Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,951
- 9,977
Mkuu kwani inachukua muda gani kutoka America kufika Tanzania? Nimeona kuna ratiba ya kuzindua Royal Tour tarehe 28 April 2022 huko Arusha. Nina imani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yenye silaha ,Mh Samia Suluhu Hassan, atakuwepo siku ya tarehe 26 April 2022 kupokea heshima za kijeshi toka kwenye majeshi yetu.Kama ibara ya kwanza ya katiba ya JMT inavyotanabaisha ni kuwa Tanzania ni dola huru ambayo ni jamhuri ya muungano.
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ilizaliwa mwaka 1964 siku ya tarehe 26 mwezi wa nne.
Ibara ya 33 ya katiba ya JMT inatanabisha wazi kuwa rais ndie mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu.
Kusherehekea siku kuu ya kuzaliwa JMT huku mkuu wa nchi hayupo ni sawa kweli?
Hii inaleta picha gani?