu za kukoma kwa utumishi wa maofisa hao, hata hivyo hakuwa tayari kuzungumzia sababu hizo akidai kwamba shirika halijataka kuweka bayana.

“Tukiwa tunataka kufanya hivyo (kueleza sababu) tutawaambia, lakini for now (kwa sasa) tuna hilo tangazo tu,” amesema Mbena
View attachment 2367706
LEMA NI MKAGUZI WA NDANI NA SHELUTETE NI CORPORATE PERSON.....NINAJUA WATU WANAJISAFISHA LAKINI KWA HILI WATAJICHAFUA .....NGOJA TUONE
 
Ajabu sababu ya kuondolewa kwao inafichwa.
Jamani hii issue ni magumashi matupu na kuna watu hapa wamebambikizwa ile wanasema funika kombe mwanaharamu apite, kwanza ni waambie tu mmoja hapa ni lema ambaye ni mkaguzi wa ndani mahiri sana, kwenye hili mwakilema alishauriwa na wabaya wake lema amwondoe ili maisha yawe mazuri mie niko ndani sana ya taasisi na nilijaribu kuelezea toka mwanzo hili walau mamlaka za juu zaidi ziweze kuingilia, lakini sasa naona watu wema wanadhulumiwa bila sababu.

Kuna siku nitaweka mwenendo wa kesi nzima na cooked evidence zao mtashangaa ila ngoja tusubiri kwanza. Kuna watu wamestaafu hapa na wako kwa mikataba(CIA, director of finance na chief engineer) wananunua mahotel kwa hela za kuchukua ofisini wanaogopa kuwa huyu mkaguzi atakuwa threat kwao in their absence.

Mimi niombe tu Mhe. Rais, VP au PM waingilie ili swala wamuite lema awafungukie mambo otherwise good people wanaumizwa sana hapa TANAPA. Naawambia this guy is good unbelievable.

Jiulize kwanini TANAPA HAWAWEKI WAZI KISA CHA KUWAONDOA? Na wanatumia polisi, takukuru na vyombo vingine kumtisha, hakika hiki ni kilio kwa watu wote wema nchi hii. Kwa heshima na tahadhima Mhe. Rais, VP au PM tumieni uwezo wenu kutoa haki hapa. Na issue yenyewe imeanzia hapa
 
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza ukomo wa utumishi wa maofisa wake wawili kwa sababu ambazo hazijawekwa bayana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma, watumishi hao ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema na kwamba utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania unaujulisha umma wa Watanzania na wadau wote wa uhifadhi na utalii kuwa waliokuwa watumishi waandamizi wa TANAPA, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Shelutete na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Lema, utumishi wao umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Shirika halitahusika na jambo lolote watakalojihusisha nalo kwa niaba ya shirika,” inaeleza taarifa hiyo ambayo hata hivyo haijabainisha sababu za kukoma kwa utumishi wao.

Mwananchi lilimtafuta Ofisa Uhifadhi Mwandamizi wa Tanapa anayeshughulika na Mawasiliano, Catherine Mbena kujua sababu za kukoma kwa utumishi wa maofisa hao, hata hivyo hakuwa tayari kuzungumzia sababu hizo akidai kwamba shirika halijataka kuweka bayana.

“Tukiwa tunataka kufanya hivyo (kueleza sababu) tutawaambia, lakini for now (kwa sasa) tuna hilo tangazo tu,” amesema Mbena
View attachment 2367706
someni hii kitu mfanye uchambuzi vizuri
https://www.jamiiforums.com/threads/public-funds-are-stolen-from-million-to-single-digit-billion-currently.1961194/

https://www.jamiiforums.com/threads/je-ni-sahihi-kwa-watumishi-wa-umma-waliofikisha-umri-wa-kustaafu-kuongezewa-mkataba.1950009/page-4#post-41757611

https://www.jamiiforums.com/threads/dear-controller-and-auditor-general-cag-take-note-on-this.1965530/
 
Walihujumu nini?? Mbona Paschal alikuwa mahiri kuipigania serkali na chama tawala?? Paschal alianza lini usaliti?? Am shocked
Labda walivurugana kwenye ule ugawaji wa campsites! Kinachoendelea mle TANAPA ni balaa tu!
 
Back
Top Bottom