Hakuna ardhi wala kijiji chochote isipokuwa mtume alipelekwa kuwaonya watu wake, ni mtu asiye na akili pekee atakayeamini kuwa mitume walitokea mashariki ya kati pekee.
amesema allah hali ya kuwa ametukuka: "....na hapana uma wowote isipokuwa alipita kati yao muonyaji.."
QURAN 35:24
Unachopaswa kukijua ni kuwa kuna mitume wametajwa kwenye quran na wengine hawakutajwa.
"Na mitume tuliokwisha kukusimulia habari zao hapo kabla, na mitume wengine ambao hatukukusimulia habari zao, na allah alizungumza na musa kwa maneno.."
Quran 4:164
shukran.