Kuna tajiri mmoja aliandika Wosia wake Mwaka juzi alifanya siri hakumshirikisha Mke wake wa Ndoa, kwa bahati mbaya alifariki Mwaka huu, baada ya maziko aliyekuwa shahidi kwenye Wosia akaijulisha familia kuwa kuna Wosia Marehemu alikuwa ameandika na akawajulisha sehemu Wosia ulipo akawaomba watakapokuwa tayari kwa ajili ya kusomewa Wosia wamjulishe. Huyo Tajiri alikuwa na Watoto wengi nje ya Ndoa, kwenye Ndoa alikuwa na Watoto Wawili, walipopata nafasi walimjulisha Shahidi wakasomewa Wosia, Mali zote alizokuwa nazo Marehemu alipewa Mke wa Ndoa na Watoto wake wengine hawakupewa chochote na sababu ya kutokupewa chochote aliandika hawakumjali wakati wa ugonjwa wake, Watoto wenyewe wengi wao walikuwa wanategemea mali za Baba yao, Mtoto mmoja kati ya ambao hawakupewa chochote alikwenda mahakamani kuweka pingamizi kuwa hakubaliani na Wosia, Kesi inaendelea mahakamani, kwa Wanasheria hili jambo muafaka wake utakuwaje?
Ni vizuri tujifunze kutafuta vya kwetu bila kusubiria mali zilizotafutwa na Mtu mwingine.