Shemeji zako wa kiume wakija kukutembelea, siku hiyo usilale na dada yao (Mke Wako). Kalale nao chumba kimoja

Hili suala linategemea ntu na ntu ...haiwezekani nishindwe kulala na wife kiss mashemeji.
 
Huo ni uoga wa kifala

Ukishaoa wewe ni taasisi inajitegemea kabisa,kimsingi hao mashemeji ndio wapo kwako kimakosa halafu uanze kuwatreat kama wafalme,watakua wanarudi kila wikend hapo halafu kwenye kupiga na hizo story ndio watajua na madhaifu yako na hawatakua serious kabisa kuhusu wewe.

Unatakiwa kuwa shemeji fulani kauzu sana mtu wa mipango,mtu adimu kuonekana kama kakakuona...unarudi usiku sana unaondoka hawajaamka na mambo yao yote unasikia toka kwa dada yao,kama hela usiwanyime...acha kwa dada yao,outing ni moja tu baada ya kujua ratiba yao,may be siku ya mwisho kesho wanaondoka ndio tokeni nao tena na mke wako(dada yao),piga speech moja ambayo siyo ya kujadiliana na usiruhusu wakuzoee zoee kifala.

Yaani mimi nilale na shemeji zangu?!...ebooooo

Labda msibani huko na kwenye dharura.

Jamaa kama unafanya hivyo sahau kuheshimika ukweni
 
Mambo vp jamiiforums.

Ninaomba kuanza kwa kutangua kusema maneno haya machungu ambayo yatawauma wanaume wengi sana. Hata mimi nilikuwa hivi hivi. Mwanaume wengi sana huwa hawawapendi shemeji zao wa kiume siku za mwanzoni.

Just imagine, kwa akili ile ya kitoto unajua kabisa huyu ndio anataka kumchukua dada yangu aende naye kwake awe analala naye siku zote for the rest of their lives. Huwaga kunakuwa na hali fulani hivi ya wivu kwa siku za kwanza ile baadae unaona kawaida tu na maisha yanaendelea.

Kuna watu watakuwa wanajiuliza wivu huu unatokea wapi wakati huyu ni kaka na dada yake na kamwe hawawezi kuoana. Wakaka wengi wanakuwaga na wivu na dada zao na mara nyingi jaribu kuangali watoto wakubwa wa kiume wanavyowachapa wadogo zao wa kike.

Huwa wanawachapa pindi wakisikia wadogo zao wapo katika uhusiano na vijana fulani wa mtaani hapo ambao ni washkaji zao wanaokaa wote vijiweni au siku dada mdogo amechelewa kurudi nyumbani bila maelezo ya kutosha. Hiyo ni aina ya wivu wa asili ambao wanaume wengi huwa nao dhidi ya ndugu zao wa kike wakiwa katika uchumba na shemeji zao.

BACK TO THE TOPIC
=====
Ewe kijana ambaye bado haujaoa mpaka sasa, siku utakapooa, shemeji zako wa kiume wakija kukutembelea, siku hiyo usilale na dada yao. Kalale nao chumba kimoja mpige story mpaka asubuhi.

Kama wao ni watu wa tungi kama wewe, siku hiyo nunua beer, choma nyama, kunyweni mlewe, msikilize mziki. Kama ni watu wa mpira, wachukue uende nao sehemu wanayoonesha mpira tofauti na hapo kwako.

Nenda nao hata huukoooo city center Kariakoo/Posta, angalieni mpira kula nao nyama choma, inelata raha na heshima sana. Unajua, unapoona katika familia fulani, wewe unakuwa ni sehemu ya familia ile. Hivi wewe kijana unalijua hili?

Kama mama mkwe wako ana watoto 3 wa kiume, basi wewe kama shemeji wa familia ile unakuwa mtoto wake wa 4. Kwa hiyo wale shemeji zako wa kiume wanakuwa brothers to you.

