Elections 2010 Sherehe za kumuapisha Rais JK - Uhuru stadium DSM

Elections 2010 Sherehe za kumuapisha Rais JK - Uhuru stadium DSM

Kuna sumu ya kidini inaendelea humu ndani...stooooop....... nendeni kupiga mswaki vinywa vyenu vinanuka harufu ya kidini. Vinywa ni vichafu na vinafaa kulaaniwa na watanzania wote bila kujali dini zao.

Mungu ibariki nchi yetu

Wabariki watanzania wote bila kujali dini zao
 
Hii mpya sijawahi kuona JK anawasalimia wageni jukwaa la VIP, alipofika kwa Mwai Kibaki kamnong'oneza "Aisee yangu kidogo haikuwa kali kama yako japo sote tumeingia kwa mlando wa nyuma" alipofika kwa mkewe mama Salma kampa mkono bila hata kumuangalia (nilitegemea ange mkumbatia na kumpiga busu hajifunzi toka kwa obama? Au ana bifu na mkewe) na alipofika kwa Kabila akampa mkono na kumkumbatia...

hayo yote hata mimi nimeyaona na hapo kwa Salma nilitegemea angefanya hivyo......
 
Nasubiri hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa pia kina Prea, Gaijin, Aprin and Bht jamani mnapoteza mwelekeo wa hii thread mnajadili mambo irrelevant kabisa...
 
JK ndiye rais lakini kuna mtu anaweza kunisaidia kujua hasa nani alikuwa mshindi halali na kwa alama ngapi? Nina wasiwasi historia yetu itakuwa ya uongo siku zijazo!
 
Hata mimi nna mashaka. Haya hebu nambia mbona unapost via black berry? Uko gesti au kanisani/msikitini?
Leo nimeona bendera ya rias wa jamhur ya muungano wa Tanzania ikiwa na rangi nyekundu. Nilikuwa naomba ufafanuzi kwa anayefaham hiyo rangi inawakilisha nini ktk bendera ya rais.
tutajuamengi safari hii
 
Ndo JK kaamuru yapeperushwe hayo madege ya vita??? ana mtisha nani?? wangekua jasiri si wangeshuka huku chini? jamani lunch na dinner kwa JK full kitimoto na mazagazaga ya kichina yote, sijui ni haramu!!! hata sijui kwa kweli
 
JK ndiye rais lakini kuna mtu anaweza kunisaidia kujua hasa nani alikuwa mshindi halali na kwa alama ngapi? Nina wasiwasi historia yetu itakuwa ya uongo siku zijazo!

Tume ya uchaguzi ndio yenye mamlaka ya mwisho. Na ilimtangaza JK kama mshindi halali. Alama ziko kwenye tovuti ya NEC. Hata kama ni uwongo imeshatoka hiyo. Tugange yajayo. Historia haitasaidia.
 
Kwa nini ulitegemea Jk amdiss mkewe kivile Preta? Tufafanulie tafadhali

nina maana alipofika kwa Salma angemkumbatia na kumpa mabusu yenye bashasha, mbwembwe na madoido
 
huh .......hivi kila afanyacho Obama ndo kimekuwa s.i. unit?
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Anaanza kuhutubia!

MC anawataka wananchi wasitoke NJE YA UWANJA! baada ya Gwaride kutoka uwanjani!
 
Nasubiri hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa pia kina Prea, Gaijin, Aprin and Bht jamani mnapoteza mwelekeo wa hii thread mnajadili mambo irrelevant kabisa...

lakini mkuu mbona bado tupo ndani ya sredi
yote tunayozungumzia si yapo humo humo uwanjani?
 
Nasubiri hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa pia kina Prea, Gaijin, Aprin and Bht jamani mnapoteza mwelekeo wa hii thread mnajadili mambo irrelevant kabisa...
Samahani mkubwa. sikujua kuna tukio muhimu hv linaendelea, ndio nikafadhaika.
I am outta here
 
JK atahudumia muda si mrefu kuna watumbuizaji kama Marlaw, Msondo Ngoma na wasanii wa THT no wonder Kusanga and the company wanajikomba kinoma kwa JK
 
Tume ya uchaguzi ndio yenye mamlaka ya mwisho. Na ilimtangaza JK kama mshindi halali. Alama ziko kwenye tovuti ya NEC. Hata kama ni uwongo imeshatoka hiyo. Tugange yajayo. Historia haitasaidia.

Mtafuta lini somo la historia shuleni kama haina maana? Za NEC (aka CCM B) nazijua nazitaka halali!
 
ok nitaanza kiarabu kutoka kushoto kwenda kulia.....kwanza shekhe, pili wazee wawili, tatu tai nyekundu....vinanichanganya hivi ujue
Umechanganya kidogo hapo!.Kiarabu huwa kinatoka kulia kwenda kushoto.
Una mawazo mazuri lakini siku zote huvai vizuri.
 
nina maana alipofika kwa Salma angemkumbatia na kumpa mabusu yenye bashasha, mbwembwe na madoido

Preta,

Rais hufanya kile itifaki inachomtaka afanye! More or less of a ROBOT! Kama kumkumbatia Salma haimo kwenye RATIBA hawezi kufanya hivyo!
 
Back
Top Bottom