Waliofuraiya sherehe za uhuru kuahirishwa mwaka jana ndio hao hao waliofuraiya sherehe za uhuru kufanyika mwaka huu,swali wamefuraiya nn kufanyika kwa sherehe za uhuru mwaka 2017?Na kilichowafarahisha mwaka 2016 kuahirishwa ni nini?
Ndio maana Ile dhana ya kuruhusu uhuru wa maoni ni ya muhimu sana,wakati sherehe za uhuru mwaka jana zinaahirishwa wapinzani wa ccm waliweka wazi kabisa kuwa katika vitu ambavyo hawaviungi mkono ni pamoja na kuahirishwa kwa sherehe za uhuru,na walitoa sababu za msingi sana,lkn wapinzania waliambulia matusi mengi kutoka ccm,matusi ambayo hayana idadi,matusi mengine siwezi kuayaandiaka hata hapa jukwaani
Baadhi ya matusi ni kama haya
Wapinzani wanapinga kila kitu,wapinzani sio wazalendo,wapinzani wamekosa hoja,na kadhali,leo hii kile wapinzani walikisema mwaka jana ndio kilichofanyika dodoma,tunajifunza nini,kinachotakiwa watanzania ni kujenga utamaduni wa kusikiliza mawazo mbabadala,bila kupigana,bila kutukanana
Kila mwanadamu mungu amempa mawazo yake,na lazima atayasema tu