Wanakuwa brothers alafu washkaji zako, tena kama umri unalingana ndio raha zaidi kwa maana hata stories pamoja na interests zinaweza kufanana kwa sehemu kubwa.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Watu wa umri wetu hatujawahi kuona baba zetu wakienda kwa shangazi zetu kulala ni taboo, mwiko,fedheha n uchuro. Mwanaume kwenda mji wa mwanaume mwenzako usiku dadako anashughulikiwa unasikia miguno na vilio!
 
Hii ndio sababu kwenda kukaa kwa shemeji ni ngumu😂😂😂

Mashemeji huwa wanaangalia familia na familia au tuseme ukoo kiujumla. Ukiona shemeji ana ngebe sana bhasi ukoo au familia aliyoingia inamtegemea ila akiingia kwenye ukoo ambao awepo au asiwepo watu wanaona sawa tu. Hata akienda kusalimia ukweni anaingia kwa adabu zote na mashemeji wakifika kwake wanaishia kusalimia tu na kulala pengine. Hapo hayo mawazo ya kipuuzi hawezi kuwa nayo
 
.Dogo....unatoa ushauri hata mahari hujawahi kutoa. Ndio kwanza bado u-msimbe
 
Mambo vp jamiiforums.

Ninaomba kuanza kwa kutangua kusema maneno haya machungu ambayo yatawauma wanaume wengi sana. Hata mimi nilikuwa hivi hivi. Mwanaume wengi sana huwa hawawapendi shemeji zao wa kiume siku za mwanzoni.

Just imagine, kwa akili ile ya kitoto unajua kabisa huyu ndio anataka kumchukua dada yangu aende naye kwake awe analala naye siku zote for the rest of their lives. Huwaga kunakuwa na hali fulani hivi ya wivu kwa siku za kwanza ile baadae unaona kawaida tu na maisha yanaendelea.

Kuna watu watakuwa wanajiuliza wivu huu unatokea wapi wakati huyu ni kaka na dada yake na kamwe hawawezi kuoana. Wakaka wengi wanakuwaga na wivu na dada zao na mara nyingi jaribu kuangali watoto wakubwa wa kiume wanavyowachapa wadogo zao wa kike.

Huwa wanawachapa pindi wakisikia wadogo zao wapo katika uhusiano na vijana fulani wa mtaani hapo ambao ni washkaji zao wanaokaa wote vijiweni au siku dada mdogo amechelewa kurudi nyumbani bila maelezo ya kutosha. Hiyo ni aina ya wivu wa asili ambao wanaume wengi huwa nao dhidi ya ndugu zao wa kike wakiwa katika uchumba na shemeji zao.

BACK TO THE TOPIC
=====
Ewe kijana ambaye bado haujaoa mpaka sasa, siku utakapooa, shemeji zako wa kiume wakija kukutembelea, siku hiyo usilale na dada yao. Kalale nao chumba kimoja mpige story mpaka asubuhi.

Kama wao ni watu wa tungi kama wewe, siku hiyo nunua beer, choma nyama, kunyweni mlewe, msikilize mziki. Kama ni watu wa mpira, wachukue uende nao sehemu wanayoonesha mpira tofauti na hapo kwako.

Nenda nao hata huukoooo city center Kariakoo/Posta, angalieni mpira kula nao nyama choma, inelata raha na heshima sana. Unajua, unapoona katika familia fulani, wewe unakuwa ni sehemu ya familia ile. Hivi wewe kijana unalijua hili?

Kama mama mkwe wako ana watoto 3 wa kiume, basi wewe kama shemeji wa familia ile unakuwa mtoto wake wa 4. Kwa hiyo wale shemeji zako wa kiume wanakuwa brothers to you.

Wanakuwa brothers alafu washkaji zako, tena kama umri unalingana ndio raha zaidi kwa maana hata stories pamoja na interests zinaweza kufanana kwa sehemu kubwa.

Hata kama wamekuja kukaa kwa siku 5 tu, basi tenga siku moja ya kwanza kwa ajili yao.

Keep them close as if they are your siblings, na kumbuka kutokulala chumba kimoja na dada yao siku hiyo sio kwa sababu ya aibu bali inajenga "decency" na heshima ya aina fulani dogo lakini yenye maana sana.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Vaa barakoa
 
Back
Top Bottom