EL ELYON
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 1,565
- 1,918
Wakuu mmebarikiwa Sana na Mwenyezi Mungu mliofunga Mungu Awakumbuke Sana.....
Nipo mkoa Fulani kikazi mbali kabisa na familia yangu. Huku kwa bahati nzuri kuna ndugu yangu kabisa ni askari.
Nilipofika nilifikia kwake kama siku tatu hivi nikawa nimehamia kwenye nyumba niliyokuwa nimeandaliwa na ofisi.
Nilifurahi Sana kukutana na ndugu yangu kwani tumekua wote tumesoma wote na hata alipoondoka kwenda depo alitokea kwangu yaani nilikuwa naishi naye kabla hata sijaoa.
Sa imekuwa kawaida nikitoka kazini yeye jioni hunitafuta au Mimi humtafuta tunatoka kidogo kisha usiku by saa mbili mi huwa tayari nmerudi kwangu lakini ndugu yangu huwa mara zote namuacha huko mtaani na jamaa zake sjui huwa anarudi kwake saa ngapi.
Nilianza kuhisi ni kama shemeji yangu mke wa ndugu yangu anahisi mume wake anapochelewa kurudi anadhani huwa Niko naye wakati si kweli akiamini mi ndo namchelewesha nilihisi Hilo mapema sana ila nikapotezea tu.
Sasa imeibuka tabia ambayo ni mpya ndugu yangu siku zingine huwa ananipigia simu nipite kwake kumpitia lakini kuna kitu nakiona ni kama mke wa ndugu yangu anajaribu kushindanisha ni Nani mwenye nguvu kwa mume wake je ni yeye mke au Mimi ndugu kwani wakati mwingine naweza nikawa nimekaa namsubiri ndugu yangu tutoke unashangaa mkewe anaongelea dirishani akiwa nje WE BABA FULANI USTOKE.....🤔 Mi kama kawa sjari kabisa hata ila huwa nashangaa tu.
Na kinachonishangaza mara nyingi nikiwa pale ndo utashangaa anamuomba mumewe hela hadharani kuna siku alimuomba hela mumewe akamwambia sina weeee dada aliwaka OOOH MBONA WENGINE WAKIKUOMBA UNAWAPA...🤔 nilishtuka Sana Ile kauli maana ni kama alikuwa ananilenga Mimi as if mi huwa namuomba hela mumewe wakati mumewe ndo huwa namtoa sana.
Kingine akiona nimeshika simu ya mumewe weeee huo mdomo utakavyovutwa nadhan mnaelewa wanaume ukiwa na mshikaji wako kushika simu yake ni kawaida sana.
Nilichogundua Yule shemeji yangu anaona kama ndugu yangu Yuko vizuri Sana na Mimi story kucheka Sana sasa ni kama hiyo Hali inamuumiza Sana kwamba kwanini mumewe hacheki naye Sana wala kupiga naye Sana story kama anavyokuwa na Mimi.
Anatumia nguvu nyingi kutaka kuonyesha ye ana nguvu kwa mumewe kuliko Mimi ndugu wa mumewe.
Cha ajabu pale kwake hata maji tu huu mwaka toka umeanza sjanywa hata maji kwake chakula ndo kabisa hata nikute wanakula sili tarudi kwangu takula niliamua hivyo maana wanawake bwana hivi ni vitu vidogo Sana lakini kwao ni vikubwa nadhani wenye uzoefu mnanielewa yaani mkeo anaweza akamnyanyasa Sana ndugu yako kisa ugari tu japo si wote.
SASA WAKUU HIVI NI KWANINI WANAWAKE WAKE ZA WATU HUWA WANALAZIMISHA WAWE NA NGUVU KWA WAUME ZAO KULIKO NDUGU WA MUME WAKATI HIZO NI NAFASI MBILI TOFAUTI MAANA MI SIWEZI KUWA MKE WA NDUGU YANGU WALA MKE WA NDUGU YANGU HAWEZI CHUKUA NAFASI YA UNDUGU WANGU KWA MUMEWE. ndoa huvunjika ila udugu ni wa milele wanawake Wana shida gani kwenye hili?
Mpka nilikuwa nawaza ingetokea mi nimekuja huku may be sina ramani naishi hapo kwake uwenda ndo ningejua kwanini Putin Hana picha akiwa anacheka...
KARIBUNI kwa maoni wenye uzoefu wa haya mambo.....