Shemeji yangu ni mchafu sana. Jana nilimtembelea akanialika chakula nikatapika mbele ya familia

Shemeji yangu ni mchafu sana. Jana nilimtembelea akanialika chakula nikatapika mbele ya familia

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Huyu mke wa mshikaji wangu anashika rekodi ya uchafu.

Nilishindwa kuwatembelea Jumapili ya Pasaka nikasema niende jana Jumatatu ya Pasaka. Wana mtoto mchanga na wanafuga bata, wakati wa naandalizi ya msosi kwa macho yangu niliona akimtawaza mtoto bila kunawa mikono, mara akajikuna sehemu za siri akaenda kukata kachumbari.

Hatujakaa sawa, bata wake akadokoa mboga kwenye sufuria, lakini kiumbe huyu wala hakujali, like nothing happened. Wakati wa msosi ulipofika nikakumbuka hayo matukio nikajikuta natapika, nikasingizia Malaria.

Wanaume wa kwenye ndoa mnavumilia mengi sana.
 
Huwezi Kumtenganisha bata na uchafu

So sad na Shem wako kaunga tela!

Plus heka heka za kulea

Utafanyaje sasa msamehe bure tu..
Kuna watu wana raha hawana kinyaa kabisa
 
Jinsia Yako tafadhari, yaani unatapika kisa Bata! Watu ugali anakula mbwa tunamfukuza tunaliendeleza alipoishia. Hivi unaweza Kula ugali na sondo(ng'oni ng'oni/ funza wa kwenye miti) wewe?
 
Kuna sehemu nilialikwaga sikukuu, kufika pale Yule dada kanunanuna, alikuwa anatematema mate, alikuwa na maralia, nimekaa nikaongea kamwita mtoto anipakulie chakula nikakataa nimeshiba, nikawaambia nimekuja kuwasalimia tu, kwani hata wewe ungejifanya nimekuja kuwasalimia tu ungekataa kula Basi.
 
Huo ndio uungwana sasa
 
Huyu mke wa mshikaji wangu anashika rekodi ya uchafu.

Nilishindwa kuwatembelea jumapili ya pasaka nikasema niende jana jumatatu ya pasaka,wanamtoto mchanga na wanafuga bata,wakati wa naandalizi...
Hiyo familia wote wachafu nakwambia sasa
 
Jinsia Yako tafadhari, yaani unatapika kisa Bata! Watu ugali anakula mbwa tunamfukuza tunaliendeleza alipoishia. Hivi unaweza Kula ugali na sondo(ng'oni ng'oni/ funza wa kwenye miti) wewe?

Although naweza pia but sio picha nzuri kabisa. Hiyo ni dalili ya mtu asie jali usafi
 
Na kwa hawa mama wa lishe...

Niliwahi ona amemaliza kujisaidia haja kubwa/ndogo!!...akaja kutengeneza kachumbali bila kunawa mikono...
 
Back
Top Bottom