Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Shemsa Mohammed: CCM Haitambeba Mtu Katika Uchaguzi Mkuu Ujao, 2025
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed amesema chama hicho hakitambeba mtu wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani na kuwa atabebwa kutokana na matokeo yake ya kukitumia chama hicho pamoja na wananchi.
Mohammed aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kichama mkoani humo ambayo inaendelea mkoa mzima wa ajili ya kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
"Chama chetu hakitarajii kuja kumbeba mtu wakati wa uchaguzi mkuu bali kazi zake ndizo zitakazo mbeba," alisema Mohammed.
Alisema ziara hiyo ambayo inafanyika Tarafa kwa Tarafa na jana Aprili 20, 2024 walikuwa Tarafa ya Nung'hu Wilaya ya Maswa ambapo walifanya kikao cha ndani kilichuhudhuriwa na viongozi wa CCM ngazi ya Kata, Matawi, Mashina, Mabalozi wa CCM, Wazee Maarufu, Viongozi wa Dini, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji,Kamati za Utekelezaji za Jumuiya zote ndani ya Chama.
Alisema kikao hicho kilienda sambamba na kusikiliza kero na changamoto za wananchi zilizoibuliwa na Viongozi hao ambapo Serikali ilizitolea ufafanuzi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa.
Wananchi wa mkoa huo wametumia ziara hiyo kumpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi kwenye Sekta za Afya, Maji, Miundombinu, Elimu, Nishati yenye thamani ya zaidi Sh. Bilioni 4.01 kwa kipindi cha Julai 2023 hadi April 2024.
Attachments
-
WhatsApp Video 2024-04-21 at 05.36.11.mp469.5 MB
-
WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.14.jpeg252.7 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.22.jpeg386.6 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.25.jpeg209.5 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.20.jpeg457.3 KB · Views: 8 -
WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.40.05.jpeg465.5 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.39.43.jpeg393 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.39.49.jpeg258 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-04-21 at 06.39.55.jpeg322.2 KB · Views: 7