Shemeji yangu amekataa! Abadani, Mwanangu hapimwi DNA ikibidi ndoa ivunjike tu

Shemeji yangu amekataa! Abadani, Mwanangu hapimwi DNA ikibidi ndoa ivunjike tu

Mkuu hujachelewa, nakuhakikishia, ukiona mwanamke anakufanyia yasiyofaa ,ni wewe umeamua akufanyie hayo.

Kua kimya Kwa mwanamke, mwisho wake ni kukuona Boya.

Sio ukimya tunachotaka hapa ni mwanaume kuna sehemu zako unatakiwa uonyeshe uwanaume lakini sio kila sehemu unaleta uwanaume wakati busara ndio zinatakiwa kaka
 
Wewe na huyo bro wako ni kama matahila tu. Wanawake wa kisasa watakubali kuumbuka kizembe hivyo? Kwanini asingemchukua mtoto kimya kimya akaenda nae kupima mpaka aombe ruhusa kwa mkewe. Mkome.
 
Hii inawezekana kwasababu vinasaba vinaenda way back vizazi vingi sana.

[emoji28][emoji28][emoji28] Hii ni ukiona Manyoya ujue tayari- partenity test lazima iombwe ustawi wa jamii au mahakamani siyo jambo la kuzoana tu.

Na process zake ni ndefu sio za siku mbili
 
Peleka kenya haina haja ya mahakama hata online unapima, ukilipia unapewa namna ya kutuma sample, then majibu wanakutumia online utapambana na stress mwenyewe
 
Mlishindwa nini kufanya bila kumshirikisha mama, issue tu ngoja nikapunge upepo na kids huku umempanga doctor kimya kimya
 
Wakuu tumefika mwisho. Tumekuwa watabe kushauri kwenye mahusiano ya wengine huku mtandaoni lakini huku field Mke wa Brother(rafiki yangu wa longtime) ametushinda.

Ni hivi Mwaka Jana Mke wa Huyu Best Yangu alijifungua mtoto wa kiume. Tulifurahi kupata mtoto wapili na sisi kama ndugu na jamaa wa karibu sana ukizingatia yeye jamaa alinisaidi sana kusoma enzi hizo kipesa na kimawazo basi tulimfanyia Tafrija ndogo ya kupata mtoto.

Siku chache baadae furaha ya jamaa iliingia shubiri kila alipokuwa akifatilia ukuaji wa mtoto.

Yaani mtoto amekuwa na sura na mwonekano tofauti na Baba na Mama yake.

Yaani Mshikaji ni Mweusi na Mke wake maji ya kunde lakini Mtoto ni Mweupe.

Kwa sayansi ndogo tuliyo nayo kama baba mweusi na Mama maji ya kunde sio rahisi kupata mtoto mweupe. Pengine angepata rangi ya kunde kama Mama yake au Mweusi kabisa kama Baba yake.

lakini Baba ni msomi hawezi kufanya maamuzu based on just feelings. Ameamua kushauriana na mkewe kuwa wakampime DNSA maana jamaa roho inakataa kumpenda mwanaye kati kati ya mashaka.

Mke amekataa kata kata kuwa Mwanaye hapimwi DNA ikibidi hata ndoa ivunjike.

Ana dai kama hamwamini mke wake basi bora waaachane.

Mimi na Braza tume baki mdomo wazi juu ya msimamo wa Mwanamama huyu.

Tulitegemea angekubali ili kumwondolea hofu mumewe na upendo uzidi kutamalaki. Hali imekuwa tofauti.
Huyo ndugu yako kabla ya kupima DNA na mtoto aanze kujipima mwenyewe kama ana uwezo wa kutungisha mimba, msimchefue Mama wawatu, huenda kafichiwa aibu yeye anaanza kuleta kidomo domo, huyo Mama kamfanya aitwe mwanaume [emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom