Shemeji yangu amegushi muhtasari wa ukoo wa mirathi

Shemeji yangu amegushi muhtasari wa ukoo wa mirathi

Sikiliza kaka nikupe elimu ya kisheria. Usidhani hao wa Asia au wazungu hawana msimamizi wa mirathi. Ushawahi kusikia THE HEIR OF A FAMILY? Huyo ndio msimamizi wa mali zote na msemaji mkuu. Narudi kwetu, ufinyu wa uwelewa kutokana na mapungufu ya lugha yetu ya kiswahili ndio unaokufanya uishie kufikiria hivyo. Kiufupi; KAZI KUBWA YA MSIMAMIZI WA MIRATHI ni kukusanya na kuzitambua mali za marehemu. SIO LAZIMA AZIGAWANYE KWA WAHUSIKA BALI CHOCHOTE KINACHOHUSU HIZO MALI YEYE NDIYE MUONGOZAJI NA MSEMAJI MKUU. Kwetu huku kutoka na uchumi mbovu na kipato haba akichaguliwa msimamizi wa mirathi mnataka mfikie hatua ya baada ya utambuzi wa mali bhasi kama muongozaji mkuu azigawe ili kusiwe na manung'uniko kati ya wanafamilia.
Kama hujaelewa hapo sijui nikusaidiaje mkuu
Njaa zetu ndio zinazotupa mlolongo usio na tija. Hapa mrithi ni nani aliyepitishwa na mahakama?
abandoned.jpg
 
Wakuu kwema huko wale town na wale wa bush mko sawa wapambanaji...wahaini, magaidi wa serikali mpo pia...🤔
Wakuu ndugu yangu alifariki baada ya maziko ukoo ulikaa kikao cha kujadili mali za marehemu na kuteua msimamizi wa mirathi. Tuliamua kwa kauli 1 kwamba mke wa marehemu ndo awe msimamizi wa mirathi na mali zingine zote tulimkabidhi yeye na hakuna aliyechukua hata kikombe cha marehemu.

Marehemu aliacha watoto wawili. Sasa tuliandika muhtasari wa ukoo wa uteuzi wa msimamizi wa mirathi na tukamkabidhi mke wa marehemu aendelee na taratibu alipofika mahakamani akaambiwa muhtasari huo ufanyiwe baadhi ya marekebisho aurudishe kwenye ukoo afanyiwe marekebisho hayo.

Yeye sjui alikaa na akina nani wakajiandikia muhtasari wakapachika majina ya mwenyekiti na katibu wake walewale wa uko na kusaini saini zao za kughushi kisha akarejesha mahamakani. Sasa alipokwama ni mahakama kumwambia waje mashahidi wawili wa ukoo kuja kuthibitisha muhtasari huo.

Alipolileta hilo ndo hapo katibu akamuomba huo muhtasari aliopeleka mahakamani ndo akatuma muhtasari tofauti wenye sahihi bandia na umefanyiwa marekebisho mvutano ukaanza hapo sasa kwanini kaandika muhtasari mwingine ambao ukoo hauujui na kwann kafoji sahihi za watu.

Siku kesi ilipotajwa ili ndugu wawili wakathibitishe niliagizwa nikashughulikie ikiwemo kuandika barua ya pingamizi kwamba muhtasari huo ulioko mahakamani hautambuliki na ukoo kwani kuna sahihi za watu wa familia zimefojiwa na muhtasari huo ni fake, pia kuna vipengele vimeondolewa bila taarifa kwa ukoo.

