Political Jurist
Senior Member
- Sep 6, 2021
- 143
- 120
Tarehe: 24 Novemba 2024Mahali: Kijiji cha Mwandoya, Wilaya ya Meatu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Ndugu Shemsa Mohamed Seif anayeendelea na ziara yake ya "Siku Saba za Moto" ambapo leo zimesalia siku mbili kabla ya kumalizika. Katika ziara hii, Mwenyekiti alitembelea Kijiji cha Mwandoya kilichopo katika Wilaya ya Meatu, ambapo alikutana na wanachama, wapenzi wa CCM, viongozi wa Kata, na viongozi wa Matawi kutoka Kata ya Mwandoya. Kata hii ina vijiji saba, vikiwemo Mwandoya, Majengo, Makomangwa, Mwagumada, Mwakaruba, Inonelwa, na Igobe.
LENGO LA ZIARA NA MAFUNZO
Katika kikao cha ndani kilichofanyika, Mwenyekiti alisisitiza umuhimu wa kila kiongozi na mwanachama kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano wa pamoja ili kuhakikisha ushindi mkubwa wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji, na Vitongoji utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Aliwahimiza wanachama wote kujitolea kwa nguvu zao kwa kutumia kampeni ya "Nyumba kwa Nyumba, Kaya kwa Kaya, Mtu kwa Mtu, na Shuka kwa Shuka" ili kuhakikisha kura za CCM zinakuwa nyingi.
USHINDI WA CCM .
Mwenyekiti alisisitiza kuwa ushindi wa CCM ni jambo lisiloweza kuepukika, akieleza kuwa wananchi wanayo imani kubwa na viongozi wa chama na wanaamini kuwa CCM ndiyo chama pekee kinachoweza kuleta maendeleo endelevu na ustawi wa jamii.
PONGEZI KWA UONGOZI WA CCM TAIFA .
Aidha, Mwenyekiti alimtambua na kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi thabiti na juhudi kubwa anazozifanya katika ufunguzi kuhakikisha chama kinapata ushindi mkubwa katika kila uchaguzi, na kuhakikisha maendeleo ya nchi yanakwenda mbele.
Imetolewa na
Idara ya Siasa na Uenezi
Mkoa wa Simiyu .