Sasa nimelifikisha hilo japo ni kama hakimu alitaka kunibabaisha fulani kwamba muhtasari huo hata usipokuwepo mahakama inaweza kuteua msimamizi wa mirathi mi nikamwambia hakimu kama ndivyo wanikabidhi huo muhtasari niondoke nao leo niupeleke kwenye ukoo kwamba mahakama imesema muhtasari hauhitajiki tena wao watateua msimamizi bila muhtasari 😀

Hakimu akanywea kidogo akasema basi uamuzi ni kwamba muhtasari urudi kwa ukoo wamsaidie msimamizi kufanya marekebisho na urudishwe mahakamani au isipofanyika hivyo basi kesi hii ya msimamizi wa mirathi itafutwa na itafunguliwa kesi nyingine ya pingamizi 😀

Mi nikwambia hakimu we mkabidhi huo muhtasari mhusika arudi kwenye ukoo wamsaidie sasa shida anarudi vipi huko wakati ameshagombana na raia wengi akiwemo katibu aliyeandika muhutasari ngoma nzito.

Lakini pia asiposaidiwa hilo kesi inafutwa na inafunguliwa ya pingamizi sasa huko ndo kutakuwa na shughuli kwani mhusika amedanganya mahakama kwa kughushi muhtasari na sahihi ya mwenyekiti na katibu wake 😀

Je wakuu mnanishauri nn mpaka hapo hasa kesi ikifunguliwa ya pingamizi kulingana na barua niliyoandika na kile amefanya shemeji yangu?
Pili je anaonewa? 🤔​
Kama shemeji yko ni mrembo na hakimu ni mwanaume hesabu huna chako..

Yalinikuta mimi ,,nikaambiwa usishindane na mwanamke..
Nikakubali yaishe..
 
Sidhan kama una akili timamu na unawaza yaliyo potofu sn ndo maana umesoma hata hujaelewa kitu umekurupuka tu na mambo ya mali sjui ni ***** ww
Wewe mwenye akili timamu umevumbua nini, zaidi ya kungojea huruma ya kuajiriwa?
Pima IQ yako, kichwa chako kina mashina mangapi ya nywele?
 
Alipozingua ni kugushi sign kama alipewa ushirikiano chanya kwanini alienda kugushi taarifa?
 
Kesi kama hii imewai tokea kweye ukoo wangu mwaka 2013
Baada ya baba mkubwa kufariki ukoo ulikubaliana mali za marehemu zibakie na mama(mke)pamoja na watoto wake
Akateuliwa mtu mmjo wa kuwasikiliza kama watakuwa na ishu yaani ni kama muangalizi wa ile familia
Baada ya kama miaka 2 hivi hakuna mali yeyote ilibakia yaani mwanamkea kauza kila kitu mpaka nyumba na hata pesa hazijulikan kapeleka wapi watoto kashindwa kulea ikabidi wazee wamuite ili wamuulize nini kimemkuta
Hakuja aliagiza tu watoto na yeye mpaka leo sijuagi alienda wapi na anaishije huko
nilijifunza kutoka ile day japokuwa nilikuwa mdogo kama miaka 13.
 
Kesi kama hii imewai tokea kweye ukoo wangu mwaka 2013
Baada ya baba mkubwa kufariki ukoo ulikubaliana mali za marehemu zibakie na mama(mke)pamoja na watoto wake
Akateuliwa mtu mmjo wa kuwasikiliza kama watakuwa na ishu yaani ni kama muangalizi wa ile familia
Baada ya kama miaka 2 hivi hakuna mali yeyote ilibakia yaani mwanamkea kauza kila kitu mpaka nyumba na hata pesa hazijulikan kapeleka wapi watoto kashindwa kulea ikabidi wazee wamuite ili wamuulize nini kimemkuta
Hakuja aliagiza tu watoto na yeye mpaka leo sijuagi alienda wapi na anaishije huko
nilijifunza kutoka ile day japokuwa nilikuwa mdogo kama miaka 13.
Sa huyu naye mali zote nje ya mirathi kakabiziwa zote na ameanZa kuuza baadhi ya vitu kwa madai kwamba ye anarudi kuishi tu kwao huko...hakuna anayetaka mirathi hiyo ila watu wamekataa ushenzi aliofanya tu
 
Back
Top Bottom